mrangi
JF-Expert Member
- Feb 19, 2014
- 88,759
- 123,368
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona wapo wengi tuNawaambien vijana wa humu, wanaojiita watoto na wana miaka 28-30 like hawajui kwamba kufumba na kufumbua 50 hii hapa kwenye kona na wamejaa mazima na mali yoyote ya maana hawana,mwisho wanaishia kuua ili kugombea mali.
Kijana usipokua makini, wewe ndio huyu huyu bwana baada ya muda sio mrefu
Afya ya akili hasa kwa umri huo ni muhimu sana, maana alishakosea na umri umeshakqenda na wadogo kwakwe wamefika mahala yeye anakuwa nusi wazimu.Miaka 54 bado anagombea mali za urithi.....duh!!!
Aloo i was never and will never be the sharpest tool in the box😝Aisee!
Uwezo wako wa akili ndio umekomea hapo??
Miaka 54 kugombea mali tena mashamba ni tatizo kubwa sana, tena na Bibi wa miaka 74?Huko moshi jamaa wa miaka 54 amemuua mama yake wa miaka 74 kwa sababu ya ugonvi wa mali alizoacha baba ama mume wa marehemu ambae ndio baba wa mtuhumiwa.
Marehemu aliacha mashamba, hayo ndio yameleta mgogoro hadi jamaa akaamua kumuua mama yake.
Matukio ya hovyo ya watu kuua wazazi wao kisa mali yanashamiri sana Kilimanjaro.
---
Adela Mushi (74), mkazi wa Okaseni, kata ya Uru kusini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro anadaiwa kuuawa kwa kunyongwa na kisha kukatwa na shoka sehemu ya usoni na mwanaye, anayedai mali zilizoachwa na marehemu baba yake.
Inadaiwa kuwa mtoto wake huyo mwenye umri wa miaka 54, alifanya tukio hilo usiku wa Septemba 23, 2024 na kisha kutelekeza mwili wa mama yake ndani ya chumba chake alichokuwa anaishi.
Mwili wa mama huyo ulikutwa ukiwa umelazwa kifudifudi huku shingoni kukiwa kumefungwa kipande cha kanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa jeshi hilo linamshikilia mwanaume huyo kwa mahojiano zaidi.
“Septemba 23, 2024 usiku wa saa 4, maeneo ya Uru Okaseni, mwanamke ajulikanaye kwa jina la Adela Dominick Mushi, aliuawa kwa kupigwa na kitu butu kichwani kisha kunyongwa kwa kutumia kipande cha kanga na mtoto wake aitwaye Nemes Dominic,” amesema Kamanda Maigwa.
Kamanda Maigwa amesema chanzo cha mauaji hayo kinachunguzwa , lakini wawili hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu wakigombea mashamba na mali za marehemu.
Mwananchi
Inashangaza sana,Kabisa unainua mkono kumuuwa mama yako mzazi?tena kwa mali za kurithi?
Ni huzuni kubwa sana hii
Miaka 54 bado anagombea mali za urithi.....duh!!!
TUkazene, ukachezee mvua ya maisha na una miaka 54, wewe gerezan hutoboi hata miaka 10Mbona wapo wengi tu
Ova
Unapotaka wazazi wakupe mali wao hizo mali waliziokota?na wewe kwanini usitafute zako leo ukaanze kuwazia mali za baba yako!!!Maisha magumu wazazi acheni ujinga wapeni watoto wenu mali wakasake life
Ajira hakuna
Kweli mkuu tujipange mapemaNawaambien vijana wa humu, wanaojiita watoto na wana miaka 28-30 like hawajui kwamba kufumba na kufumbua 50 hii hapa kwenye kona na wamejaa mazima na mali yoyote ya maana hawana,mwisho wanaishia kuua ili kugombea mali.
Kijana usipokua makini, wewe ndio huyu huyu bwana baada ya muda sio mrefu
Umaskini na tamaa. Miaka 54 bado unahitaji kurithi Nini kutoka mzazi?!😡😡😡kuna nn huko?
Ni kwa vile tu Mungu alifanya kesho kuwa fumbo, mimba ya huyo jamaa angeichoropoa.Alimzaa akiwa na miaka 20
Bila shaka Muuza Kangala atakua anamjua huyu mtuhumiwa.Kapoteza ramani 54 bado yupo home....means hana familia huyo..ni design ya walevi wanywa mataputapu.
Ana IQ ya kuku huyu!Aisee!
Uwezo wako wa akili ndio umekomea hapo??
Sisi wazazi tulipewa mali na nani? We si unayo mali na uma uza kwa 10M tu?Maisha magumu wazazi acheni ujinga wapeni watoto wenu mali wakasake life
Ajira hakuna