Moshi: Mama afariki Dunia akiwa nyumbani kwa kukosa pesa ya matibabu, aacha watoto wadogo

Moshi: Mama afariki Dunia akiwa nyumbani kwa kukosa pesa ya matibabu, aacha watoto wadogo

Huo ni ujinga kbsa angempeleka tuu hospital angedaiwa matibabu ikaw mgonjw ameshapona

Hao wachaga wawap
 
Yeap hata ingekuwa 50 kwa mikoa still masikini wapo ..sasa hao 10% usiombe ukawa ni wewe na ukoo wako.

Kama mpo safi hamna neno ila tambua wapo wanatoka huko wengi njaa kali
Na maskini WA Kilimanjaro sio kama maskini WA nachingwea
Maskini WA Kilimanjaro halali nyumba ya nyasi Bali ya bati
 
Na maskini WA Kilimanjaro sio kama maskini WA nachingwea
Maskini WA Kilimanjaro halali nyumba ya nyasi Bali ya bati
Ila anakosa pesa ya kwenda hospital I mpaka anakufa..

Basi umaskini wenu wa kukosa pesa za kwenda hospital

Achana na wa juzi huyu ni WA pili👇👇


Screenshot_20230318-133929.png
 
Na sasa Serikali itafurahia watoto wakifa kwa kukosa Matibabu hasa wale ambao Wazazi wao walikuwa Wana uwezo wa kuwalipia Bima ambazo kwa sasa imekuwa kama anasa.
 
Unajua gharama zakuuguza mtu mwenye stroke mzee baba, usiombe yakukute nakama huna bima ndio utatamani ufe wewe kwanza.
Alikuwa anaugua ugonjwa wa tumbo kuhara na kutapika. Je, hiyo ni stroke?
Hebu soma vizuri utangulizi wake ktk uzi huu.
 
Alikuwa anaugua ugonjwa wa tumbo kuhara na kutapika. Je, hiyo ni stroke?
Hebu soma vizuri utangulizi wake ktk uzi huu.
""Mume wa marehemu amesema alikuwa anakabiliwa na ukata mkubwa kutokana na kumuhudumia mama yake mzazi ambae amepooza upande mmoja wa mwili"". Umeona hayo maneno hapo wakati unasoma story nzima mkuu au tunakimbilia kutoa judgement kwakuwa hayajakukuta. Yasikiage tu!
 
Marehemu Happiness Kasmiry kutoka kijiji cha Usari, Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro alishikwa na ugonjwa wa tumbo wa kuhara na kutapika kwa siku kadhaa kabla ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake kutokana na Kukosekana kwa fedha ya matibabu.

Mume wa marehemu huyo ajulikanae kwa jina la John Kasmiry alihakangaika kutafuta pesa ya kumpeleka Hospital kwa siku kadhaa bila mafanikio.

Mume wa marehemu amesema alikuwa anakabiliwa na ukata mkubwa kutokana na kumuhudumia mama yake mzazi ambae amepooza upande mmoja wa mwili.

Marehemu ameacha watoto watatu wadogo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Ismail Urassa amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema ni kweli familia ilikosa namna ya kumpeleka kupata matibabu kutokana na ukata hivyo mama huyo kufariki dunia akiwa nyumbani kwake.
Daah inasikitisha sana kwa huo ugonjwa angewaji hospital angerudi mzima kabisa apumzike kwa amani dada nawaonea huruma watoto aliowaacha, Upendo wa mama haufanani na mtu yeyote.
 
Kwani si kunakuwaga na watu wa social ambao huwa wanalenga watu walioshindwa kabisa kumudu matibabu, Na je Mtu anaweza kukosa kabisa matibabu hata kama amefikishwa kwenye government health facility kwa kukosa pesa? Mnifahamishe jaman me nipo Afghanistan huku.
 
RIP mama, ila hiyo gharama inayotumika katika mazishi, ingetumika kumtibu angeokoa uhai wake.
 
Watu Wana roho mbaya, majirani wote wameshindwa kumpa msaada hata wa laki akaanze matibabu, mpaka mtu anakufa
Huyo jamaa nae mzembe laki yote ya Nini angeomba tu asaidiwe usafiri hata bodaboda na elfu 5 tu ya mapokezi
 
Very sorry ila kwenye msiba ndugu watakuja na magari na ng'ombe wachinjwe

Tubadlke sasa nyakat hizi nikumsaidia mgonjwa si mipeano ya harusi/shughuli
 
Back
Top Bottom