Uchaguzi 2020 Moshi: Mkurugenzi akataa kupokea fomu za wagombea kwa sababu walizituhumu sio halisi, awataka wakazithibitishe polisi kwanza

Uchaguzi 2020 Moshi: Mkurugenzi akataa kupokea fomu za wagombea kwa sababu walizituhumu sio halisi, awataka wakazithibitishe polisi kwanza

wacha ujinga. Wangefuata ushauri wako Mkurugenzi angezipokea na Kisha tarehe 26 angewakata kwa kuto kurudisha fomu halali

WALIKOSEA KUSIKILIZA USHAURI WA CCM. HAPO WANGEJIFANYA KAMA HAWAJUI CHOCHOTE ALAFU WANGEZIRUDISHA MAPEEMA WAONE KAMA ZINGEKATALIWA AU LA MI BINAFSI NAMUUNGA MKONO MKURUGENZI
 
Bila tume huru wapinzani wanajisumbua tu. Huyu msimamizi anaonekana hata kwambali kwamba hawezi tangaza ushindi kwa mpinzani kwa namna yeyote hata ashinde kwa 90%.
Umenena vema vema mkuu
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Inatakiwa Apasuliwe Mkurugenzi mmoja ili wengine watie akili. [/QUOTE said:
Jf bhana
But n kweli inaonekana wana tabia ambayo inaotea mizizi kabisa
We're in zero-tolerance zone now
 
Wagombea wa CHADEMA Moshi wakataliwa kupokelewa fomu zao na Mkurugenzi

Huyu mkurugenzi Castory Msigala majibu yake hajakaa kama ni mtumishi wa kutumikia umma, anatoa kauli kama vile ofisi ya Mkurugenzi ni ofisi binafsi ya mtu au ya CCM Mpya.

Masuala haya kuwasukumiwa Polisi kuingilia mchakato wa uchaguzi kufanya uchunguzi wakati ameteuliwa kuwa Msimamizi wa Uchaguzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na ana mamlaka ya kusikiliza na kutatua changamoto zozote kwa niaba ya Tume ya Uchaguzi inatia shaka anavyoamua kutotoa ushirikiano ili majibu na hatua sahihi zichukuliwe wagombea wapate haki yao.
 
Sijui viongozi wa chadema wote akili zao zinafanana yani amepewa fomu akasema ni feki Sasa hiyo feki unarudishaje wakati haijathibitishwa??
 
Mkurugenzi anatakiwa kuwa na hekima kuliko alivyoonyesha. Yeye kama msimamizi hana haki yakukataa fomu yeyote ambayo ameitoa mwenyewe hata kama wanaoirudisha wameonyesha wasiwasi nazo. Yeye ni mtumishi wa umma na wananchi wote ndio mabosi wake. Alitakiwa awathibitishie kuwa hizo fomu walizopewa ni halali kwa kuwaonyesha fomu nyingine zinazofanana nazo. Badala ya kususa alitakiwa awaandikie kuwa atapokea fomu zote zilizotolewa na ofisi yake pamoja na risiti tofauti zilizotolewa. Lugha ya kusema kuwa hawezi kuziamini kwa sababu mtu yeyote anaweza kuchonga mhuri ni kuthibitisha hofu ya hawa wagombea kuwa alikuwa na mpango wa kuzikataa toka awali. NEC nao wanatakiwa kutoa maamuzi mapema panapotokea sintofahamu kama hizi.

Amandla...
Lililopo..

Nimekupa fomu kisha ukasema ni feki.

Kisha ukaijaza na kuirudisha...so far does it make sense to you sir?

Mimi kama fomu niliyopewa ingekuwa feki ningeirudisha bila kuijaza na kudai iliyo halali maana kama naijua feki basi iliyohalali naijua vema.

Ukinirudishia fomu uliyoijaza huku uliita feki kuna mengi...kwanza ulikurupuka kunichafua. Pili, je nitajibu nini kama fomu uliyoirudisha kweli ni feki na ni mtego, niliyokupatia ilikuwa halali hivyo ulifanya mchezo wa kuset minds za watu kwamba nimekupq feki ilihali ilikuwa halali...sasa wakati wa kurudisha unarudisha feki.
 
Wakitandikwa wakurugenziccm kama wawili watatu kipigo cha mbwa koko ndipo CCM itazinduka na kuacha ufala wao

Hivi umemsikiliza mkurugenzi kweli? Kosa lake ni lipi?
 
wamelianzisha wenyewe sasa waiona ngondo wafunga milango
 
Sasa mkurugenzi kakosea nini hapo?

