Wizara ya Ardhi
Govt Institution
- May 14, 2024
- 306
- 165
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Ndugu Godfrey Mnzava, amekabidhi hati 50 za ardhi kwa Wananchi wa Kijiji cha Koresa, Kata ya Kirua Vunjo Kusini, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Mfumo wa Ardhi Kliniki Kidijitali, maarufu kama “E-Ardhi Huduma Popote.”
Uzinduzi huo umeenda sambamba na utoaji wa elimu kwa Wananchi 200 kuhusu matumizi ya mfumo wa E-Ardhi, unaowezesha wananchi kupata huduma za ardhi kwa njia ya kidijitali na kurahisisha upatikanaji wa hati za ardhi.
Katika utekelezaji wa zoezi hilo, jumla ya wananchi 890 wamepimiwa ardhi na kuwekwa mawe katika viwanja vyao, hatua inayoweka utambulisho na mipaka rasmi ya maeneo yao.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava amewataka wasimamizi wa upimaji wa ardhi kuhakikisha mipango ya matumizi ya ardhi inazingatia mahitaji ya jamii, ikiwemo kutenga maeneo kwa ajili ya viwanja vya michezo vya watoto, mikutano ya wananchi, shule, barabara, hospitali na taasisi nyingine muhimu.
Amesema upangaji wa maeneo unatakiwa kuangalia mahitaji ya sasa na ya baadaye ili kuepusha changamoto za ukosefu wa maeneo ya huduma za kijamii baada ya makazi kuendelea kukua.
Naye, Diwani wa Kata ya Kirua Vunjo Kusini, Godfrey Mkunde (Nyerere), amesema amefurahishwa kuona zoezi hilo likitekelezwa katika kata yake, akieleza kuwa huduma hiyo itawasaidia wananchi kupata huduma za ardhi kwa urahisi zaidi.
Kwa upande wake, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Bi. Salome Kessy, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha zoezi hilo linakamilishwa kwa muda mfupi, akielekeza kuwa mchakato wa utoaji wa huduma kwa wananchi uzingatie muda wa hadi saa 72.
Naye Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Rehema Mdee, amewataka watendaji wa vijiji na kata kuwaongoza na kuwasaidia wananchi kutumia mfumo huo, ikiwemo kuwasaidia kufungua akaunti zao za E-Ardhi ili waweze kupata huduma za ardhi kwa njia ya kidijitali.