Morogoro: Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', akamatwa na Polisi

Morogoro: Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', akamatwa na Polisi

Baraza la sanaa la taifa ndilo linawajibu wa kushughulika na kazi za sanaa na wasanii ikiwemo content ya kazi zao

Msanii akitoa kazi inayokuwa na content isiyo na maadili au isiyokubalika na jamii ya watanzani, ni BASATA ndio wanatakiwa kushughulika na msanii husika hata kumpatia adhabu inayostahili ikiwepo kuifungia kazi husika na msanii mwenyewe

hii ni tofauti kwa Nay wa Mitego!
kwa nini Amekamatwa na polisi ilhali BASATA ipo?
hapa jeshi limeingilia majukumu ya Basata!
ni nani katoa order ya Nay kukamatwa bila ya Basata?
Yule yule aliye mpa ruhusa mtu asiyejulikana kumuonesha kitambulisho Nape
 
Weshaona fashion sikuizi kutukana, wameharibu jf sikuhizi nayo hovyo tu, huyo wanayemuiga yuko States na hawezi kanyaga Tz, muda si mrefu jf tunaipoteza maana naona hata mods ni kama wanatumika.
Unakerwa na upande mmoja wa shilingi?Chanzo cha haya in nini?
 
Msanii wa kizazi kipya Emanuel Elibarik alimaarufu kama NEY wa mitego amekamatwa asubuhi hii huko morogoro

View attachment 486993



Sehemu ya wimbo wa Ney wa Mitego:

=======

Hivi Uhuru wa Kuongea bado upo? Siamini nchi inaendeshwa kwa kiki!
Nasikia kuna viongozi wamefoji vyeti? Wapooo! Mheshimiwa hivi unamjua Bashite kutoka Kolomije? We si Dokta wa kutumbua majipu?

We mtu gani sasa? Hutaki kushauriwa, hutaki kukosolewa? ...Naona kichaa kapewa rungu! Hahahaha

Mmh. . Hapa nae kaenda mbali. Sawa message sent. Lakini kwa jinsi yeyote asingepona, angechuja kidogo maneno yake. Pamoja na yote atakayo pambana nayo asante sana kutufikishia ujumbe. Inahitaji ujisiri!
 
Mfano nitunge nyimbo kuhamasisha mapinduzi au ugaidi

Au mauaji kwahiyo unataka polisi wasiingilie kisa wao sio basata

Sijazungumzia Ney hapa ila nakuonyesha taswira ,polisi wanayo haki ,mbona akina sheikh ponda walikamatwa na polisi kisha kuhojiwa kwahiyo Polisi waliingilia kazi ya bakwata

Mwandishi wa habari anapotumia kalamu vibaya labda kuhamasisha vurugu polisi watamkamata kumhoji huyo mwandishi wa habari na kumhoji licha ya kuwepo chombo cha kuwasimamia wandishi,

Basata haiwazui polisi ,kazi ya polisi ni kuhoji na kulinda usalama siyo kufungia wimbo basata ndio wenye mamlaka ya kufungia wimbo au kumpiga ban au fine msanii
 
Mfano nitunge nyimbo kuhamasisha mapinduzi au ugaidi

Au mauaji kwhiyo unataka polisi wasiingilie kisa wao sio basata

Sijazungumzia Ney hapa ila nakuonyesha taswira ,polisi wanayo haki ,mbona akina sheikh ponda wakikamatwa na polisi kwahiyo Polisi waliingikia kazi ya bakwata
Mleta mada hana uelewa huo.
 
Weshaona fashion sikuizi kutukana, wameharibu jf sikuhizi nayo hovyo tu, huyo wanayemuiga yuko States na hawezi kanyaga Tz, muda si mrefu jf tunaipoteza maana naona hata mods ni kama wanatumika.
Hujajibi swali kamtukana nani?
 
Tafuta Comments za Tangu anaingia na kuanza sakata la Sukari nilimpinga lakini haikunizuia kumuunga Mkono anapopatia!

Hata Kesho akipata kwny Jambo lolote sitosita kumuunga Mkono!

Sina utaratibu wa kumuunga Mkono Mtu kwa kila Jambo Kama ambavyo sina kawaida ya kumkosoa Mtu kwa kila Jambo!

Hata Lowassa huwa namuunga Mkono sana Mtu , mfano alipoweka Siasa pembeni na kuhudhuria Golden Jubilee ya Mkapa ya kutimiza Miaka 50 ya ndoa
Jibu murua hili mtu mwingine angeweza kutoa povu na pengine kuyakana maandiko yake ila swali limejibiwa kwa hoja iliyoshiba na wengi wetu hushindwa jambo hili mtu kajikita penye kuponda tu au kusifia tu. Hongera ndugu kwa kuweka rekodi sawa .
 
Bado kuna watu wanategemea viwanda vitajengwa nchi hii basi wavivu wa kufikiria, wakujenga viwanda ndo hao akina manji mnaowanyanyasa, Gwajima alikuwa na mpango wa kununua treni sasa mnamtengenezea vipindi vya kumzalilisha atapata wapi moyo wa kuwekeza nchi hii. Serikali ya awamu hii ya tano ni ya vioja na kutafuta kiki.
 
Autro yake ndio imeniua kabisa anasema
"Mtu gani wewe hupendi kushauriwa,hupendi kukosolewa umelogwa wewe unajiona ndugu yake Na yesu"

Kweli hapa akichomoza sizonje atakuwa mpenzi WA mungu kwa kusema kweli..
 
Back
Top Bottom