Hela yote hiyo wanaitoa wap
Washakwambia kina Mo Dewji, tajiri aliyenunua mashamba ya mkonge na hayaendelezi! (Ila twajuwa kayafanyia nini), labda watoto wa lamba lamba (Azam), Labda watoto wa....kifupi matajiri tu, au wale ma CEO walioletwa hapa kufanya kwenye makampuni ya Benki na Makinikia!
Ushajuwa sasa, kifupi, ziko hapa kwa ajili ya elites tu, wenye pesa na wanaojiweza kifedha...
Sasa mwenzangu mie ukijitutumua angalia usije ukaumbuka...Maana hakuna guarantee mtoto akitoka pale utampeleka Harvard au Cambridge University..Na hapo kama kamaliza salama, yaani siyo choko, teja, mimba au boza tu lanalojuwa kuongea king'eng'e huku ukiliambia likawape kuku chakula likakwambia kwani huna mfanyakazi wa ndani?!
Ni shule inayowatayarisha watoto wakaishi na kusoma majuu, siyo ya kikwetu ya kufua na sabuni mbuni, kusonga ugali au kupalilia garden..
Ni shule ya wanaojiweza tu, Overpaid CEO's, expatriates and so called businesspeople in TZ, na sio wewe uliopunguziwa mshahara wako toka 40m/= per month to 15m/=, ridhika na ulicho nacho...