Uchaguzi 2020 Moshi mjini: Mkutano wa Kampeni wa mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Magufuli. Asema atafufua viwanda vilivyolala

Uchaguzi 2020 Moshi mjini: Mkutano wa Kampeni wa mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Magufuli. Asema atafufua viwanda vilivyolala

Juzi ulisema kanda ya huko ni ya watu wasomi hawashoboki na unachokiandika hapa, vipi tena mkuu.
Magu anajua kucheza na akili za watu,kwa mfano Dr.Kimei wa Vunjo ameomba Vunjo ipewe halmashauri kwa sababu za msingi.
Nae Magu kamjibu akitaka madiwani wote watoke CCM ili wakishaapishwa wamletee Magu hiyo agenda, ataishughulikia haraka lakini kwa sharti la kuchagua madiwani wote,mbunge na Raisi kwa tiketi ya CCM.
 
Jana na juzi walikuwa wanaangalia msukule unaoishi leo wanapata burudani. Life no stress.
Ccm safari hii wameshikwa maqer Leo.kwa hivyo shule zimefungwa Leo hapo moshi.
 
Vipi Sahani ya Kushiba? Maana Ubwabwa wa kushiba unaonekana kwenye sahani.

Moshiii Mpoooooooooooo!! Asanteni Asanteni Sana.
Sahani iko tupu yani uwanja hakuna watu pamoja na kugawa vinguo vyao bure,dis iz moshi canan ya tanzania
 
Magu anajua kucheza na akili za watu,kwa mfano Dr.Kimei wa Vunjo ameomba Vunjo ipewe halmashauri kwa sababu za msingi.
Nae Magu kamjibu akitaka madiwani wote watoke CCM ili wakishaapishwa wamletee Magu hiyo agenda, ataishughulikia haraka lakini kwa sharti la kuchagua madiwani wote,mbunge na Raisi kwa tiketi ya CCM.
Ndio Kampeni pia
 
NEC kuweni makini, Chadema wamesha ona kipigo kizito ndani ya sanduku la kura wanatafuta mtu wa kumrushia Lawama msipoangalia wanaweza susia uchaguzi dakika yoyote kutoka sasa ili Lawama ziwe juu yenu.
 
NEC kuweni makini, Chadema wamesha ona kipigo kizito ndani ya sanduku la kura wanatafuta mtu wa kumrushia Lawama msipoangalia wanaweza susia uchaguzi dakika yoyote kutoka sasa ili Lawama ziwe juu yenu.
Yaaaah waambie waachie mawakara wote Kila kutuo ili tuone watu wanavyoshindwa asubuhi
 
Lakini ni juzi tu ulipokuwa ukisema, kanda hiyo haidanganyiki!!

Vipi Leo, kunabakora zilipita majumbani kwenu kulazimisha watu wapande hayo mabasi?

October 28 is only next week, after which JPM will be sworn in again at Mkapa Stadium
Walevi hata ulaya wapo lakini siyo kama kwenu, wengine wameletwa toka Tanga, Singida, Pwani na Morogoro
 
Moshi shikamooo! Ahsanteni sana. Kama Moshi wamekubali wewe uko sijui manyoni hutatubabaisha abadani.
Kama lisu aliweza kupata watu chato ndio atashindwa magufuli kupata watu moshi?
 
Mzee amefeli, hizo ni ahadi hewa, apumzike tu kwa kweli.
 
MAGUFULI: Nawashukuru viongozi wa dini kwa Dua na Sala zao. Ninajua wagombe wenzangu wa ubunge wameeleza yote na mikakati mbalimbali ya chama cha mapinduzi kama ilivyofafanuliwa kwenye Ilani. Nchi yetu imebarikiwa kwa mambo mengi sana, binadamu wa kwanza, mti mrefu, mlima mrefu kuliko yote Afrika, madini ya Tanzanite, Tanzania ni nchi ya pili kuwa na mifugo wengi. ya tatu kwa kuvumbua kiwango kikubwa cha gesi asili na nne kwa kuzalisha dhahabu barani Afrika.

