Brother ngoja ni share kidogo kuna jamaa alimkimbia mke wake huko mikoani akaenda Dar baada ya kufika huko na kukaa miaka mitatu akakutana na binti mmoja katika haya makanisa yetu ya kilokole basi yule baba akafunga ndoa kabisa na huyo binti wakadumu kwenye ndoa kwa miaka mitatu..
Baada ya miaka hiyo Yule mwanamke wa ndoa ya awali akasikia mshikaji alishaoa na anaishi na mke mwingine Dar dada wa watu akafunga safari hadi Dar kweli akathibitisha kuwa mshikaji alishaoa miaka mitatu iliyopita.
Yule mama alienda mahakamani kufile rehabilition ya ndoa yake na kuwa anataka ndoa yake walipelekeshana mahakamani mwisho wa siku yule aliyevamia ndoa aliambia ndoa ya pili ni batili kwa hiyo mke wa wali anahaki na ndoa yake na ndoa ya pili ilitenguliwa..
Kumbuka huyu hakudai fidia ya fumanizi yeye alitaka ndoa yake tu na huyo binti haki haikumuungali.
Kwa hiyo Angalizo kwa nyie mabinti mnaotaka kula chakula kilichokwisha pikwa hii casde itawaharabia maisha yenu na soon tutaona ongezeko la vichaa mirembe