Kama kweli hivo ndivyo ilivyotokea; basi Mwenyekiti na Serikali ya Kijiji hicho wawajibike haraka kwa kujiuzulu kwani hawatoshi katika nafasi hiyo.
Nasema hivyo kwa sababu:
1. Fedha wanazopataau kukusanya kutoka vyanzo mbalimbali e.g. Faini za makesi, Makusanyo ya vilabu vya pombe, magenge/soko migahawa Makusanyo ya maliasili e.g. mchanga,mawe fedha zinaishia wapi? Mbona hakuna Taarifa ya Mapato na Matumizi(Hili ni kwa vijiji vingi tu hapa Tz.)
2. Huyo mwanaume awajibishwe au afunguliwe mashtaka ya Uzembe uliopelekea kifo cha mke. Nasema hivyo kwa sababu ; hivi hana ndugu/majirani? alishindwa kwenda kukopa? alishindwa kuuza baadhi ya mali(vitu) - hana hata kuku au hata kipande cha ardhi aweke rehani ili watu wamkopeshe? Kama yote hayo yalishindikana bora tu hata angeenda kuiba mahali akamatwe halafu achomekee hali ya mke wake. [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] Mbona Wachaga wana kamsemo kao kanakosema "Kuliko uzae mpumbavu ni bora uzae mwizi" Mpumbavu kwa kichaga ni Tondo, mwizi ni Mbafu