Moshi: Mfanyabiashara aua kwa bastola Himo

Mtu ana ml 100 tu tena zipo Bank anaenda kunywa pombe na bastola. Hapo ukichunguza wote walikuwa kwenye state ya ulevi wa kupindukia
Ulevi sio kitu kizuri hata kidogo, ndio maana inashauriwa pombe inywewe kwa kiasi
 
Wanasema kwamba kwenye ulimwengu wa crime, bunduki uliyoifanyia uhalifu kwa kukatisha uhai wa mtu hakikisha unaitupa au kuiharibu kwa namna yoyote ile.. sijawahi kufahamu kujua Nini main reason katika hili.. [emoji848]
Aisee
 
Hususan ikiwa umekutwa red handed unatekeleza tukio la kuua kwa silaha kwa mtu ambaye alikuwa ni target , wanasema silaha idondoshe chini hata kama askari au mashuhuda wamekuona kwa 100% .. sijajua Nini kipo nyuma ya hili
 
Angesema tu sorry asieee nimevurugwa huko nimepewa taarifa mbaya naendesha tu gari hapa ila akili hata haipo hapa. Samahani sana ni bahati mbaya niwie radhi mkuu.
Inategemea na jinsi alivyomfuata kutoka kwenye Bodaboda. Pengine aliona maisha yake yako hatarini na wakimchangia wanaweza kumuuwa.

Kama walikuwa wametoka msibani, uwezekano mkubwa ni walikuwa wamelewa. Na kitendo cha kusimamisha pikipiki hiyo saa nne na nusu usiku, kushuka na kumfuata, makosa ni ya marehemu. Tena especially kama ajali haikutokea.

Hapo ulevi wao uliwatuma wamuoshee. Sikubaliani na matumizi ya hovyo ya bastola, lakini marehemu ana makosa zaidi kwa maoni yangu.
 
Watu weusi tuna matatizo ya akili by nature, Hili suala la watu kuruhusiwa kumiliki Silaha always nalipinga. Hayo mambo ni kwa watu weupe tu. Hapa kwetu mtu akishamiliki silaha tu anaanza kujiona ni mbabe.
 
Samaleko wana jukwaaa! Ni habari iliyozua gumzo katika mji mdogo wa Himo mkaoni Kilimanjaro.

====
Ni mauaji yaliyotikisa mji wa kibiashara wa Himo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro, baada ya mfanyabiashara mashuhuri katika mji huo, Kennedy Minja (47) kudaiwa kumfyatulia risasi na kumuua papo hapo, mkazi wa Kilema, Deogratius Lyimo.

Baada ya tukio hilo, inaelezwa mfanyabiashara huyo aliendesha gari lake umbali wa kilomita 27 kutoka mji wa Himo hadi Moshi mjini ambako inadaiwa alijisalimisha kituo kikuu cha Polisi na hadi leo ana siku 18 anashikiliwa polisi.

Ni tukio lilitikisa mji huo kutokana na umaarufu wa mfanyabiashara huyo wa mazao na namna mauaji hayo yanavyodaiwa kutokea, yakihusishwa na mzozo wa dakika chache baina yake na marehemu.

Wananchi wa mji huo hawaelewi kiini hasa cha mauaji, kama kweli ni baada ya tajiri huyo kuwakosakosa kuwagonga marehemu na ndugu yake waliokuwa na pikipiki au la.

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limethibitisha kumshikilia mfanyabiashara huyo pamoja na bastola anayodaiwa kuitumia katika mauaji hayo na huenda akafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia leo kwa tuhuma za mauaji.

Alipoulizwa jana kuhusu ni lini mfanyabiashara huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani, Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo alisema: "Jalada limeshapelekwa kwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali, ila nafuatilia kujua ni lini atafikishwa mahakamani, huku kukiwa na taarifa huenda akafikishwa mahakamani kesho.

Awali Kamanda wa polisi mkoani hapa, Simon Maigwa alisema tukio hilo lilitokea saa 4:30 usiku wa kuamkia Mei 17, 2023 katika Barabara ya Himo-Marangu ambako mfanyabiashara huyo anadaiwa kumuua Lyimo.

Aliyeshuhudia afunguka
Richard Mahoo, aliyekuwa amempakia Deogratius, wakitokea Himo kuelekea Kilema alidai walipofika karibu na ofisi ya mbunge wa Vunjo, mfanyabiashara huyo aliingia barabarani bila tahadhari na kutaka kuwagonga na gari lake.

