Morrison akasirika, alalamikia timu ya taifa “Mnaita wachezaji wa Azam FC wakati timu yao inafungwa na Simba”

Morrison akasirika, alalamikia timu ya taifa “Mnaita wachezaji wa Azam FC wakati timu yao inafungwa na Simba”

Hajui tu jinsi alivyochafua CV yake. Hana msimamo kwake pesa kwanza mengine baadae
Wewe mbona CV yako imechafuka lakini bado ukapata huyo uliyenaye leo!!???
Mungu ni Mwema wakati wote kwa watu wote.
 
Na kweli ile timu kwa ni mwendo wa connection
Morison anaweza kuperform vizuri kuliko many players waliomo kikosini
 
Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison ameshutumu maamuzi yanayofanyika katika kuita wachezaji wa timu ya taifa lake la Ghana kwa madai kuwa kuna ubabaishaji mwingi na wanatana kwa kujuana.

Morrison amesikitishwa na kitendo cha kuonekana anadharaulika wakati amecheza katika klab kadhaa kubwa Arika ana kufanya vizuri huku wanaoitwa wengi ni wale ambao wanaonekana kuwa na uwezo wa kawaida kuliko yeye.

Amedai kuwa hiyo inafanyika kwa kuw ayeye hana watu wanaomuunganisha na timu yake ya taifa na kuamini kuwa kutouitwa kwake siyo suala la uwezo bali ni connection.

“Mnaita watu wengine kwa kuwa wanachea Ligi za Ulaya na nje YA Afrika, mmeifanya timu ya taifa ya Ghana kama biashara ya familia, hauwezi kuitwa lazima uwe na koneksheni.
View attachment 2164567
“Hao mnaowaita wana umuhimu gani wa kipekee?? Mnadharau baadhi ya ligi nyingine za Afrika na kuwachukua wachezaji wa ligi ya ndani ambao hata timu za hazipo Champions League[emoji2363]

“Nilichagua jezi namba 3 iliyokuwa ikivaliwa na ASAMOAH GYAN kwa kuwa nilikuwa namkubali lakini hilo nalo halikuwahi kuthaminiwa, bora nielekeza nguvu zangu Simba.

“Nimeshazungumza na watu wa Shirikisho nimewaambia nimecheza AS Vita, Orlando Pirates, Yanga na sasa nipo katika klau kubwa Tanzania, Simba lakini sijawahi kufikiriwa.

“Mnasema ligi ya Tanzania siyo nzui kiivyo, lakini ni nyie ndiyo ambao mmeita wachezaji wawili kutoka Azam FC wakati ni timu ambayo inafungwa na Simba na inazidiwa na Simba, hiyo ni kwa kuwa wana marafiki kwenye Shirikisho,” anasema Morrison.
Angekuwa raia wa Senegal angeitwa maana kocha ni Mla Bangi mwenzie.

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Punguza uzungu unavua bukta unatembea na pumburiko nje is not awa culture pls
 
Upo sahihi mkuu ila lazima kina Mwajuma Ndala ndefu.Waje kukupinga.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
Hao wapo tu ndugu yangu ,japo Morison anachukuliwa kama mtu asiyejitambua kwa baadhi ya watu bado ukweli unabaki kuwa kuna nyakati nyingi tu anaongea points za msingi sana , rejea kesi yake dhidi ya Yanga
 
Kwa ufupi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ghana cha SASA sijaona wakumweka benchi BM3 NASEMA SIJAONA WA KUMWEKA BENCHI BM3
 

JICHO LA MWEWE: Eti rafiki yangu Morrison analilia timu ya Taifa Ghana​



morispooic

Summary

  • NEYMAR alishakuwa tajiri kabla hajaenda Ulaya. Mwaka 2012 wakati akicheza klabu ya Santos alishanunua boti ya kifahari (yatch) yenye thamani ya dola 10 milioni. Ni pesa nyingi. Ina maana tayari alishakuwa tajiri kwa kucheza Ligi Kuu ya Brazil.
ADVERTISEMENT

New Content Item (1)

By Edo Kumwembe
More by this Author

NEYMAR alishakuwa tajiri kabla hajaenda Ulaya. Mwaka 2012 wakati akicheza klabu ya Santos alishanunua boti ya kifahari (yatch) yenye thamani ya dola 10 milioni. Ni pesa nyingi. Ina maana tayari alishakuwa tajiri kwa kucheza Ligi Kuu ya Brazil.

Hata hivyo, inasemekana mambo mawili yalisababisha aende Ulaya mwaka 2013 huku akisaini klabu ya Barcelona katika uhamisho ambao lilikuwa suala la muda tu kwa sababu lazima Neymar ilikuwa aende kucheza Ulaya.

Kulikuwa na sababu mbili. Wabrazil walimlazimisha akacheze Ulaya. Sababu ya kwanza ni kwamba haijalishi angeonyesha kipaji cha namna gani akiwa Brazil lakini kamwe asingefikiriwa kuwa Mwanasoka Bora wa Dunia kama angeendelea kucheza kwao.

Haijalishi kama angetwaa ubingwa wa Amerika Kusini (Copa Amerika), haijalishi kama angechukua ubingwa wa klabu bingwa kwa mataifa ya Amerika Kusini (Copa Libertadores), haijalishi kama angechukua Kombe la Dunia akiwa na Brazil. Kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia inabidi ucheze Ulaya.

Ni ngumu kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia kama hauchezi katika ligi kubwa Ulaya. Ni ngumu pia ukiwa unacheza Amerika Kusini, Afrika, Asia wala kule juu Australia. Inabidi ukaonyeshe kipaji chako Ulaya katika ligi ngumu dhidi ya timu imara.

