Morogoro: Stand ya Daladala kuhamishiwa kilomita 2+ kutoka katikati ya mji ni kero kwa Wananchi

Utazoea tu usijali. Kelele za lawama kwa hiki kipind cha mwanzo ni kawaida. Muda wote stendi inajengwa unaona umekaa kimya tu sahivi unalalamika ulitegemea stend ikikamilika wataifanya soko
 
Utazoea tu usijali. Kelele za lawama kwa hiki kipind cha mwanzo ni kawaida. Muda wote stendi inajengwa unaona umekaa kimya tu sahivi unalalamika ulitegemea stend ikikamilika wataifanya soko
Ulitangaza kuwa unajenga stand huko porini?
Uliogopa nini kutangaza kabla hujaanza ujenzi?
 
Huyo anaongelea stendi ya daladala wewe unakuja na stendi ya mabasi ya ruti ndefu. Mavi ya bata......
 
Hili nilishalisemea pia moja ya maamuz ya hovyo kabisa ni kujenga stend moja ili kuaccomodate mji mzima , ukiangalia na ukuaji wa miji ulivyo Kasi , ndani ya miaka 15 Tu stend inakuwa imezidiwa na inakuwa outclassed..... Dsm inatakiwa iwe na stend tatu , bagamoyo Road iwe na stend yake nzuri Tu ya kisasa , Kilwa Road pia iwe na stendi na yenyewe , bila kusahahu morogoro road pia kuwe na stend ya kisasa ....... Na pia kuwe na stend za daladala kama Ile ya mbezi na mawasiliano kila baada ya km 5 au nane achilia mbali vituo vidogo vidogo vya kushusha abiria Kwa barabara zinazoingia mjini ...... Mwanza Wana stendi kuu mbili Kwa barabara kuu zinazoingia na kutoka mjin , kulikuwa na maamuz ya hovyo pia ya kuzipeleka pori nashukru Kwa watu waliopambana mpak zikabaki maeneo ya mjini ila wakaziboresha na kutengeneza stendi ndogo ndogo along the road Kwa ajili ya kushusha na kupakia abiria ,....

Unapohamisha hamisha stend kupeleka pori unavuruga uchumi wa watu waliowekeza pale stend , na kuleta adha kubwa Kwa wasafiri na kuongeza gharama , hali ikija kukaa pouw tena unakuta stend ulikohamishia nako kumebanana unavuruga tena uchumi kule, na kupeleka porin yaan unakuwa mtu wa kutengeneza na kuvuruga ....ifikie hatua tuelewe stend ni mahali pa kushusha na kupakia abiria huwez kusema et magar yote yatatosheka na stend moja kubwa hamna kitu
 
Kwa ufahamu wangu hiki unachoshauri ndicho kitakachofanyika
 
Wamekalia kuvimbiana mitumbo tu hata akili ya kupanga root za daladala au bajaji hawana

We mtu anatoka hilo stendi lao kuu la mafiga akifika mjini hakuna kituo cha kushushiwa,matokeo yake madereva wa mabasi na bajaji wanakimbizana na mapolisi tu,sasa unajiuliza wawashushie abiria angani au,pumbafu
 

Ueongea point nzuri sana, kama mamlaka husika zingekuwa zinawashirikisha wananchi kwa ujumla wao kutoa maoni kabla ya kutekeleza miradi inayowagusa wao moja kwa moja ingesaidia sana kuepuka maamuzi ya hovyo wanayofanya viongozi, maamuzi hayo ya hovyo yanafanywa kwakuwa wao wenyewe hawatumii huduma hizo kwakuwa wanatumia usafiri wa serikali na hivyo inakuwa vigumu kuonja kero na adha zilizopo
 
Mkuu naunga mkono.
 
Ulitakeje tubomoe nyumba za msajili?
 
Issue ya usafi wa vyooni unaanzia kwetu watumiaji ....tambua sisi wabongo ustarabu ni zero

Ova
 
Haitakuwa haki, fikiria wakizuia magari binafsi yasifike katikati ya mji yote yaegeshwe masika na fire, utajisikiaje kutembea kwa miguu mpaka ufike katikati ya mji
Huo mji upo shaghalabagala hata system ya mitalo ni mibovu,
Mvua ikinyesha hapo stendi huwaga kuna mafuriko,

Bora wamehamisha tu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Daladala ilikuwa ni kero pale, watumiaji wa daladala sio wastaarabu kama sie wa usafiri wa private. Watuachie sie lile eneo tuwe tunapaki ndinga zetu.
 
Mtazoea tu mkuu ni swala la ku change mindset ,mbona haulalamiki kile kituo cha Treni ya reli ya kati kilipo,ni mbali na makazi ya walio wengi hapo Morogoro,mwanzoni inakuwa ni usumbufu ila baadaye utakuja kukubaliana na hiyo mipango...
 
Mtazoea tu mkuu ni swala la ku change mindset ,mbona haulalamiki kile kituo cha Treni ya reli ya kati kilipo,ni mbali na makazi ya walio wengi hapo Morogoro,mwanzoni inakuwa ni usumbufu ila baadaye utakuja kukubaliana na hiyo mipango...

Umbali is not a serious issue, wanahitajika kuweka kituo kimoja cha kushusha na kupakia abiria katikati ya mji
 
Issue ya usafi wa vyooni unaanzia kwetu watumiaji ....tambua sisi wabongo ustarabu ni zero

Ova
Angalia mfano wa vyo vya kulipia tena vya Halmashauri vinaangaliwa kwa makini.
Lakini vyoo vinahitaji maji,sabuni,tissue n.k
 
Naona mto mada alikuja na jazba na roho mbaya, huwezi waambia watu eti imehamia sua, Unaijua SUA wewe au unaropoka tu!!!
 
Nchi hii haijawahi kuwa na mipango , Tulipohamishwa kutoka Mnazi mmoja na Kisutu kupelekwa ubungo tukajua yameisha , sasa ni hivi ni Mbezi Luis , lakini nakuapia haitoisha miaka mingi tutapelekwa Kibaha .
[emoji3][emoji3][emoji3]soon mtafika moro ... Halafu hata miaka 30 haijafika tangu waihamishie ubungo .. inavyoonekana kila kiongozi akikaa madarakani anatafuta chocho la kupiga hela
 
Stendi kuwa katikati ya mji ni kero tu, ndo kukua kwa mji, km 2 ni karibu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…