Mahoo alidai kitendo kile kilisababisha Deogratius kushuka kwenye pikipiki na kumfuata na kumuuliza kwa nini anataka kuwagonga, lakini mtuhumiwa alishuka kwenye gari na kutamka maneno kuwa, “nyie mlikuwa mnatakaje”. “Kauli ile ilimkera marehemu na kuanza kushikana na kuanza kupigana. Wakati huo mimi nilikuwa naegesha pikipiki vizuri ili niwafuate, kitendo cha mimi kushuka kwenye pikipiki nikasikia mlio wa bastola, nikachanganyikiwa na kukimbia,"alidai.

Aliongeza: "Nilikimbia kama hatua 200 ndipo nikasimama na kuangalia nini kinaendelea, huyo mwenye gari akapiga tena risasi nyingine kunielekezea mimi, lakini haikunipata, ndipo akawasha gari na kukimbia," alidai Mahoo.

Kwa mujibu wa shuhuda huyo, baada ya milio hiyo ya risasi watu walijitokeza na kumchukua marehemu na kumpeleka Hospitali ya Faraja Himo na walipomfikisha waliambiwa ameshafariki dunia.

Kwa upande wa baba mkubwa wa marehemu, Isaack Lyimo alisema kijana wake alitokea kwenye msiba wilayani Siha akiwa na rafiki yake na walipofika Himo, walichukua pikipiki ya huyo rafiki yake kwa ajili ya kuelekea nyumbani Kijiji cha Kyou, Kilema.

Mzazi huyo alidai walipofika jirani na ofisi ya mbunge wa Vunjo kulitokea kuzozana kati ya mfanyabiashara huyo na mtoto wake baada ya mfanyabiashara huyo kuingia barabarani bila tahadhari na kutaka kuwagonga.

Kulingana na maelezo aliyopewa, katika mabishano hayo walifikia hatua ya kutaka kupigana, ndipo mfanyabiashara huyo inadaiwa alikwenda kwenye gari na kuchukua bastola na kumfyatulia risasi mtoto wake na kumuua papo hapo.

Mwananchi
We bwana acha uongo, ati kilometa 27 toka Himo hadi Moshi.
Unafikiri sisi chasaka wa kuja?
Nimeacha hata kusoma.
 
Tanzania hakuna sheria ya blood money. Ingekuwa Uarabuni au Pakistan angelipa blood money mchezo kwisha anaachiwa.

Kwa hapa atatoa rushwa kwa wakubwa aachiwe na familia ya marehemu haitaambulia chochote
Ndio maana amewahi kijishtaki' ili aseme "niliua bila ya kukusudia". Kesi kwishney!
 
Hizo bastola mnazouziana kipesalization bila kuangalia mental stability ya kuhold up strange situation kama hizo ni janga.Watu wengine wana ukichaa uliojificha.Kigezo cha kumiliki silaha kisiwe pesa pekee.Akili,Saikolojia na historia ya mhusika ni muhimu vichunguzwe kwa undani zaidi
 
Samaleko wana jukwaaa! Ni habari iliyozua gumzo katika mji mdogo wa Himo mkaoni Kilimanjaro.

====
Ni mauaji yaliyotikisa mji wa kibiashara wa Himo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro, baada ya mfanyabiashara mashuhuri katika mji huo, Kennedy Minja (47) kudaiwa kumfyatulia risasi na kumuua papo hapo, mkazi wa Kilema, Deogratius Lyimo.

Baada ya tukio hilo, inaelezwa mfanyabiashara huyo aliendesha gari lake umbali wa kilomita 27 kutoka mji wa Himo hadi Moshi mjini ambako inadaiwa alijisalimisha kituo kikuu cha Polisi na hadi leo ana siku 18 anashikiliwa polisi.

Ni tukio lilitikisa mji huo kutokana na umaarufu wa mfanyabiashara huyo wa mazao na namna mauaji hayo yanavyodaiwa kutokea, yakihusishwa na mzozo wa dakika chache baina yake na marehemu.

Wananchi wa mji huo hawaelewi kiini hasa cha mauaji, kama kweli ni baada ya tajiri huyo kuwakosakosa kuwagonga marehemu na ndugu yake waliokuwa na pikipiki au la.

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limethibitisha kumshikilia mfanyabiashara huyo pamoja na bastola anayodaiwa kuitumia katika mauaji hayo na huenda akafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia leo kwa tuhuma za mauaji.

Alipoulizwa jana kuhusu ni lini mfanyabiashara huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani, Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo alisema: "Jalada limeshapelekwa kwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali, ila nafuatilia kujua ni lini atafikishwa mahakamani, huku kukiwa na taarifa huenda akafikishwa mahakamani kesho.

Awali Kamanda wa polisi mkoani hapa, Simon Maigwa alisema tukio hilo lilitokea saa 4:30 usiku wa kuamkia Mei 17, 2023 katika Barabara ya Himo-Marangu ambako mfanyabiashara huyo anadaiwa kumuua Lyimo.

