A
Anonymous
Guest
Eneo la Mazimbu Road, Morogoro, katika barabara kuu ya Dodoma, limekuwa na changamoto ya zebra za kuvukia barabara kufutika. Eneo hilo hutumiwa na wananchi wengi, hasa wanaotokea au kuelekea kwenye njia inayounganisha na kituo cha SGR na kuingia kwenye barabara kuu.
Suala hili limekuwa changamoto kubwa, hasa ikizingatiwa kuwa barabara hiyo hutumiwa na mabasi na magari makubwa. Baada ya zebra kufutika, imekuwa vigumu kwa madereva, hasa wa magari makubwa, kusimama katika eneo hilo na kutoa nafasi kwa wananchi kuvuka barabara kwa usalama.