peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,949
Mkurugenzi wa Moshi Manispaa, amelala na kusinzia, sasa wezi wameiba na solar na taa takribani betri 50 na solar panels 30 na taa zimeibiwa na zinaendelea kuibiwa kwenye Barabara ya Nyerere (Nyerere Road) kuelekea kiwanda cha soda cha Bonite.
Hii ni zaidi ya hatari na tukiendelea kukaa kimya watazimaliza, viongozi saidieni kumuondoa mkurugenzi anasimamia watu wanaohujumu miundombinu ya Watanzania.
Uongozi wa mkurugenzi una matatizo makubwa.
Angalieni picha hizi hapa👇
UPDATE_JULY 28, 2024
Moshi. Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ipo tayari kurejesha taa za barabarani za umeme wa jua (sola) 120 zilizoibwa katika wimbi linaloendelea la wizi, lakini kwanza inataka kufahamu kiini cha kuibuka kwa uhalifu huo.
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi wa manispaa hiyo, Mwajuma Nasombe wakati akijibu malalamiko ya wananchi wanaohoji ukimya wa halmashauri kufunga taa mpya na kurejesha taa katika barabara hizo muhimu.
Kwa miaka mitatu mfululizo, Mji wa Moshi na vitongoji vyake umeshuhudia wimbi kubwa la wizi wa taa hizo za sola pamoja na betri zake. Barabara zilizoathirika zaidi ni Sukari, Zara au Tembo na Bonite pamoja na baadhi ya kata.
Mwananchi