Wangekua vizuri wasingepigwa tukio la Oktober 7 mwaka Jana
Mi ninachojiuliza.
Kwanini Hezbollah hawawezi kulenga viongozi wakubwa kijeshi wa Israel? Wanasiasa na viongozi wao?
Israel na CIA wanaua viongozi wa Hezbollah na Iran kila siku, juzi hapa walimuua kiongozi wa Hamas nchini Iran, ikawa sintofahamu walitumia silaha ipi...
Israel wanapiga HQ za Hezbollah, Hivi Hezbollah hawana missiles kupiga nyumba hata ya waziri wa ulinzi Israel?
Hii kusema tuta replace watu kila siku ni ujinga...
Kuna vichwa katika miaka 100 wanatokea mara moja kwenye kizazi.
Huwezi replace kila mtu katika wakati sahihi, ndio maana Israel wanaelewa hilo, kuna watu Mungu huwa anawabariki wanakuwa na upekee tu.
Kama Hezbollah hawawezi weka makachero ndani ya Israel, wafuatilie mienendo ya kila kitu hakuna siku Hezbollah au Hamas itawaweza... Zitabaki hizo story kila siku za kufa shaheed..
Vita ya kurusha tukombora uchwara kambi za IDF wanakufa askari wa 3 na majeruhi 6 halafu nyie mnapigwa kuanzia HQ zenu, viongozi wa wings zote za jeshi, na mamia ya raia wenu wanauawa ni upuuzi.
Wataendelea hivyo hivyo kila siku "tutaleta mwingine". Huku wakizidi kuchinjwa...
Mimi ningekuwa kwenye uongozi, ukiua mkuu wa majeshi na sisi tunapiga sehemu yeyote kwenye watu wenu potential iwe bungeni, polisi, nyumba ya waziri, ikulu n.k ni mbwai mbwai hapo ndipo heshima inakuja.
Nashundwa kuelewa.
1- Israel ina air defense ambazo ni unpenetratable?
2- Hezbollah, Hamas na Iran wanaogopa majibu yatakuwa makali?
3-Au viongozi wa kijeshi Israel na mawaziri wanajificha kwenye mahandaki pia?
Kiukweli hii vita ya kizamani ya kufuata sheria eti kulenga wanajeshi, miundombinu na kulenga miti, Israel imetoka huko zamani.
Wao ni kulenga vichwa tu....