Uchaguzi 2020 Moshi: Mkurugenzi akataa kupokea fomu za wagombea kwa sababu walizituhumu sio halisi, awataka wakazithibitishe polisi kwanza

Uchaguzi 2020 Moshi: Mkurugenzi akataa kupokea fomu za wagombea kwa sababu walizituhumu sio halisi, awataka wakazithibitishe polisi kwanza

Lile la risti linaweza kuwa logic.
Na wakiishafuatialia hivyo akathibitisha ni malipo halali ..Sawa

Hili la fomu Mkurugenzi yuko sahihi, na nashangaa kama zilikuwa fake kwanini walijaza na kurudisha? Je zikitupwa kuwa wamefoji?

Kama wanarudisha huku walusema si halali waende polisi zikathibishwe warudishe, . Hapa CDM hawako . Sahihi
 
CDM nao wanajichanganya.
Kwa maelezo yaliyo kwenye clip. Hapo Kuna kujichanganya. Ila walio kwenye uwanja. CDM na Mkurugenzi wanajua zaidi.
 
Wakitandikwa wakurugenziccm kama wawili watatu kipigo cha mbwa koko ndipo CCM itazinduka na kuacha ufala wao
Kosa lake ni lipi hapo? Walioanza kusema wamepewa fomu fake ni Chadema wenyewe. Sasa kama mtu unahisi umepewa fomu fake si unatakiwa kuithibitisha polisi kabla ya kuirejesha?
 
Mengine wanayataka fomu walikaa nazo siku zote ili iweje,
 
🙂 🙂 🙂 mengine inabidi mtu ucheke tu!!
Hapo ina maana Mkurugenzi anatimiza wajibu wake kiweledi na busara!!???
 
Sasa fomu orijino inathibitishwaje polisi? Fomu inathibitishwa kukiwa na copy yake
Tena si polisi bali na wakili au mahakama!! Ila bw. DED msomi anaelekeza zikathibitishwe polisi!!!
Hakika tutaona mengi chini ya tawala za CCM na wateule wao
 
Mkurugenzi anatakiwa kuwa na hekima kuliko alivyoonyesha. Yeye kama msimamizi hana haki yakukataa fomu yeyote ambayo ameitoa mwenyewe hata kama wanaoirudisha wameonyesha wasiwasi nazo. Yeye ni mtumishi wa umma na wananchi wote ndio mabosi wake. Alitakiwa awathibitishie kuwa hizo fomu walizopewa ni halali kwa kuwaonyesha fomu nyingine zinazofanana nazo. Badala ya kususa alitakiwa awaandikie kuwa atapokea fomu zote zilizotolewa na ofisi yake pamoja na risiti tofauti zilizotolewa. Lugha ya kusema kuwa hawezi kuziamini kwa sababu mtu yeyote anaweza kuchonga mhuri ni kuthibitisha hofu ya hawa wagombea kuwa alikuwa na mpango wa kuzikataa toka awali. NEC nao wanatakiwa kutoa maamuzi mapema panapotokea sintofahamu kama hizi.

Amandla...
Wakurungezi waliopo waliokotwa kwenye NGOs,wakapewa madaraka wakaajiriwa.kwa mantiki hiyo hawajui uongozi na hawana uzoefu serikalini.
 
Wagombea wa CHADEMA Moshi wakataliwa kupokelewa fomu zao na Mkurugenzi.
======

Mkurugenzi amegoma kupokea fomu baada ya tuhuma za awali kwamba sio halisi na kutaka kabla wahusika hawajazirudisha wakathibitishe polisi kama ni halisi ama La.

Baada ya katibu wa CHADEMA kuhoji iwapo vyama vyote vinaenda polisi kuthibitisha, amejibu yeye aliemtuhumu na wote waliomtuhumu ndio wanatakiwa kwenda polisi kuzithibitisha kabla hawajazileta kwake.