Aliyeshuhudia afunguka
Richard Mahoo, aliyekuwa amempakia Deogratius, wakitokea Himo kuelekea Kilema alidai walipofika karibu na ofisi ya mbunge wa Vunjo, mfanyabiashara huyo aliingia barabarani bila tahadhari na kutaka kuwagonga na gari lake.

Mahoo alidai kitendo kile kilisababisha Deogratius kushuka kwenye pikipiki na kumfuata na kumuuliza kwa nini anataka kuwagonga, lakini mtuhumiwa alishuka kwenye gari na kutamka maneno kuwa, “nyie mlikuwa mnatakaje”. “Kauli ile ilimkera marehemu na kuanza kushikana na kuanza kupigana. Wakati huo mimi nilikuwa naegesha pikipiki vizuri ili niwafuate, kitendo cha mimi kushuka kwenye pikipiki nikasikia mlio wa bastola, nikachanganyikiwa na kukimbia,"alidai.

Aliongeza: "Nilikimbia kama hatua 200 ndipo nikasimama na kuangalia nini kinaendelea, huyo mwenye gari akapiga tena risasi nyingine kunielekezea mimi, lakini haikunipata, ndipo akawasha gari na kukimbia," alidai Mahoo.

Kwa mujibu wa shuhuda huyo, baada ya milio hiyo ya risasi watu walijitokeza na kumchukua marehemu na kumpeleka Hospitali ya Faraja Himo na walipomfikisha waliambiwa ameshafariki dunia.

Kwa upande wa baba mkubwa wa marehemu, Isaack Lyimo alisema kijana wake alitokea kwenye msiba wilayani Siha akiwa na rafiki yake na walipofika Himo, walichukua pikipiki ya huyo rafiki yake kwa ajili ya kuelekea nyumbani Kijiji cha Kyou, Kilema.

Mzazi huyo alidai walipofika jirani na ofisi ya mbunge wa Vunjo kulitokea kuzozana kati ya mfanyabiashara huyo na mtoto wake baada ya mfanyabiashara huyo kuingia barabarani bila tahadhari na kutaka kuwagonga.

Kulingana na maelezo aliyopewa, katika mabishano hayo walifikia hatua ya kutaka kupigana, ndipo mfanyabiashara huyo inadaiwa alikwenda kwenye gari na kuchukua bastola na kumfyatulia risasi mtoto wake na kumuua papo hapo.

Mwananchi
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali inapostahili. Ila wakati mwingine Bodaboda nao huwa wana yao.
 
Wawe makini na maelezo Yao

Mmoja ,walipigana
Mwingine, walizozana na kutaka kupigana

Hatujui muuaji ,anasemaje alitaka kuibiwa akajihami au lah
 
NARUDIA KUSEMA HUMU NA NISHASEMA SANA HUMU
asilimia kubwa ya wanaomiliki bastola
Haziwasaidi chochote zaidi ya kuwaletea majanga

Ova
Uko sahihi juzi kati kuna mshamba mmoja katishia watu na kupiga bullet Moja juu Garage fulani
Kumbe pale kuna Mwanaume anamchora tu
Dakika 10 watu wa Kazi kazini wa hapa wakaondoka nae ....
Tumieni na zitunzeni Bastola zenu vzr kama mlivoelekezwa wakati mnakabidhiwa.
 
Wenda wote walikuwa under influence... Alcohol may be .

Too bad.
Mwenye Bastola huyo ni mkorofi ukisoma Vzr utaona kuanzia uendeshaji majibu yake mpk maamuzi yake.
Kama aliua yule waliyekua wanagombana nae kivipi tena alimrushia yule mwingine risasi ya nini
Ilikua na yeye auwawe tu.
 
Bora Familia idai fidia kwa mtuhumiwa, maana km ana pesa atakaa ndani mda mchache then anatoka nje.

Bora wadai fidia aseeh.
 
Hapo familia iende tu kwenye mahakama ya kimila. Kwenye mahakama za kawaida tayari jamaa anashinda kama kakaa siku 18 bila kupanda kizimbani. Pia kitendo cha kukimbilia town alishajua watetezi wake wako kule. Hapo ni mahakama ya kimila tu ndo inafaa.
 
Wachaga ni kabila la ajabu mno hapa Tanzania
Serikali iwahamishie hao wachaga wa "ajabu' kenya haraka sana.
Kama wamasai "wema"wa longido na ngorongoro wamehamishiwa kwenye mapori ya msomera , hao wachaga wana nini na wao wasipakiwe kwenye mafuso wapelekwe kwenye mapori ya loitoktoki, kenya?
 
Back
Top Bottom