Morogoro: Mpangaji afungiwa ndani Saa 27 na Mmiliki wa nyumba kwa madai ya kukiuka Notisi ya kuhama

Halafu watu ambao kufanikiwa kwao ni mashaka kwa kuungaunga huwa ni shida sana.
Yaani sijui ni hata ni Kwanini huwa inakuwaga hivyo.
 
Umesoma wapi kuwa mkataba umeisha?
Mwenye nyumba amevunja mkataba kwa sms
Mkataba ukivunjwa hata kwa sms lazima kutakuwa na sababu za msingi zitakazomlazimisha mwenye nyumba kufanya hivyo! Hata hivyo mpangaji anatakiwa kupewa notisi ya mwezi mmoja ili ahame ! AkΔ±kalidi notisi matokeo ndio hayo.
 
Naona kondoo anamfanyizia kondoo mwenzake.
 
Bongo sekta ya upangishaji nyumba imekaa kiduwanzi sana, mtu anataka malipo ya miezi sita wakati wafanyakazi karibia wote wanalipwa kwa mwezi, wiki au siku! Ni uhovyo tu ila ndio sekta huria hii kila mtu anafanya anavyoona inamfaa na mali yake.
Kimbembe ukitaka kuhama ghafla utaona huo usumbufu wake. Chukulia umelipa kodi ya mwaka after 2 months umepata uhamisho, unadai miezi 10. Utafurahia na roho yako hizo subiri subiri za mwenye nyumba. Atakulazimisha usubirie hadi apate mpangaji mwengine ndio arudishe hela na wengine kwa hasira anaweza asikupe miezi yote akisingizia ni umekatisha mkataba na blaa blaa zingine 🀣🀣🀣
 
Lazima mwenye nyumba akupe muda wa kujipanga na kutafuta nyumba nyingine(notice), tusiendekeze ujinga wa wenye nyumba kuendesha nyumba zao kiswahili swahili.
Mkuu upo sawa, masuala/Biashara ya upangaji nchini inaongozwa na sheria ya upangaji.

Kwa kusikiliza video hiyo hapo, maelezo ya mwenye nyumba mwenyewe, yeye ndiye aliyevunja mkataba tena kwa njia ya simu na SMS.

Mpangaji wake aliposisitiza kupatiwa notisi ya maandishi, inaelekea kwenye mkataba wao hakuna kipengele kinachoruhusu kuvunja mkataba kwa njia ya simu au SMS isipokuwa notice ya maandishi.

Inaonekana mwenye nyumba kusikia hivyo akaenda kumfungia ndani kabla hata hiyo notisi ya mdomo/simu/sms kuisha. Na mwenye nyumba hajasema kuwa anamdai kodi Mpangaji wake.

Huyu mwenye nyumba asipokuwa makini hiyo nyumba itakuwa mali ya Mpangaji wake huyo hivi hivi! Na hela ya usumbufu juu!!

Alitakiwa afuate utaratibu rasmi wa kumuondolea vitu ndani na pili amevuka mipaka kwa kumfungia Mpangaji wake ndani. Inaonesha alikuwa na nia mbaya.

Akianza kuhesabiwa gharama za usumbufu, madhara na hasara aliyomsababishia Mpangaji wake kwa muda huo wa masaa 27 na baada ya hapo.

Pia akihesabiwa hasara ya upotevu na uharibifu wa mali uliojitokeza wakati na baada ya kumtupia vitu njee asianze kulialia kupitia mbeleko ya kuonewa kwa sababu yeye ni mwanamke!!!

Mpangaji atulie, aviache vitu hapo nje, mpaka kesi iamuliwa, ndio mwenye nyumba atajifunza sawa sawa!!!

Mwana kulitafuta mwana kulipata!!!
 
Kwa maelezo ya balozi huyu mama mwenye nyumba anaonekana ni mkorofi sana.
Aisee mkorofi mnooo.
 
Mkuu, madam makubaliano yakiwepo utaratibu ni kufuata sheria.
 
Doh waswahili mnapenda kutumia mihemko aiseeee!
Mwenye nyumba hajasema kama anamdai jamaa kodi,bali alisema anataka abadili matumizi ya nyumba.
Mpangaji pia hakusema kama ameshindwa kulipa kodi,bali alidai mwenye nyumba alitaka kuibadili nyumba ama kuikarabati.
Sasa madai yenu ya kusema kuwa mpangaji mkorofi hakulipa kodi na aondoke mnayatoa wapi!??
Halafu mwenye nyumba bwege kweli,kuna notice gani ya SMS tena unamtumia mtu muda huo huo na unaenda kumtimua muda huo huo!??
Hata balozi anadai huyo mwenye nyumba hakuwa na barua yeyote ya kuhalalisha alichofanya.
Still mnamtetea mwenye nyumba!??
Waswahili banaaa!!

Mie ningekua ni jamaa namuanzishia kesi ikiwemo ya upotevu wa mali.
Tena kitendo cha kumfungia mtu ndani namfungulia kesi ya attempt murder case.
Pumbafu kabisa.
Je kama moto ungezuka ghafla humo ndani jamaa angenusurika vipi!?
Kumbe mijitu ya Mbeya ni mapang'ang'a hivi!?
 
πŸ™‹β€β™‚οΈπŸŽ―πŸ‘πŸ‘ŒπŸ‘πŸ€πŸ™πŸŽ–οΈ
 
Mkataba ukivunjwa hata kwa sms lazima kutakuwa na sababu za msingi zitakazomlazimisha mwenye nyumba kufanya hivyo! Hata hivyo mpangaji anatakiwa kupewa notisi ya mwezi mmoja ili ahame ! AkΔ±kalidi notisi matokeo ndio hayo.
Mkuu sheria ya upangaji haielekezi hatua za aina hiyo. Kasome ile sheria vizuri. Usiwapoteze wenye nyumba!!!
 
πŸ™‹β€β™‚οΈπŸŽ―πŸ‘πŸ‘ŒπŸ‘πŸ€πŸ™πŸŽ–οΈ
Sema kiuhalisia usithubutu ukapanga nyumba mwenye nyumba mwanamke umeula wa chuya.
Hata mamaangu mzazi ni mwenye nyumba ila naona balaa wanalopata wapangaji wake.
Sasa sijui hii kijinsia imekaaje?
 
Sema kiuhalisia usithubutu ukapanga nyumba mwenye nyumba mwanamke umeula wa chuya.
Hata mamaangu mzazi ni mwenye nyumba ila naona balaa wanalopata wapangaji wake.
Sasa sijui hii kijinsia imekaaje?
Mkuu ni tabia ya mtu, stress, kutojiamini na uelewa mdogo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…