Zaidi ya kilomita 1422 tunapakana na bahari, ina maziwa, mito, misitu, ina vitu mbalimbali. Nchi hii imebarikiwa sana na Mungu. Nchi yetu ni tajiri, miaka mitano iliyopita tumedhihirisha sisi sio masikini, sisi ni matajiri. Tumefanya mambo mengi makubwa tena kwa nguvu zetu wenyewe, najua mengi mnayafahamu.

Katika kipindi cha miaka mitano tuliweza kuanza kukusanya kodi kwa mwezi kutoka bilioni 850 mpaka trilioni 1.5 na kuna baadhi ya miezi tumefika trilioni 1.6. Tumeweza kujenga vituo vya afya, zahanati, kupeleka umeme kwenye vijiji. Kwa kudhihirisha Tanzania ni tajiri tumeanzisha miradi mikubwa. Tumejenga barabara za lami zaidi ya kilomita 3,500 na tunaendelea kujenga kilomita 2,500. Ndege 11, kununua na kujenga radar katika viwanja viwanja vyetu vikubwa kwa kutumia fedha zetu. Tumeanzisha mradi wa kujenga reli ya umeme, treni ambazo zinatumika Ulaya. Ninaweza kutaja miradi mingi langi lengo ni kuwathibitishia wanamoshi tuko pazuri na tunaenda vizuri.

Tumebarikiwa kuwa na nchi tajiri, kinachohitajika ni kupata kiongozi atakaeweza kuutumia utajiri huu kwa manufaa ya watanzania wote. Na mimi naamini hiyo kazi inanifa kwa sababu nimeonesha katika miaka mitano iliyopita. Mimi naamini kazi hiyo inawafaa wabunge wa CCM, madiwani wa CCM kwa sababu tumeiandaa vizuri katika ilani ya uchaguzi.

Lengo kubwa la kushusha bei ya umeme, tunataka tuwe na viwanda vingi. Tunataka viwanda vilivyolala tuvifufue vyote na kwa hapa Kilimanjaro, Moshi tumeanza, palikuwa na kiwanda cha ngozi nafikiri Karanga kilichokuwa chini ya Magereza.

Leo ukienda kwenye kiwanda hicho utafikiri umefika Ulaya, kitakuwa kinatengeneza pea ya viatu kwa mwaka milioni 1.2, bado hujaweka mikufu, mtaitaje ile? Mikoba, unajua sijamnunulia mke wangu mkoba tangu nimuoe kwa hiyo msishangae nikisahau, kwa hiyo mikoba, mikanda na vitu vingine vitaanza kutengenezwa hapa.

Palitokea ugonjwa wa korona dunia nzima, watu wamekufa maelfu tukaambiwa Afrika maiti zitakuwa zinaokotwa barabarani. Katika mtihani mkubwa nilioupata ulikuwa ni huo katika uongozi wangu.

===============


Reli ya umeme inasaidia vipi Moshi! wenyewe bado wana gari moshi!!. Hivyo viwanda nani kaviaribu. CCM hawataki kufanya vitu kaskazini ni watu wenyewe ndiyo wana maendeleo sio serikali
 
Walevi hata ulaya wapo lakini siyo kama kwenu, wengine wameletwa toka Tanga, Singida, Pwani na Morogoro
Kama huko kwenu kuna walevi wengi kama hivo, basi huwenda kila penye mji wa watu watano, watatu Kati Yao ndio walevi, na ndio watakaompa Kura JPM!!

Basi JPM Atashinda Kwa kimbunga!!
 
Reli ya umeme inasaidia vipi Moshi! wenyewe bado wana gari moshi!!. Hivyo viwanda nani kaviaribu
Unaakili ndogo Sana wewe, huwenda kipimo chake ni kama akili ya popo!

Unachokiongea hapa ndicho kimedhihilisha hayo!

Wewe ni wa kuonewa huruma
 
Back
Top Bottom