Pia katibu wa CHADEMA alilalamikia kuwa na risiti za aina mbili kwa wagombea wa CCM na CHADEMA ambapo risiti za CHADEMA zimekuwa printed kwenye computer ilhali za CCM ni stakabadhi ya halmashauri.

Kuhusu hilo mkurugenzi, amemtaka kuwasilisha kwa maandishi malalamiko yao na yeye atakaa na wataalam kuangalia kipi ni kipi lakini amesema uko utata, zipo ambazo ni stakabadhi kama za mahakama, nyingine za mfumo na nzuri ni ya stakabadhi lakini wakitaka majibu wawasilishe malalamiko yao.

Pia mwenyekiti amelalamika suala la risiti ya mgombea ubunge kuandikwa ni ya mgombea udiwani, mkurugenzi ametaka wayawasilishe wamalizane.

=====

Kwa upande wake mkurugenzi amesema ametoa fomu halali na CHADEMA wakaandika barua na kumpelekea wakimtuhumu amewapa fomu zisizo halisi na baadae kwenda polisi. Ikabidi awaandikie kwamba hilo suala halina shida lakini kwa kuwa wameenda polisi, yeye hana uweza wa kutambua kitu 'fake' hivyo watafute mamlaka yenye weledi wa kutambua hivyo asingeweza kuzipokea.

Hiyo siyo haki; mkurugenzi afuate sheria tu.
 
Duu, ni ile kauli nimekupa gari, nakulipa mshahara na marupurupu haalafu eti utangaze .........! au analipa fadhila! sasa polisi watathibitishaje ilhali yeye ndie alizitoa? Vituko katika ubora wake
 
Dah hii ni mbaya sana kwa Upendo na amani ya taifa hili
Hakuna ubaya wowote ni hisia zako tu mkuu
Hao viongozi wa chadema hawajui wanae pambana naye sasa unamtuhumu mtu ambaye kesho unarudi tena kwake sio ujuha huo bora Basi madai yangekua ya kweli Mimi naona chadema imekosa watu wenye hekima kuanzia ngazi za juu hadi viongozi wa chini
 
Hayo ya kwenda p1 ni sheria au ndo uzumbukuku ulionao?
Chadema ujuaji utawaponza sana. Fomu amewapa yeye lakini na vyama vingine vimepewa. Kwanini nyinyi ndio munaona mumeonewa?. Hao wengine wanasemaje? Kama kuna hofu ya hivyo kwanini musiende wote kwa pamoja na vyama vingine kulitatua hilo suala?
 
CHADEMA wataka TUME YA UCHAGUZI kumuondoa msimamizi wa uchaguzi Moshi Vijijini ambaye ni mkurugenzi wa wilaya Castory Msigala kwa vile hawana imani naye kutokana na matendo na mienendo yake ktk kazi ya kusimamia mchakato mzima wa kuelekea katika kufanyika uchaguzi mkuu ulio wa haki na huru oktoba 2020.

Mfano fomu walizopewa CHADEMA zinautofauti mkubwa na zile fomu walizopewa wagombea wa CCM.

Risiti kwa ajili ya malipo walizopewa CHADEMA kwa ajili ya fomu zinautofauti na risiti walizopewa CCM kwa ajili ya kufanyia malipo.

Mkurugenzi amekiri fomu zina utofauti na mkurugenzi hana uwezo wa kutambua fomu halali au la.

Chanzo: Mwananchi digital
Kumbe ni huu jamaaa!! Kada kindakindaki na maslahi wa chama pendwa, kitambo saaana. Yupo tayari kwa lolote ili mradi anachokisimamia kisifeli. Alikuwa Songea akahamishiwa Mbeya huko, kumbe sasa yupo huko??. Tuendelee kumuombaMungu wa kweli aonyeshe Muujiza kwenye haya matendo. Kwa haya yanayoendelea Mungu tusaidie
 
Back
Top Bottom