Uchaguzi 2020 Moshi mjini: Mkutano wa Kampeni wa mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Magufuli. Asema atafufua viwanda vilivyolala

Uchaguzi 2020 Moshi mjini: Mkutano wa Kampeni wa mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Magufuli. Asema atafufua viwanda vilivyolala

Reli ya umeme inasaidia vipi Moshi! wenyewe bado wana gari moshi!!. Hivyo viwanda nani kaviaribu. CCM hawataki kufanya vitu kaskazini ni watu wenyewe ndiyo wana maendeleo sio serikali. KCMC haijajegwa na serikali.
 
Kuna watu hawaamini wanachokiona[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mwaka 2015 alifika Moshi kuomba kura kwa sera ya Tanzania ya viwanda, kwa ahadi kuwa akichaguliwa atafufua viwanda vya Moshi.

Magufuli amekuwa rais wa Tanzania tangu 2015 chini ya sera ya Tanzania ya Viwanda, hakuna kiwanda kilichofufuliwa Moshi mpaka sasa.

Mwaka huu 2020 Magufuli hana sera rasmi ya Tanzania ya viwanda (imefutwa?) halafu anarudia tena kuwaahidi wakazi wa Moshi kufufua viwanda!!

Anadhani watu wa Moshi ni wajinga sana. Ngoja ifike tarehe 28 Oktoba wamshikishe adabu.
 
Tuliambiwa kuna viwanda 4000, mara ajira millioni 6 zimezalishwa awamu hii ila kiuhalisia hata uchukue darubini huwezi kuona hayo yanayosemwa, wawekezaji wamefunga biashara na kutimkia kwao ,miaka 5 wahitimu wanasubiri neema na hakuna nyongeza ya mshahara sasa kama hivyo vidogo vimemshinda anakuja vipi na habari ya kufufua viwanda!
 
Ila Moshi Kuna watoto wazuri bwana...pisi kali kinoma nawaona kwa Tv
Utatuharibia watoto wetu wewe, na pia miaka 30 inakuhusu. Yaani hata sura tu umeshindwa ng'amua kuwa ni watoto wa shule, "minor" au "under 18"!!?
 
Tuliambiwa kuna viwanda 4000, mara ajira millioni 6ziumezalishwa awamu hii ila kiuhalisia hata uchukue darubini huwezi kuona hayo yanayosemwa, wawekezaji wamefunga biashara na kutimkia kwao ,miaka 5 wahitimu wanasubiri neema na hakuna nyongeza ya mshahara sasa kama hivyo vidogo vimemshinda anakuja vipi na habari ya kufufua viwanda kama viwanda
Msomi gani wewe, uajiliwe na Nani na hujitamhui kama umesoma au la

Kama wasomi Tz wako kama wewe, ni Bora msiajiliwe kabisa

October 28 is only next week, after which JPM will be sworn in again at Mkapa Stadium
 
Moshi shikamooo! Ahsanteni sana. Kama Moshi wamekubali wewe uko sijui manyoni hutatubabaisha abadani.
Nyie mapopoma hata 2015 mlipata watu moshi ila kwenye sanduku la kura mkapigwa chini!Watu moshi na kaskazini kwa ujumla endeleni kuwasikia hivyo hivyo kwenye bomba!
 
Msomi gani wewe, uajiliwe na Nani na hujitamhui kama umesoma au la

Kama wasomi Tz wako kama wewe, ni Bora msiajiliwe kabisa

October 28 is only next week, after which JPM will be sworn in again at Mkapa Stadium
Wewe ndiye popoma kabisa,huyo uliyemquote ameandika hoja za maana sana!Wewe umeishia kutoa kashfa tu,jinga kabisa!
 
MAGUFULI: Nawashukuru viongozi wa dini kwa Dua na Sala zao. Ninajua wagombe wenzangu wa ubunge wameeleza yote na mikakati mbalimbali ya chama cha mapinduzi kama ilivyofafanuliwa kwenye Ilani. Nchi yetu imebarikiwa kwa mambo mengi sana, binadamu wa kwanza, mti mrefu, mlima mrefu kuliko yote Afrika, madini ya Tanzanite, Tanzania ni nchi ya pili kuwa na mifugo wengi. ya tatu kwa kuvumbua kiwango kikubwa cha gesi asili na nne kwa kuzalisha dhahabu barani Afrika.

Zaidi ya kilomita 1422 tunapakana na bahari, ina maziwa, mito, misitu, ina vitu mbalimbali. Nchi hii imebarikiwa sana na Mungu. Nchi yetu ni tajiri, miaka mitano iliyopita tumedhihirisha sisi sio masikini, sisi ni matajiri. Tumefanya mambo mengi makubwa tena kwa nguvu zetu wenyewe, najua mengi mnayafahamu.

Katika kipindi cha miaka mitano tuliweza kuanza kukusanya kodi kwa mwezi kutoka bilioni 850 mpaka trilioni 1.5 na kuna baadhi ya miezi tumefika trilioni 1.6. Tumeweza kujenga vituo vya afya, zahanati, kupeleka umeme kwenye vijiji. Kwa kudhihirisha Tanzania ni tajiri tumeanzisha miradi mikubwa. Tumejenga barabara za lami zaidi ya kilomita 3,500 na tunaendelea kujenga kilomita 2,500. Ndege 11, kununua na kujenga radar katika viwanja viwanja vyetu vikubwa kwa kutumia fedha zetu. Tumeanzisha mradi wa kujenga reli ya umeme, treni ambazo zinatumika Ulaya. Ninaweza kutaja miradi mingi langi lengo ni kuwathibitishia wanamoshi tuko pazuri na tunaenda vizuri.

