Uchaguzi 2020 Moshi: Mkurugenzi akataa kupokea fomu za wagombea kwa sababu walizituhumu sio halisi, awataka wakazithibitishe polisi kwanza

Kwani kazi yake si ni kupokea fomu? Suala la feki au sio feki linaanzia wapi kama ni yeye mwenyewe ndiye alitoa fomu baada ya malipo kufanyika?
Suala feki limeanzia kwa wachukua fomu mkuu.
 

Mmmh, mkuu unatumia nguvu kubwa kujaribu kutetea uovu, lakini Logic inakataa.
 
Kimasihara tu inch inaweza kuingia pabaya
 
Mimi naichukia CCM lakini hatamimi ningelikuwa huyo Mkurugenzi ningezikataa hizo Fomu mpaka zithibitishwe na Polisi kwani Hapo Mtego ni 50/50 Kati ya Chadema na Mkurugenzi.
Kila mmoja hapo anaweza kumuingiza Mkenge mwenzake asiponipanga.

Mtego wa Chadema:
Fomu walizozituhumua kuwa ni Feki wamezijaza na kuzirudisha kwa Waliyemtuhumu! Kama Mkurugenzi aliwapa Fomu OG Chadema wanaweza kurudisha Fake na kumueke Mtego Mkurugenzi kuwa aliwapa Fomu Fake na wana ushahidi wa Kwenda Polisi kutoa Taarifa na Ushahidi wa Barua ya kueleza wasiwasi wao.

Mtego wa Mkurugenzi:
Kama aliwapa Fomu Fake Chadema anasubiri wazirudisha na kuwaondosha kwenye Kugombea huku akiwaripoti Polisi kuwa Chadema wametengeneza Fomu Fake kuichafua Serikali, Na atadai yeye aliwapa Fomu OG.

Hapo kiufupi Wanategana lakini DED kawa mjanja.
 
..tatizo pia ni mamlaka ya nidhamu na uteuzi ya huyo mkurugenzi.

..kwasababu mkurugenzi ameteuliwa toka serikali kuu, basi anakuwa haheshimu watu alioteuliwa kuwatumikia, ambao ni wananchi wa halmashauri husika.
 
Dah hii ni mbaya sana kwa Upendo na amani ya taifa hili
 
Mimi naichukia CCM lakini hatamimi ningelikuwa huyo Mkurugenzi ningezikataa hizo Fomu mpaka zithibitishwe na Polisi kwani Hapo Mtego ni 50/50 Kati ya Chadema na Mkurugenzi...
OCD alimtonya. Huu mwaka huu! Mhn
 
Kama hawana imani nae wasishiriki uchaguzi wa hayo majimbo. Serikali za mitaa mliwakatili wenyeviti kisa tu nyie hamgombei, tuone sasa mkisusa na huu uchaguzi.
 
Tofauti moja ya mashine mkuu....lakini zote za ofisi moja.

Labda kitabu kiliisha....au wa CCM mashine ilikuwa inasumbua...

Mkurungezi ana majibu.
 
mie namshangaa sana jiwe, kama hataki ushindani anashindwa nn kufuta rasmi uwepo wa vyama pinzani hapa tz?? ijulikane duniani kote kwamba nchi yetu ni mfumo wa chama kimoja...Full Stop!.
 
Tofauti moja ya mashine mkuu....lakini zote za ofisi moja.

Labda kitabu kiliisha....au wa CCM mashine ilikuwa inasumbua...

Mkurungezi ana majibu.
Alipaswa ku clear hiyo doubt right away bila kupotezeana muda na maneno mengi yasiyo na maana

Hii nchi ikiharibika msije kusema hakuna walio onya juu ya viashiria hivi vya kipumbavu kabisa
 
Mmmh, mkuu unatumia nguvu kubwa kujaribu kutetea uovu, lakini Logic inakataa.
Kwangu logic itakataa nitakapo msikia mkurungezi akisema aliwapa wagombea wengine fomu zisizo fanana bila sababu maalum mkuu.

Kwa hiyo wagombea wa vyama vingine hawajarudisha! Je, zimepokelewa au wanasubiri uteuzi kisha waambiwe fomu zao ni feki.

Uteuzi haupo mbali tusubiri tuone...maana kwa maelezo ya mwenyekiti wa CDM sio CDM tu waliopewa hizo fomu...hata NCCR.

Je, NCCR wamesharudisha? Zimekubaliwa? Tusubiri kwenye uteuzi.
 
Alipaswa ku clear hiyo doubt right away bila kupotezeana muda na maneno mengi yasiyo na maana

Hii nchi ikiharibika msije kusema hakuna walio onya juu ya viashiria hivi vya kipumbavu kabisa
Binafsi baada ya hii video nimewafutilia hawa watu...wanamivutano ya wenyewe kwa wenyewe.

Ukiondoa siasa...wana mambo binafsi. Wanavutana saana.

Ngoja nihifadhi maneno.
 
Unashabikia dhuluma tu.
Watu kama nyie ni kwenda motoni moja kwa moja.
Je umesahau dhuluma ya uchaguz wa serikali za mitaa?

Taifa la wizi wizi na udanganyifu
Ni kwa nini tunawanyima wananchi haki ya kuchagua viongozi wao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…