Moshi: Yanayojiri katika Kongamano la BAWACHA Siku ya Wanawake Duniani Machi 3, 2023; Rais Samia mgeni rasmi

Moshi: Yanayojiri katika Kongamano la BAWACHA Siku ya Wanawake Duniani Machi 3, 2023; Rais Samia mgeni rasmi

Enzi za chadema ilipokuwa chadema chini ya Mwamba Dr. Slaa uzi kama huu saa hii ungekuwa na coments zaidi ya 600
 
Mbali na Malemo tv Gani nyingine (local) itaonesha maana naona TBC hawana habari na Moshi.
 
MASAHIHISHO - Kwa Mujibu wa Daftari la Chadema Digital , Chadema ina wanachama Mil 15.4
Hata El Sahaaf hakuwa hivyo kwa propoganda. Yaani kwa dakika chache tu mwenzako kasema milioni 10 wewe unasema milioni 15. Weka ushahidi hapa.Hata timu za Kariakoo zinajinasibu kuwa na wanachama milioni 10!
If wishes were horses beggars would ride.

Unatukana akili za watu.Wakati mwingine shirikisha ubongo.
 
Ni Asubuhi tulivu siku ya Jumatano tarehe 8 March ikiwa ni kilele Cha Siku ya Wanawake Duniani.

Macho na masikio ya Watanzania leo yanaelekezwa katika mji maarufu wa Moshi mkoani Kilimanjaro.

Chama kikuu Cha Chadema chenye wafuasi takribani Milioni 10 nchini kupitia Baraza lake la Wanawake Bawacha linafanya Kongamano kubwa la kuadhimisha siku hii ya Wanawake Kitaifa katika Ukumbi wa KURINGE.

Kinachovutia kwenye Kongamano hili la Bawacha mwaka huu ni mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye atakuwa mgeni Rasmi kwenye Kongamano hilo.

Kukubali kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni Rasmi kwenye Kongamano la Chadema kumevuta hisia za mamilioni ya Watanzania na hata Jamii ya Kimataifa.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ndiye atakayekuwa mwenyeji wa Rais Samia na anatarajia kumpokea kuanzia saa 3 asubuhi.

Rais Samia kuhutubia Jukwaa moja na Chama kikuu Cha Upinzani Chadema kinaonyesha kilele Cha mafanikio ya Maridhiano ya kisiasa yaliyoasisiwa na Rais pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.

Rais Samia Suluhu Hassan amesikika mara kadhaa akitangaza hadharani kwamba wapinzani nchini siyo maadui wake tofauti na mtangulizi wake John Magufuli aliyejiapiza kuangamiza upinzani nchini na hatimaye kuuvuruga uchaguzi mkuu wa mwaka 2020

Mji wa Moshi ambao ni Kati ya ngome kuu za Chadema nchini umepambwa na bendera nyingi za chama hicho kikuu Cha Upinzani huku mazungumzo katika mikusanyiko mbalimbali ikiwa ni tukio hili la kihistoria.

Molemo Media tunatarajia kuwaletea mubashara matukio yote muhimu yatakayoendelea hapa ukumbini mjini Moshi kabla na wakati wa Kongamano hilo

Karibuni Sana
Mimi kama Mimi nawapongeza wote waliofanikisha maridhiano.Kwa wengi damage has already been done lakini kila yule aliyechangia kuliunganisha taifa apewe anachostahili.
 
Enzi za chadema ilipokuwa chadema chini ya Mwamba Dr. Slaa uzi kama huu saa hii ungekuwa na coments zaidi ya 600
Na enzi za baba yako hili kongamano lisinge kuwepo
 
Hayo ndio matokeo ya maridhiano, pale unapoambiwa na mwenzio siasa sio uadui, hapo mnaanza kukaribishana mpaka nyumbani, ajabu wanafiki wanataka hayo maridhiano yasihusishe ruzuku hata kama ipo kisheria, lakini yaguse pengine pote.
Hao watu ni maadui wa mama Tanzania na wanaumwa Apedomia.Yuko wapi mwalimu mkuu wa watu? Alimtabiria Mbowe kuwa ni miongoni mwa wajenzi wa Tanzania mpya.
 
Angekuwepo shwetaani wa afrika, ukumbi wangejazwa FFU wakiwa na mabom, mbwa, bunduki na washawasha.

lakn leo mama anaenda na kalamu na notibuku ili kuchukua changamoto za watanzania wenzake ambao ni wanachama wa chadema na anazitatua.

maRPC na OCDs watapeana mikono na makamanda wenzao wa heshima wa chadema badala ya kuwachota tanganyika jeki na kuwasukuma ndani.

MAMA TUNAOMBA MAOFISA WOTE WALIOKUWA WANATUMIWA NA SHETANI WA AFRIKA UWAKAMATE NA KUWASWEKA LUPANGO.
Pesa mingi hauna, bima kubwa hauna, usafiri hauna hata wa baiskeli, unaishi kwa kuunga unga kama mbwa, watoto ndio umefanikiwa kuzaa wa wanawake watano tofauti tofauti yaani kifupi future yako ni nyeusi. Huyo mama pesa anazo, anaweza kukusweka ndani hata sasahivi na usitoke milele, ana uhakika wa maisha yake na kizazi chake. Amka mtu mweusi ulikwisha laaniwa enzi na enzi
 
Hizi kura za hawa wanachama huwa zinakwendaga wapi?!.

Ni ulikuwa ngome enzi zile, sasa Chadema haina tena mbunge hata mmoja!, hii ni ngome gani?.
P
Yaani bwna Njaa hivi siku hizi umekuwaje? Umekuwa kama Mgalatia! Ni nani aliyekuroga? Je,unaamini Chademaninakosa wabunge kihalali? Wewe ni natural lawyer ama ni positive lawyer?
 
Hata El Sahaaf hakuwa hivyo kwa propoganda. Yaani kwa dakika chache tu mwenzako kasema milioni 10 wewe unasema milioni 15.
Weka ushahidi hapa.Hata timu za Kariakoo zinajinasibu kuwa na wanachama milioni 10!
If wishes were horses beggars would ride.
Unatukana akili za watu.Wakati mwingine shirikisha ubongo.
😄😄😄
 
Ni Asubuhi tulivu siku ya Jumatano tarehe 8 March ikiwa ni kilele Cha Siku ya Wanawake Duniani.

Macho na masikio ya Watanzania leo yanaelekezwa katika mji maarufu wa Moshi mkoani Kilimanjaro...
Mama apewe kadi kubwa kubwa ya CHADEMA hapo Moshi asiondoke hivi hivi.
 
Mh. Mbowe ameingia tayari kwa kumkaribisha Mgeni rasmi Mheshimiwa Rais Samia Suluhu .
=
1678262104935.png

=
 
Hata El Sahaaf hakuwa hivyo kwa propoganda. Yaani kwa dakika chache tu mwenzako kasema milioni 10 wewe unasema milioni 15.
Weka ushahidi hapa.Hata timu za Kariakoo zinajinasibu kuwa na wanachama milioni 10!
If wishes were horses beggars would ride.
Unatukana akili za watu.Wakati mwingine shirikisha ubongo.
Hutaki Unaacha
 
Back
Top Bottom