Moshi: Padri wa Kanisa Katoliki alaani walioiba sadaka kanisani

Moshi: Padri wa Kanisa Katoliki alaani walioiba sadaka kanisani

hakuna shida yeyote waibe tuu sadaka zenyewe niwizi mtupu wanaibia wahumini😅sadaka yavipaji,majitoleo🤣🤣🤣🤣🤣wakiristo wezi kishenzi🤣🤣
 
Paroko wa Parokia ya Narumu, Kata ya Machame Mashariki, Padri Thomas Chuwa amelaani vikali katika ibada ya Misa Takatifu kitendo kilichofanyika katika Ibada ya Jumapili iliyopita ambapo watu / mtu wasiojulikana wameiba kapu la sadaka kanisani.

Sadaka hizo zilikuwa ni majitoleo ya shukrani, vipaji pamoja na sadaka ya Misa Takatifu katika Ibada ya Misa ya kwanza ya Jumapili iliyopita.

Padri Chuwa amewaasa waamuni wa kanisa hilo kusali Sala Maalum kwa muda wa siku tatu kwa ajili ya watu/mtu huyo aliyeiba sadaka hizo na kuwa kitendo hicho kilichofanyika kanisani hapo ni kibaya sana na anamkabidhi Mungu.
Novena ya siku tatu
 
Kule geita wameingia na kuharibu vitu vya ndani ya kanisa, haya sasa moshi nako wameiba sadaka. Swali la kuuliza ni kina nani hao wanaoingia makanisani na kufanya uhuni huo? Kama si wenyewe wanayoyajua mazingira yao?

Kanisa katoliki ni taasisi kubwa na ina mali nyingi za thamani hivyo kulazimika kuwa na ulinzi mkali. Ulinzi wote huo mkali kibaka au jambazi ataingilia wapi?

Anyway kama hali imefikia mpaka watu wanaiba makanisani bila hofu ya Mungu basi maadili ya kiroho yameporomoka kwa kiwango cha kutisha
Usikute ndo mambo kama ya kipind kile yameanza
 
Hii inanikumbusha kisa cha mwizi msalabani, aliokolewa.
 
hata mimi hilo suala la sala maalamu siungi mkono amuachie Mungu tu
Unamuachiaje bila kusema na yeye! na njia ya kusema na Mungu ili umuachie Ni sala. Tunasema na Mungu kwa njia ya Sala!
Kwahiyo kanisa imetennga siku tatu ili kusema na Mungu Juu ya Jambo Hilo ili kumuachia mapenzi yake yatimizwe! Kwahiyo usipinge usilolijua!
 
Stress Challenger na Mokiti muache wizi
20230225_225606.jpg
 
Back
Top Bottom