Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Muhim sana chiefKweli mkuu tujipange mapema
Nami ndicho kimenishangaza aiseeMiaka 54 bado anagombea mali za urithi.....duh!!!
SadWatu wa huko kwenye mali au pesa wanakuua na hawajali kitu
Ashauza huyo tayar inawezekanaSisi wazazi tulipewa mali na nani? We si unayo mali na uma uza kwa 10M tu?
Inawezekana pia.Ashauza huyo tayar inawezekana
Sasa basi aliyekufa angeenda nazo kama alikuwa anajitafutia mwenyeweSisi wazazi tulipewa mali na nani? We si unayo mali na uma uza kwa 10M tu?
Huyu atakuwa mlevi na malaya.Miaka 54 kama hakuna ulichofanya kujiwekeza duniani ndio imeisha hivyo.
Sawa mwana simbaaa usisahau kuwagawai watoto mali zako.Nimekuunga mkono huko juuu ila para ya mwisho hapana aisee...
Si kuna wajukuu na ndugu wengine. Au unafikiri miaka 54 hakuwa na mtoto au mama alikuwa na mtoto mmoja tuNi kama familia imejibonyeza kitufe cha self destruct.
Baba kafariki mama kauawa na mtoto ananyongwa. Familia yote inapotea😪
Kwakweli ndo tunachokifanya kwa sasa kuwekeza kwa ajili ya watoto...Sawa mwana simbaaa usisahau kuwagawai watoto mali zako.
AiseeHuko moshi jamaa wa miaka 54 amemuua mama yake wa miaka 74 kwa sababu ya ugonvi wa mali alizoacha baba ama mume wa marehemu ambae ndio baba wa mtuhumiwa.
Marehemu aliacha mashamba, hayo ndio yameleta mgogoro hadi jamaa akaamua kumuua mama yake.
Matukio ya hovyo ya watu kuua wazazi wao kisa mali yanashamiri sana Kilimanjaro.
---
Adela Mushi (74), mkazi wa Okaseni, kata ya Uru kusini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro anadaiwa kuuawa kwa kunyongwa na kisha kukatwa na shoka sehemu ya usoni na mwanaye, anayedai mali zilizoachwa na marehemu baba yake.
Inadaiwa kuwa mtoto wake huyo mwenye umri wa miaka 54, alifanya tukio hilo usiku wa Septemba 23, 2024 na kisha kutelekeza mwili wa mama yake ndani ya chumba chake alichokuwa anaishi.
Mwili wa mama huyo ulikutwa ukiwa umelazwa kifudifudi huku shingoni kukiwa kumefungwa kipande cha kanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa jeshi hilo linamshikilia mwanaume huyo kwa mahojiano zaidi.
“Septemba 23, 2024 usiku wa saa 4, maeneo ya Uru Okaseni, mwanamke ajulikanaye kwa jina la Adela Dominick Mushi, aliuawa kwa kupigwa na kitu butu kichwani kisha kunyongwa kwa kutumia kipande cha kanga na mtoto wake aitwaye Nemes Dominic,” amesema Kamanda Maigwa.
Kamanda Maigwa amesema chanzo cha mauaji hayo kinachunguzwa , lakini wawili hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu wakigombea mashamba na mali za marehemu.
Mwananchi
Hapana bwana hii mamboz yenu ya kila mtoto anakuja na baraka zake ni kujidanganya....waridhike kivipi bwana wakati wee mzazi umebugi.Kwakweli ndo tunachokifanya kwa sasa kuwekeza kwa ajili ya watoto...
Ila wakikuta hamna wafundishwe kuridhika na kama hawajapewa basi wajue sio chao bado...
Sasa wee unazaa ili mtoto aje kukusaidia...pambana mwenyewe na maisha yako sii ulijidai kidume kutia watu mimba haya mtoto anataka mali mpe acha roho mbaya.Looh maskini!
Mtoto laana kabisa huyu, ama kweli kuzaa si kupata!