Mossad wapo vizuri kwenye intelijensia

Hahaaa.

Unaona sasa? Ndo maana nikakuambia hayo ni makundi ya wanamgambo tu yasiyo na resources za kutosha.

Ili yaweze kutekeleza hayo inabidi yawe na resources!
 
Sasa hivi IDF inajiandaa na Ground operation ya kwenda kusafisha safisha mabaki ya Hezibollah kusini mwa Lebanoni.
 
Vita ni mbinu na timing
 
israel ana pesa huwez mfananisha na lebanoni..hapo maishariki ya kati akitoka msaudia na uturuki na yeye yumo
Hizo ndio akili Israel amshinde pesa Qatar, UAE, Kuwait unaota nini. Nchi ya kusaidiwa hio kwenda kukinga kibakul8 Washington huoni hata aibu.
 
Kiuwezo Israeli na marekani hawalingani na Hezbollah wao Wana teknolojia ya juu ya silaha na ulinzi wa anga pamoja na ndege Vita ( fighters jets) Hezbollah wangekua na ndege hata 5 tu Israel asingepigana na Lebanon wangetafuta amani kwa njia ya diplomasia.
Israeli anaficha taarifa za madhara anayoyapata lakini kiukweli anashambuliwa sana wao Kila mabomu yalitua watakwambia limeanguka open areas na hakuna madhara. Hii ipo kimkakati zaidi ili kimdhoofisha adui ni mbinu za kivita ili tunapoelekea watatoa kilio nje Kila mtu atasikia.
 
Fauda ni balaa. Hua najiuliza directors wa zile movies wanamakusudio gani?

Israel amejipenyeza kwenye maeneo mengi sana, inakua ngumu kupambana nao kirahisi. Inabidi kichwa kitulie sana.

Uko salama Mzee mwenzangu
Tazama Series moja inaitwa SPY. Inamuelezea jasusi mmoja wa Israel anaitwa ELL COHEN,alijipenyeza kwenye Royal Family ya Rais wa Syria Haffez Assad akikisanya Information kabla ya Vita ya 1967 kati ya Israel na Arabs. Alikamatwa baada ya Vita vya siku 6 lakini alikamilisha Mission yake. Alikamatwa baada ya kuji Expose kwa demu wa kiarabu mtoto wa General wa jeshi wa Syria.
 
Hizo ndio akili Israel amshinde pesa Qatar, UAE, Kuwait unaota nini. Nchi ya kusaidiwa hio kwenda kukinga kibakul8 Washington huoni hata aibu.
Marekani hasaidiagi rofa wewe,hivi kwa mtazamo wako kati ya usa na Israel nani anamnyenyekea mwenzake?jibu unalo
 
Iran hawataki usumbufu na teknolojia yao ya nuclear. Wanakula watapoteza sana. Ila vibaraka wao ndio wanasakiziwa kwenda mbele.
 
Mkuu Kosugi, nini kitafuata unafikiri......Iran haitaki kabisa vita, haiwezi kufanya lolote.....Umesikia hotuba ya Ayatollah lakini? Kaloa na baada ya hotuba kapelekwa mafichoni....
Lazima aingie chombo kabla hajanyonyolewa sharubu zile.
 
Marekani hasaidiagi rofa wewe,hivi kwa mtazamo wako kati ya usa na Israel nani anamnyenyekea mwenzake?jibu unalo
Bwege wewe hizo silaha anazo pewa Israel ni nini hizo kama hasaidiwi. Israel si mafala tu kama wewe, toka lini Israel alipigana vita bila kupewa silaha na kusaidiwa na US.

Israel ni omba omba tu kwa US lini US alienda omba msada kwa Israel, leta dalili zako. Afu tazama misada ya US kwa Israel utapata jibu.

Eti nani anaye mtegemea mwenzie haha. Wewe ni bwege la mwisho kama unamini Israel anatetemekewa na US anatumiwa na US kwa agenda za US
 
Hahaaa.

Unaona sasa? Ndo maana nikakuambia hayo ni makundi ya wanamgambo tu yasiyo na resources za kutosha.

Ili yaweze kutekeleza hayo inabidi yawe na resources!
Tukiachana na Hezbollah ambayo unasema ni militia, inakuwaje Iran ambayo ni nchi na ina resources inafanyiwa mauaji mara kadhaa kwa wanasayansi, ma general wa jeshi rejea Qasem Suleiman, Kiongozi wa Hamas kuuawa nchini mwao Tehran, wao kwanini hawafanyi kulipiza ndani ya Israel.

Siku ile wanarusha drones na missiles kwanini wasipige hata bunge la Israel? Piga jengo la wizara na hata ikulu kabisa...

Tuma majasusi waue hata wakubwa wawili wa jeshi la IDF...

Hili suala ndio maana Lebanese wanaiuza Hezbollah, wanaona Iran ikutumia ardhi za wenzake kama uwanja wa vita, sehemu za kujaribu silaha na kufanyia mafunzo ya kivita kwa askari wake.

