Morogoro: Mpangaji afungiwa ndani Saa 27 na Mmiliki wa nyumba kwa madai ya kukiuka Notisi ya kuhama

Morogoro: Mpangaji afungiwa ndani Saa 27 na Mmiliki wa nyumba kwa madai ya kukiuka Notisi ya kuhama

Wakuu, huu ni Uungwana kweli?

Huko Marogoro mwenye nyumba kamfungia ndani saa 27 mpangaji kisa amekiuka notisi

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mmiliki wa nyumba Plot namba 149 BLOCK ‘A’ Kihonda Kilimanjaro, Dk. Lusako Mwakiruma ilioyopo Mtaa wa Kilimanjaro Manispaa ya Morogoro, amemfungia ndani mpangaji wake kwa saa 27 kisha kumtolea vitu vyake nje, kwa madai kuwa mpangaji huyo, Paschal Paulo alishindwa kupokea notisi ya kumtaka ahame kwenye nyumba hiyo ndani ya mwezi mmoja.
Pascal njoo huku umsaidie wajina wako, hii itakuwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa wananchi.
 
Unalinganisha vitu visivyo faa kulinganisha.
Ukienda kununua nyama unaanza kuandikiana mkataba na muuzaji?
Nyama biashara ya pesa ndogo wakati nyumba biashara ya pesa nyingi.
Ushaona Chama Cha wanunuzi nyama buchani pekee?
Kuna Chama Cha wapangaji pekee.
Tumia akili yako yote kabla hujasema lolote.
Kuna kupata shida katikati ya mkataba wako ikachangia kukosa pango kamili inapoisha pesa iliyo lipia tayari. Tusijitoe utu, hata taasisi za fedha wanasikiliza wateja wanaowadai na kuchelewesha malipo baada ya kupata tatizo.
Yan umeshindwaje kuielewa hoja yangu? Hoja ni kwamba mpangaji hawezi kufanya maamuzi ya ni lini alipe na ni kwa namna gani malipo hayo yatakuwa.
Halafu inakuwa mkuu; Yan Tatizo lilikuwa linasubiri ili lijitokeze wakati mpangaji anapotakiwa alipe kodi?? Kiustaarabu hatukatai tatizo linaweza kujitokeza; lakini Mlipaji/Mpngaji katika hali ya kawaida huenda kumwona mwenye nyumba na kujieleza na sio kumkwepa au kufanya uhuni. Kwani huyo Mpangaji hana namna au vyanzo vingine vya kupata fedha ili akalipe kodi??
Ukiona wewe mpangaji umebanwa sana kifedha ni vyema ukajinyenyekesha kwa mwenye nyumba hata kama itakubidi uweke rehani baadhi ya vitu vyako ili uendelee kujiaminisha na kusubiriwa hali iwe nzuri.
 
Unalinganisha vitu visivyo faa kulinganisha.
Ukienda kununua nyama unaanza kuandikiana mkataba na muuzaji?
Nyama biashara ya pesa ndogo wakati nyumba biashara ya pesa nyingi.
Ushaona Chama Cha wanunuzi nyama buchani pekee?
Kuna Chama Cha wapangaji pekee.
Tumia akili yako yote kabla hujasema lolote.
Kuna kupata shida katikati ya mkataba wako ikachangia kukosa pango kamili inapoisha pesa iliyo lipia tayari. Tusijitoe utu, hata taasisi za fedha wanasikiliza wateja wanaowadai na kuchelewesha malipo baada ya kupata tatizo.
Mkuu; Nilisahau hapo juu kukuambia kwamba Hakuna pesa ndogo. Kodi ya nyumba ni pesa kama pesa nyingine kwenye biashara. Kama ingelikuwa ni pesa ndogo si angelipa chap' sio mpaka afungiwe ndani kama utumbo.
 
Nimemwachia Kodi ya miezi 3 hajanilipa na bill ya maji ya miezi 6 nimelipia mwenyewe. Ili mradi tu aniachie gofu na pagale langu nifugie hata njiwa itanilipa.
Mkuu; Ulitumia Utaratibu gani katika kufanya hayo? i.e. Uliwashirikisha akina nani e.g. uongazi wa mtaa/kitongoji/kijiji ili iwe ni ushahidi dhidi ya Ukorofi wake au ulifanya kimya-kimya kama ulivyomfungia humo ndani kimya kimya?? (Utani lakini au ni kwa kicheko; Ukataji gogo ilikuwaje mkuu?
 
Niliamua kuwa mpole tu aondoke. Sipendi shari. Au ningeng'oa bati si eti
 
Hakuna haja ya kung'oa bati lakini sheria ingembana alipe malimbikizo na halafu kuondoka kwa hiari bila shuruti.
Tambua, mimi ni tukio lingine sio Morogoro alikofungiwa huyo kamanda, ila ni kweli, mpangaji wangu nilimruhusu andoke na deni la miezi mitatu na bill ya maji ya miezi 6, KIROHO safi, sijui balozi, au mashahidi sikutaka.
 
Ukilipwa kodi kwa haraka hakikisha pia nyumba inakarabatiwa, maji yapo na unatoa notice stahiki ukitaka mtu ahame
Yeah. Haki iendane na Wajibu. Mwenye nyuma awajibike kwa yale yanayompasa ili kuhalalisha Malipo ya kodi na Mpangaji naye alipe kodi ili kwa kodi hiyo kumwezesha mwenye nyumba atimize yale yanayostahili.
 
Na wewe una m
Angekuwa Salum au Asha kafanya hivyo, tungeipata Waislam wote humu JF na Tanzania nzima.

Lakini kwa kuwa kafanya kondoo mwenzao wa kilimanjaro, wote kimyaa.
Na wewe una majini kama vile Shehe Sule anasema waislam na hata mtume alikua na majini!?
 
Back
Top Bottom