Naafikiana nawe kuwa stand haikuwa inatosha lakini
- Pamoja na changamoto hizo hapakuwa na effective utilization of resources mfano ilikuwa ni kawaida kabisa askari wa usalama barabarani kutosimamia mabasi yanayoingia na kutoka stand na hata baadhi ya madereva walikuwa wanavunja sheria mbele yao na wao hawakuwa na meno kwakuwa baadhi ya daladala ni zao.
- Hapakuwa na proper planning ya namna sahihi ya kuondokana na hizo changamoto, kwa mfano daladala za vijijini kama Mngeta, Mzumbe nk zilikuwa zinaegesha kwa masaa mengi stand tangu asubuhi mpaka alasiri bila sababu.
- Route zilizoanzishwa zilitakiwa zizingatie mahitaji ya muhimu ya wananchi katikati ya mji kama vile hospitali, kituo kikuu cha polisi, ofisi za Manispaa, mabenki, mahakama nk ili kuwaondolea usumbufu wa kutembea umbali mrefu (kutoka Masika hadi katikati ya mji na kutoka katikati ya mji hadi Misitu/maliasili/Simbaoil hasa wakati wa mvua na jua kali.)
Kumbuka wanaoumia ni wananchi wa kipato cha chini, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanaosoma shule za serikali ambao wanatoka kwenye familia duni, mathalani, mwanafunzi anaishi Kihonda, anasoma Sumaye Bigwa, Kola Hill, Lupanga na Kingalu anashushwa Masika, anatembea kwa miguu mpaka Manispaa akavizie usafiri wa Bigwa, au mwanafunzi huyo anatoka Sumaye Bigwa, Kola Hill, Lupanga na Kingalu, anatembea kwa miguu mpaka Misitu/maliasili/Simbaoil kwenda kusubiri usafiri wa Kihonda kwa sababu Masika wapo askari wanazuia mabasi kuchukua abiria.
- Kusema ukweli wananchi/wanafunzi wa kipato cha chini ndiyo wanateseka, lakini endapo wanaopanga hizo route na hivyo vituo vya kupakilia na kushushia abiria wangesafiri kwa public transport kwa angalau wiki moja huenda wangeelewa kinacholalamikiwa, lakini kwakuwa wao wako kwenye magari binafsi, hawatakaa waelewe.
- Kama viongozi husika wangekaa na wananchi wanaotumia daladala na kujadiliana nao, wachukue concerns zao na wazifanyie kazi ingekuwa jambo la busara zaidi kuliko kuwashinikiza wananchi kukabiliana na hali mbaya ya mfumo wa usafiri iliyoamriwa kwa interests zao binafsi.