Tumebarikiwa kuwa na nchi tajiri, kinachohitajika ni kupata kiongozi atakaeweza kuutumia utajiri huu kwa manufaa ya watanzania wote. Na mimi naamini hiyo kazi inanifa kwa sababu nimeonesha katika miaka mitano iliyopita. Mimi naamini kazi hiyo inawafaa wabunge wa CCM, madiwani wa CCM kwa sababu tumeiandaa vizuri katika ilani ya uchaguzi.

Lengo kubwa la kushusha bei ya umeme, tunataka tuwe na viwanda vingi. Tunataka viwanda vilivyolala tuvifufue vyote na kwa hapa Kilimanjaro, Moshi tumeanza, palikuwa na kiwanda cha ngozi nafikiri Karanga kilichokuwa chini ya Magereza.

Leo ukienda kwenye kiwanda hicho utafikiri umefika Ulaya, kitakuwa kinatengeneza pea ya viatu kwa mwaka milioni 1.2, bado hujaweka mikufu, mtaitaje ile? Mikoba, unajua sijamnunulia mke wangu mkoba tangu nimuoe kwa hiyo msishangae nikisahau, kwa hiyo mikoba, mikanda na vitu vingine vitaanza kutengenezwa hapa.

Palitokea ugonjwa wa korona dunia nzima, watu wamekufa maelfu tukaambiwa Afrika maiti zitakuwa zinaokotwa barabarani. Katika mtihani mkubwa nilioupata ulikuwa ni huo katika uongozi wangu.

===============

Mwaka 2015 ulisema utafufua viwanda,mwaka 2020 unasema utafufua viwanda. Moshi Wananchi wamekuelewa?
 
Magu anajua kucheza na akili za watu,kwa mfano Dr.Kimei wa Vunjo ameomba Vunjo ipewe halmashauri kwa sababu za msingi.
Nae Magu kamjibu akitaka madiwani wote watoke CCM ili wakishaapishwa wamletee Magu hiyo agenda, ataishughulikia haraka lakini kwa sharti la kuchagua madiwani wote,mbunge na Raisi kwa tiketi ya CCM.
Hiyo ni akili au ujinga?
Yaani mtu mzima anakupa sababu za kimsingi za kwanini anahitaji jambo fulani halafu wewe unatoa majibu ya kipumbavu, halafu unasema anajua kucheza na akili za watu. Huo ni ujinga na upumbavu.

Watu wa Kilimanjaro wanataka haki, uhuru na maendeleo yao, sio kuwalamba viatu watawala. Waligoma huo upuuzi wa kuwalamba viatu watawala tangu za enzi za wakoloni, enzi za TANU na zama za CCM.
 
Tuliambiwa kuna viwanda 4000, mara ajira millioni 6ziumezalishwa awamu hii ila kiuhalisia hata uchukue darubini huwezi kuona hayo yanayosemwa, wawekezaji wamefunga biashara na kutimkia kwao ,miaka 5 wahitimu wanasubiri neema na hakuna nyongeza ya mshahara sasa kama hivyo vidogo vimemshinda anakuja vipi na habari ya kufufua viwanda kama viwanda
Kama ulimsikiliza polepole umepotea,, yeye anaongea tu chochote kinachomjia.
 
Unafufuaje kiwanda kilicholala?
Unafufua kitu kilichokufa na unaamcha kitu kilicholala.

Sasa tuambiwe, Mheshimiwa alikuwa anamaanisha lipi?
 
Hiyo ni akili au ujinga?
Yaani mtu mzima anakupa sababu za kimsingi za kwanini anahitaji jambo fulani halafu wewe unatoa majibu ya kipumbavu, halafu unasema anajua kucheza na akili za watu. Huo ni ujinga na upumbavu.

Watu wa Kilimanjaro wanataka haki, uhuru na maendeleo yao, sio kuwalamba viatu watawala. Waligoma huo upuuzi wa kuwalamba viatu watawala tangu za enzi za wakoloni, enzi za TANU na zama za CCM.
Unajipendekeeeeza!!

Hao waliokuwa wamejaaa uwanjani kumsikiliza huyo usiyempenda walikuwa ni watu kusini wale?

Juzi ulisema kuwa, JPM hatapata watu kwenye Kampeni zake kanda za kaskazini, Leo unabadiri wazo

Mjusi mkubwa wewe
 
Hiyo ni akili au ujinga?
Yaani mtu mzima anakupa sababu za kimsingi za kwanini anahitaji jambo fulani halafu wewe unatoa majibu ya kipumbavu, halafu unasema anajua kucheza na akili za watu. Huo ni ujinga na upumbavu.

Watu wa Kilimanjaro wanataka haki, uhuru na maendeleo yao, sio kuwalamba viatu watawala. Waligoma huo upuuzi wa kuwalamba viatu watawala tangu za enzi za wakoloni, enzi za TANU na zama za CCM.
Tusubiri 28 Oct
 
Back
Top Bottom