Sababu nyingine iliyowasukuma Wabrazil wamwambie Neymar akacheze Ulaya ni ukweli kwamba walitaka akomae katika soka la Ulaya kabla ya kuiwakilisha Brazil katika michuano ya Fainali za Kombe la Dunia nchini humo mwaka 2014. Ndio maana Neymar aliondoka mwaka mmoja kabla ya Kombe la Dunia. Walitaka akatoe ushamba Ulaya na acheze mara kwa mara kabla ya kuwa mchezaji wao muhimu zaidi katika michuano hiyo ambayo ingefanyika nchini kwao.

Nimekumbuka kuhusu Neymar baada ya majuzi kuendelea kumsoma Bernard Morrison ambaye amekuwa akililia kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ghana wakati huu akicheza soka Afrika Mashariki. Nimecheka kidogo.

Kuna mwandishi mmoja kutoka Ghana huwa anakuja Tanzania kutazama baadhi ya mechi za Simba. Inaonekana kama vile ana kampeni maalumu na rafiki yake Morrison kuhusu staa huyu kuitwa timu ya taifa ya Ghana.

Kuna ukweli mwingi ambao Morrison anausahau. Amekuwa akiwaponda kina Andre Ayew na mdogo wake Jordan Ayew kama vile wapo nyuma yake kisoka naye kupitia hizi mechi dhidi ya Coastal Union anaona kama anastahili.

Mpira una viwango vyake. Kuna Waghana zaidi ya 100 ambao inawezekana kiasili hawafikii kipaji cha Morrison, lakini wanacheza soka katika nchi ambazo ligi zao ni bora kuliko Tanzania. Ghana wanakuchaguaje wakati unacheza Tanzania?

Inaweza kuwa ngekewa kama unacheza nafasi fulani ambayo wana matatizo nayo lakini sio nafasi ya Morrison. Kule Afrika Magharibi makipa wengi wanaocheza ndani ya Afrika au ndani ya nchi zao huwa wanapata bahati ya kuitwa katika vikosi vyao. Kuna makipa wachache wa Afrika wanaotamba nje ya nchi zao au nje ya bara la Afrika.

Rafiki yangu Morrison ananichekesha. Nimepitia orodha ya Waghana wanaocheza timu ya taifa nje ya watoto wa Abeid Pele nimekutana na watu wanaocheza Ligi Kuu za Ujerumani, Ubelgiji, Ufaransa, England na kwingineko. Alitaka aitwe kwa sababu gani? Ulazima huo unatoka wapi?

Mchezaji anaweza kuwa na kipaji cha kawaida, lakini kama anacheza katika ligi kubwa basi anastahili kupata nafasi. Anacheza katika ushindani mwingi kila wikiendi. Huo ndio ukweli wa kawaida kwa makocha wanaofundisha timu za taifa.

Rafiki yangu Morrison alie kwa kujilaumu mwenyewe tu. Kipaji chake kipo wazi na wala hakustahili kuwa hapa. Kwa namna alivyo au anavyocheza alistahili kuwa huko Ulaya miaka mingi iliyopita, lakini ameendekeza kuwa mchekeshaji zaidi ya kuwa mwanasoka.

Sio kwa bahati mbaya kwamba yuko hapa. Sio yeye tu. Kuna wanasoka wengi maridhawa wa kigeni katika ligi yetu ambao sio kwa bahati mbaya wapo hapa. Kuna ambao wapo hapa kwa sababu umri umewapita isipokuwa wanamudu tu kucheza hapa, kuna ambao ni walevi tunawajua hawawezi kucheza ligi ‘serious’ zenye ushindani.

Kuna wale wenye utovu wa nidhamu akiwepo yeye mwenyewe. Sio kwa bahati mbaya kwamba tunao wanasoka wengi wa kigeni mahiri na wanamudu kucheza Tanzania kwa sababu ya mfumo wa soka letu. Wasingeweza kucheza nje na kutamba.

Morrison anafahamu fika kitu gani cha kufanya ili aweze kuitwa timu ya taifa ya Ghana. Anajua kwamba anawadanganya Watanzania kwamba anaonewa lakini ukweli anaujua moyoni. Kucheza Simba au Yanga katika mechi za CAF hakutoshi kukufanya uitwe timu za taifa za Ghana, Cameroon, Ivory Coast, Mali au Senegal. Ndio maana miaka nenda rudi tupo na Serge Wawa Pascal na wala halalamiki.

Kuna mahala ambapo alipaswa kujipima kweli kweli kiasi cha kuhalalisha kuitwa timu ya taifa ya Ghana. Ikumbukwe kuwa hata Simba yenyewe hajaikamata vya kutosha kuweza kuhalalisha kuitwa katika timu ya taifa ya Ghana.

Ukiwataja wachezaji watatu muhimu kwa Simba kwa sasa yeye hayupo. Inakuwaje analilia kuichezea Ghana? Analeta udanganyifu kwa sababu anajua kwamba mashabiki wetu huwa wanapenda kuambiwa vitu wanavyotaka kusikia.

Hata hawa rafiki zetu Zambia kuna nyakati ambazo mchezaji wao alikuwa akija Tanzania kuwa wanagoma kukuita katika timu ya taifa. Davis Mwape alipokuja Yanga wakaacha kumuita timu ya taifa. Sielewi kwanini wamebadili msimamo wao kwa Clatous Chama na Rally Bwalya. Labda kwa sababu Simba inafika mbali katika michuano ya kimataifa
 
Back
Top Bottom