Moshi: Yanayojiri katika Kongamano la BAWACHA Siku ya Wanawake Duniani Machi 3, 2023; Rais Samia mgeni rasmi

Ni Asubuhi tulivu siku ya Jumatano tarehe 8 March ikiwa ni kilele Cha Siku ya Wanawake Duniani.

Macho na masikio ya Watanzania leo yanaelekezwa katika mji maarufu wa Moshi mkoani Kilimanjaro.

Chama kikuu Cha Chadema chenye wafuasi takribani Milioni 10 nchini kupitia Baraza lake la Wanawake Bawacha linafanya Kongamano kubwa la kuadhimisha siku hii ya Wanawake Kitaifa katika Ukumbi wa KURINGE.

Kinachovutia kwenye Kongamano hili la Bawacha mwaka huu ni mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye atakuwa mgeni Rasmi kwenye Kongamano hilo.

Kukubali kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni Rasmi kwenye Kongamano la Chadema kumevuta hisia za mamilioni ya Watanzania na hata Jamii ya Kimataifa.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ndiye atakayekuwa mwenyeji wa Rais Samia na anatarajia kumpokea kuanzia saa 3 asubuhi.

Rais Samia kuhutubia Jukwaa moja na Chama kikuu Cha Upinzani Chadema kinaonyesha kilele Cha mafanikio ya Maridhiano ya kisiasa yaliyoasisiwa na Rais pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.

Rais Samia Suluhu Hassan amesikika mara kadhaa akitangaza hadharani kwamba wapinzani nchini siyo maadui wake tofauti na mtangulizi wake John Magufuli aliyejiapiza kuangamiza upinzani nchini na hatimaye kuuvuruga uchaguzi mkuu wa mwaka 2020

Mji wa Moshi ambao ni Kati ya ngome kuu za Chadema nchini umepambwa na bendera nyingi za chama hicho kikuu Cha Upinzani huku mazungumzo katika mikusanyiko mbalimbali ikiwa ni tukio hili la kihistoria.

Molemo Media tunatarajia kuwaletea mubashara matukio yote muhimu yatakayoendelea hapa ukumbini mjini Moshi kabla na wakati wa Kongamano hilo

Karibuni Sana
Ulipotea kabisa toka kesi ya Mbowe, I missed you a lot!
 
Shwange kutoka mitaa ya Moshi
 
Tukae kwa kutulia tukiwa tunasubiri hotuba nzito ya Bawacha itayoenda kuligusa taifa letu
 
Baadhi ya mabango yaliyoandaliwa na BAWACHA
IMG-20230308-WA0021.jpg
 
Awamu zilizopita Ilikuwa siyo rahisi TBC kujihusisha na mambo positive ya vyama vya upinzani.

Lakini matunda ya Maridhiano sasa ni dhahiri leo Kongamano la BAWACHA la Siku ya Wanawake Duniani litarushwa live na TBC.

Mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya mMuungano wa Tanzania Mama Samia.

Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA pia atahudhuria pamoja na viongozi wengine wa vyama mbalimbali walioalikwa.
 
Awamu zilizopita Ilikuwa Siyo rahisi TBC kujihusisha na mambo positive ya vyama vya upinzani

Lakini matunda ya Maridhiano sasa ni dhahiri Leo Kongamano la BAWACHA la Siku ya Wanawake Duniani litarushwa live na TBC

Mgeni rasmi ni mh Rais wa JMT mama Samia

Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema pia atahudhuria pamoja na viongozi wengine wa vyama mbalimbali walioalikwa
Maajabu yako wapi wakati wanaenda kusifia harakati za mama.
 
Tbc ni television ya Taifa ila wanazidiwa akili na Millars Ayo...Wanataka kujbrand kupitia Huu mkutano,hawana Tofauti na Mandonga.
 
Ni Asubuhi tulivu siku ya Jumatano tarehe 8 March ikiwa ni kilele Cha Siku ya Wanawake Duniani.

Macho na masikio ya Watanzania leo yanaelekezwa katika mji maarufu wa Moshi mkoani Kilimanjaro.

Chama kikuu Cha Chadema chenye wafuasi takribani Milioni 10 nchini kupitia Baraza lake la Wanawake Bawacha linafanya Kongamano kubwa la kuadhimisha siku hii ya Wanawake Kitaifa katika Ukumbi wa KURINGE.

Kinachovutia kwenye Kongamano hili la Bawacha mwaka huu ni mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye atakuwa mgeni Rasmi kwenye Kongamano hilo.

Kukubali kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni Rasmi kwenye Kongamano la Chadema kumevuta hisia za mamilioni ya Watanzania na hata Jamii ya Kimataifa.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ndiye atakayekuwa mwenyeji wa Rais Samia na anatarajia kumpokea kuanzia saa 3 asubuhi.

Rais Samia kuhutubia Jukwaa moja na Chama kikuu Cha Upinzani Chadema kinaonyesha kilele Cha mafanikio ya Maridhiano ya kisiasa yaliyoasisiwa na Rais pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.

Rais Samia Suluhu Hassan amesikika mara kadhaa akitangaza hadharani kwamba wapinzani nchini siyo maadui wake tofauti na mtangulizi wake John Magufuli aliyejiapiza kuangamiza upinzani nchini na hatimaye kuuvuruga uchaguzi mkuu wa mwaka 2020

Mji wa Moshi ambao ni Kati ya ngome kuu za Chadema nchini umepambwa na bendera nyingi za chama hicho kikuu Cha Upinzani huku mazungumzo katika mikusanyiko mbalimbali ikiwa ni tukio hili la kihistoria.

Molemo Media tunatarajia kuwaletea mubashara matukio yote muhimu yatakayoendelea hapa ukumbini mjini Moshi kabla na wakati wa Kongamano hilo

Karibuni Sana
MASAHIHISHO - Kwa Mujibu wa Daftari la Chadema Digital , Chadema ina wanachama Mil 15.4
 
Back
Top Bottom