Uchaguzi 2020 Moshi mjini: Mkutano wa Kampeni wa mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Magufuli. Asema atafufua viwanda vilivyolala

Uchaguzi 2020 Moshi mjini: Mkutano wa Kampeni wa mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Magufuli. Asema atafufua viwanda vilivyolala

Baada ya 28 October, mtarukaruka Serengeti Kwa adabu!!

Mbuzi kasoro mkia wewe
Wewe mbwa subiri kuosha miguu ya watu hapo lumumba!Regardless ya kitakachotokea na nani atashinda,maisha yataendelea na nitaendelea kuishi!
Wewe hapo sasa,pressure juu CCM ikianguka!Utakufa mbwa wewe usiyejua kujitafutia zaidi ya kulamba miguu ya watu uendeshe familia,shwain!
 
Hajamnunulia mke wake mkoba tangu amuoe [emoji23][emoji23] Tulikuwa tunamlaumu bure huyu mzee kama ilishindikana kurahisisha maisha ya mkewe kwa watanzania asingeweza.
CCM mfungeni huyu mzee breki ya mdomo hata kwa kumroga anazidi kuwaharibia. Hakuna njia nyingine inabidi akapumzike Chato na awamu hii watanzania tununue mkoba tumpe afikishe kwa mkewe mama zawadi.
 
Wewe mbwa subiri kuosha miguu ya watu hapo lumumba!Regardless ya kitakachotokea na nani atashinda,maisha yataendelea na nitaendelea kuishi!
Wewe hapo sasa,pressure juu CCM ikianguka!Utakufa mbwa wewe usiyejua kujitafutia zaidi ya kulamba miguu ya watu uendeshe familia,shwain!
Naweza kukulisha wewe na familia yako na hata ukoo wako

28 October, Serengeti mtapungua nyinyi! We subiri
 
MAGUFULI: Nawashukuru viongozi wa dini kwa Dua na Sala zao. Ninajua wagombe wenzangu wa ubunge wameeleza yote na mikakati mbalimbali ya chama cha mapinduzi kama ilivyofafanuliwa kwenye Ilani. Nchi yetu imebarikiwa kwa mambo mengi sana, binadamu wa kwanza, mti mrefu, mlima mrefu kuliko yote Afrika, madini ya Tanzanite, Tanzania ni nchi ya pili kuwa na mifugo wengi. ya tatu kwa kuvumbua kiwango kikubwa cha gesi asili na nne kwa kuzalisha dhahabu barani Afrika.

Zaidi ya kilomita 1422 tunapakana na bahari, ina maziwa, mito, misitu, ina vitu mbalimbali. Nchi hii imebarikiwa sana na Mungu. Nchi yetu ni tajiri, miaka mitano iliyopita tumedhihirisha sisi sio masikini, sisi ni matajiri. Tumefanya mambo mengi makubwa tena kwa nguvu zetu wenyewe, najua mengi mnayafahamu.

Katika kipindi cha miaka mitano tuliweza kuanza kukusanya kodi kwa mwezi kutoka bilioni 850 mpaka trilioni 1.5 na kuna baadhi ya miezi tumefika trilioni 1.6. Tumeweza kujenga vituo vya afya, zahanati, kupeleka umeme kwenye vijiji. Kwa kudhihirisha Tanzania ni tajiri tumeanzisha miradi mikubwa. Tumejenga barabara za lami zaidi ya kilomita 3,500 na tunaendelea kujenga kilomita 2,500. Ndege 11, kununua na kujenga radar katika viwanja viwanja vyetu vikubwa kwa kutumia fedha zetu. Tumeanzisha mradi wa kujenga reli ya umeme, treni ambazo zinatumika Ulaya. Ninaweza kutaja miradi mingi langi lengo ni kuwathibitishia wanamoshi tuko pazuri na tunaenda vizuri.

Tumebarikiwa kuwa na nchi tajiri, kinachohitajika ni kupata kiongozi atakaeweza kuutumia utajiri huu kwa manufaa ya watanzania wote. Na mimi naamini hiyo kazi inanifa kwa sababu nimeonesha katika miaka mitano iliyopita. Mimi naamini kazi hiyo inawafaa wabunge wa CCM, madiwani wa CCM kwa sababu tumeiandaa vizuri katika ilani ya uchaguzi.

Lengo kubwa la kushusha bei ya umeme, tunataka tuwe na viwanda vingi. Tunataka viwanda vilivyolala tuvifufue vyote na kwa hapa Kilimanjaro, Moshi tumeanza, palikuwa na kiwanda cha ngozi nafikiri Karanga kilichokuwa chini ya Magereza.

Leo ukienda kwenye kiwanda hicho utafikiri umefika Ulaya, kitakuwa kinatengeneza pea ya viatu kwa mwaka milioni 1.2, bado hujaweka mikufu, mtaitaje ile? Mikoba, unajua sijamnunulia mke wangu mkoba tangu nimuoe kwa hiyo msishangae nikisahau, kwa hiyo mikoba, mikanda na vitu vingine vitaanza kutengenezwa hapa.

Palitokea ugonjwa wa korona dunia nzima, watu wamekufa maelfu tukaambiwa Afrika maiti zitakuwa zinaokotwa barabarani. Katika mtihani mkubwa nilioupata ulikuwa ni huo katika uongozi wangu.

===============

Maendeleo yanahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Ardhi ni majumuisho ya yote aliyoyabainisha mh Magufuli kuwa nchi imebarikiwa kuwa navyo. Watu tunao wa kutosha na kwa miaka 5 naamini tumeongezeka zaidi kwa ushauri wa mh kusema tuzaane kwa fujo. Nini ni mkwamo wa maendeleo ya Tanzania? Siasa na sera ya CCM is the best. Uongozi mbovu wa CCM ndio shida.
 
Kafanyiwa na Dua na ASKOFU mkuu wa KKKT Askofu Shoo na Shehe mkuu wa Kilimanjaro na team yake waliofika kwenye mkutano wake wa kampeni.

Bado anaendeleza hizo porojo za viwanda?
 
Utatuharibia watoto wetu wewe, na pia miaka 30 inakuhusu. Yaani hata sura tu umeshindwa ng'amua kuwa ni watoto wa shule, "minor" au "under 18"!!?
Sikuona watoto wa shule bali pisi Kali wadada.
By the way mimi sio msagaji.
 
Sawa ila tunawakumbusha baada ya kumaliza msisahau kuwarudisha kwenye malori raia mlipowatoa ,pia mfidie muda mliowapotezea wanafunzi na walimu kwenda kumsikiliza meko inabidi jmos wanafunzi wasome kufidia muda mliowapotezea kwenda kujaza watu uwanjani.
Sasa hivi watawarisha vizuri ili wapige kura ,baada ya kura ndo wanaanza kufokewa
 
Back
Top Bottom