mnajadili mambo kiwepesi wepesi kiasi kwamba mnalisha watu matango pori tofauti na uhalisia ulivyo!Hii ni changamoto sana kwa JF!
Nilikuwa namsikiliza US security advisor pamoja na wataalamu kadhaa kupitia runinga!
Walichosema ni kuwa huwa kuna intelligence sharing kati ya vyombo vya usalama i.e CIA na FSB!Lakini kutokana na tension kuwa kubwa kati ya Russia na US juu ya Ukraine,kumekuwa na kutokuaminiana!US alitoa tu taarifa Russia kuwa kumepangwa tukio la kigaidi katika sehemu ya mikusanyiko wiki 2 zilizopita,akasema tukio hilo litatokea within 48 hours!Hakutoa additional information juu ya wahusika au intel hizo kazipataje kutokana na kutokuaminiana na Russia hivyo kutoa source ya intel ni Risk!
Upande wa Russia kukawa na hisia kuwa huenda US anafanya michezo ya propaganda ili kujenga hali ya hofu kwa watu wa Russia!Na masaa 48 yakapita kweli bila shambulio kutokea!Tukio limekuja kutokea wiki 2 baadae!
Fikiri kama leo Russia ampe US tip kuwa kunaweza kutokea shambulio dhidi ya ndege za abiria ndani ya US!Russia asimpe details US za kumshawishi kuwa kuna tukio kama hilo!Je,US atafanyaje?US anaweza kuground ndege zote zisipae kwa muda usiojulikana?Based on what?A tip with no evidence from unfriendly country?
Haya mambo sio mepesi kama wengi humu mnavyoyachukulia!