Lazima Israel anawachota akili Lebanese na serikali yao kiurahisi kwamba "stop being stupid, Iran inatumia nchi yenu kama uwanja wa vita , wao wanaishi salama, nyie mnaumia, watoto wenu wanakufa" kwa hizo propaganda hata mimi ningeshawishika kwa sababu kuna logical reasoning...

Iran anauliwa Qasem Suleiman, wakatoa taarifa watashambulia kambi za US Iraq, wakapiga missile hawakuua askari hata mmoja...
Yaani Iran ina alert adui, askari wote wakajificha.

Shambulio la juzi Israel, wanatoa taarifa watalipa kisasi, matokeo yake US na EU, Jordan wakaweka air defenses kulinda anga la Israel... Wakapiga maeneo baadhi hakuna hata damage ya maana iliyotokea...

Vitendo kama hivi anavyofanya Iran vinaleta sintofahamu na maswali.

Iran haitaki kabisa kujiingiza vitani, inatumia Houthi, Hamas na Hezbollah kuwaweka front ndio tafsiri baina ya watu wa Lebanon, Syria na hata Yemen.

Ndio maana kuna raia huko Syria walishangilia Israel kuipiga Beirut majuzi..

Hata Ayatollah nimesikiliza katika hotuba yake juzi, ni kama alitoa kauli ya kulalama hadi usikilize kwa umakini akisema "watu wa Lebanon wasisahau kwamba Hezbollah ndio aliindoa Israel kwenye ardhi ya Lebanon......."

Kauli yake ni kama anaona kuna uzito wa uungwaji mkono kwa baadhi ya viongozi wa serikali na raia wa Lebanon tofauti na miaka kadhaa nyuma, hao utakuta ni wachache waliojidhihirisha, utakuta kuna wengi zaidi ambao hawaiungi mkono Iran ila hawataki kujidhihirisha.

Kwa kifupi strategy za Iran zimefika mwisho, labda abadili strategy.

Siamini kama Iran hana resources za kutosha kuiadhibu Israel, lakini Iran kila siku ni kutuma proxies wenyewe wanakunywa juisi na biryani Tehran.

Iran hivi sasa kama ina maanisha waingie ulingoni wao wenyewe kukaangana na Israel, na hiko ndicho ME na dunia nzima wanasubiri kuona.
 
Iran ni vikwazo ndo vinavyomfanya ashindwe kufanya mambo mengi.

Zana nyingi alizonazo Iran ni za Kizamani.

Mfano, ile helikopta aliyokuwa amepanda Rais aliyekufa ilikuwa ni ya mwaka 1979, kama sijakosea.

Ilinunuliwa kipindi cha Shah.

Sasa fikiria 2024 watu bado wanatumia vyombo vya usafiri vya mwaka 47!

Israel ina state of the art weaponry kutoka Marekani na kwingineko.


 
Haya masuala yanatafakarisha sana, utakuta hata humo Iran kuna viongozi ambao hawaamini katika falsafa za kupigana kijeshi na magharibi, wamechoka kuishi maisha ya vikwazo, wanaamini katika kushindana kiuchumi, wakiangalia UAE, Qatar na hata Saudia walipo, India, Japan ,South Korea n.k

Tuangalie Japan alivyo transform kutoka taifa la vita kuwa taifa la maendeleo... Leo gari nyingi sana wanauza kwenda US, electronics n.k.. japo ww2 walikuwa maadui.

Tazama South Korea walioacha kufuata nyayo za North Korea, US wanatumia bidhaa nyingi sana za SK, simu, computers , fridge n.k

Tazama India, wananchi wa US wanatumia dawa nyingi tu kutoka India, India .. Najaribu kuingia kichwani mwa viongozi wa Iran wanao ona Iran isiendelee na mambo ya kivita...

Usije shangaa wanatofautiana mitazamo na kuuzana wao kwa wao...
 
Oh yeah!

Mtu aliye na resources [mwenye hela] ni rahisi sana kumrubuni aliye na njaa!
 
Hezbollah is a religious organization under the guise of a political organisation and it draws most of its members from Shi'ite Islamist sect.
 
Safi sana, hata kiuhalisia unaonekana ni muungwana pia, hapa tupo kishabiki tuu, isitufanye tukagawanyika
 
Baada ya huyo jana jumamosi kashushwa mavumbini kiongozi mwingine mkubwa wa Hezbollah.

Tuliwaambia kitambo MOSSAD wako ndani ya Iran na Lebanon,na Syria huko. Kuna kipofu mmoja pye Chang shen akawa anashusha dislike. Nikamwambia bado kitambo kidogo uta*like* tu.
Hata huyo Iran anyamaze kimya asijaribu huu moto.
Israel sio ya kuichukulia poa kama waraabu wa mpalange wanavyoiwazia kwa kuitazama kwenye site mirror kama nchi ndogo.

Bahati mbaya wengi wanadhani Israel inaitegemea sana USA. Ila vice versa USA ndio wananitegemea Israel kisayansi.
Wa-Israel ndio watu wanaoaminika wenye IQ kubwa kwa dunia ya sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…