Moshi: Mama afariki Dunia akiwa nyumbani kwa kukosa pesa ya matibabu, aacha watoto wadogo

Moshi: Mama afariki Dunia akiwa nyumbani kwa kukosa pesa ya matibabu, aacha watoto wadogo

Kama kweli hivo ndivyo ilivyotokea; basi Mwenyekiti na Serikali ya Kijiji hicho wawajibike haraka kwa kujiuzulu kwani hawatoshi katika nafasi hiyo.
Nasema hivyo kwa sababu:
1. Fedha wanazopataau kukusanya kutoka vyanzo mbalimbali e.g. Faini za makesi, Makusanyo ya vilabu vya pombe, magenge/soko migahawa Makusanyo ya maliasili e.g. mchanga,mawe fedha zinaishia wapi? Mbona hakuna Taarifa ya Mapato na Matumizi(Hili ni kwa vijiji vingi tu hapa Tz.)
2. Huyo mwanaume awajibishwe au afunguliwe mashtaka ya Uzembe uliopelekea kifo cha mke. Nasema hivyo kwa sababu ; hivi hana ndugu/majirani? alishindwa kwenda kukopa? alishindwa kuuza baadhi ya mali(vitu) - hana hata kuku au hata kipande cha ardhi aweke rehani ili watu wamkopeshe? Kama yote hayo yalishindikana bora tu hata angeenda kuiba mahali akamatwe halafu achomekee hali ya mke wake. [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] Mbona Wachaga wana kamsemo kao kanakosema "Kuliko uzae mpumbavu ni bora uzae mwizi" Mpumbavu kwa kichaga ni Tondo, mwizi ni Mbafu
Unajua gharama zakuuguza mtu mwenye stroke mzee baba, usiombe yakukute nakama huna bima ndio utatamani ufe wewe kwanza.
 
Una kufa kweli mkuu hakuna atakaye hangaika nawe hii ndio Africa.
Case ya emergency kama ya huyo mama apo lazima apokelewe na kupewa huduma kwanza. Tuache kutunga sera zetu wakuu. Ndio maana hata wagonjwa wa ajali wakipelekwa hospitali husikii kuhusu gharama ya faili wala nini. Ni matibabu kwanza.
 
Nadhani ujanielewa jamaa, hio LAKI umeandika kiurahisi sana mtaani kuipata hio mtu kukupa sio rahisi Kama ulivyoandika jomba, mtaani kupata LAKI kwa watu wanaokopesha kwa riba tena unaweka asset Kama TV kubwa, LAPTOP yaani ulivyoandika sio rahisi hivyo
Nakuelewa sana ndugu, kama hayajamkuta hawezi kukuelewa.
 
Hela ya matibabu haikupatikana, cha ajabu msibani yatapikwa masufuria ya ubwabwa, nyama bila kusahau mapipa ya mbege....
Apumzike kwa amani, umasikini ni mbaya sana
 
Na hata angekuja humu mtandaoni kuomba msaada angetukanwa na kudhihakiwa.

LAKINI MASHENZI HAYO YAMO HUMU PIA YANAJIFANYA KUSEKETEEKAAA
 
Tuanze leo basi kuwachangia waliokwama mahospitalini Kupata tiba.
Pale Muhimbili kanisa katoliki ukipeleka hata pampa's moja tu ya sh 500 inapokelewa ni sadaka tosha kwa ajili ya watoto wachanga wenye uhitaji, kuliko kuhonga malaya milioni Ili akupe UTI, na stress.
Trueeeeeee
 
Very sad,, ila kuchangia umiss na yale yote Mwenyezi Mungu ameyakataza wako sawa/fasta
 
baba yangu alifariki hivihivi nadhani ni uelewa mdogo na umaskini pia maana alipelekwa hospitali amezidiwa,alikufa kimasihara.kuhara kunaua,pole wafiwa
 
Back
Top Bottom