Wewe unapewa fomu kisha unasem ni feki halafu unataka uirudishe kwa aliyekupa fomu feki tena.

Huyo jamaa wanayemuita katibu analisauti likubwa tu na anaongea saana ila kichwani hamna kitu.

Hata mimi nisingeipokea...nenda kqnishtaki nimekupa fomu feki...ili nishtakiwe kwa kujaribu kukurubuni.
Kwani kazi yake si ni kupokea fomu? Suala la feki au sio feki linaanzia wapi kama ni yeye mwenyewe ndiye alitoa fomu baada ya malipo kufanyika?
 
Sasa mkurugenzi kakosea nini hapo?

Wewe unapewa fomu kisha unasem ni feki halafu unataka uirudishe kwa aliyekupa fomu feki tena.

Huyo jamaa wanayemuita katibu analisauti likubwa tu na anaongea saana ila kichwani hamna kitu.

Hata mimi nisingeipokea...nenda kqnishtaki nimekupa fomu feki...ili nishtakiwe kwa kujaribu kukurubuni.
Hebu mtaalam tusaidie kwanini wagombea wa ccm wamepewa risiti ya halmashauri na wengine wasipewe wapewe ya tofauti?

Kwanini risiti za wagombea ubunge zimeandikwa za wagombea udiwani?

Acheni kujifanya mna akili sana kuliko wengine
Muda mwingine ficheni upumbavu
 
Lililopo..

Nimekupa fomu kisha ukasema ni feki.

Kisha ukaijaza na kuirudisha...so far does it make sense to you sir?

Mimi kama fomu niliyopewa ingekuwa feki ningeirudisha bila kuijaza na kudai iliyo halali maana kama naijua feki basi iliyohalali naijua vema.

Ukinirudishia fomu uliyoijaza huku uliita feki kuna mengi...kwanza ulikurupuka kunichafua. Pili, je nitajibu nini kama fomu uliyoirudisha kweli ni feki na ni mtego, niliyokupatia ilikuwa halali hivyo ulifanya mchezo wa kuset minds za watu kwamba nimekupq feki ilihali ilikuwa halali...sasa wakati wa kurudisha unarudisha feki.

Umenipa fomu nikasema feki.

Nikaijaza, ukaihakiki na kuipokea kwamba iko sawasawa na kuniteua kugombea. Nitaonekana na jamii kuwa nilikurupuka na kwa vile mimi ni muungwana nitakuomba msamaha na wewe utajengeka katika macho ya jamii kuwa ni mtenda haki.

Nikaijaza, ukakataa kuipokea kwa vile ni feki na sio fomu halisi. Nitawarudia wote niliowaambia toka awali kuhusu wasiwasi wangu kuwa una nia mbaya na mimi. Jamii itakuhukumu na utaonekana kweli wewe hauko hapo kwa ajili ya haki bali kufanya upendeleo kwa baadhi ya wagombea.

Nikakataa kuijaza, na wewe ukakataa kunipa mpya kwa maelezo kuwa uliyonipa ni halali. Siku ya siku ikifika unatoa taarifa kuwa nimejitoa kwa kutorudisha fomu yeyote iliyojazwa. Jamii itanihukumu mimi kwa kukurupuka na kukupa upenyo wa kunitoa katika mpambano kihalali kabisa.

Kuhusu mimi kurudisha fomu feki wakati umenipa iliyo halali haiingii kichwani kwa sababu nia yangu ni kugombea. Kwa mtaji huo, sina sababu yeyote ya kubadilisha fomu halali kwa feki. Aidha, unaweza kuniambia hii fomu uliyoleta ni feki na ukanipa nyingine halali ili niirudishe katika wakati muafaka ambao utakubaliwa na NEC. Kwa kufanya hivyo nitakuwa nimeumbuka.

Mimi naona matatizo yanatokea kwa sababu baadhi ya watumishi wa umma wanasahau kuwa wao ni watumishi wetu na wanatakiwa kuwa wanyenyekevu kwa raia wote na sio wale tuu waliomshinda mamlaka.

Amandla...
 
Sasa mkurugenzi kakosea nini hapo?

Wewe unapewa fomu kisha unasem ni feki halafu unataka uirudishe kwa aliyekupa fomu feki tena.

Huyo jamaa wanayemuita katibu analisauti likubwa tu na anaongea saana ila kichwani hamna kitu.

Hata mimi nisingeipokea...nenda kqnishtaki nimekupa fomu feki...ili nishtakiwe kwa kujaribu kukurubuni.
100% correct
 
Back
Top Bottom