Most expensive schools in Tanzania

Most expensive schools in Tanzania

Kweli kabisa, na mifano tunayo mitaani, hakuna ubishi na unayosema, wengi wakitoka hapo ni king'eng'e cha kina Chris Brown, lakini akili za maisha hakuna, hawajuwi kupika, kufanya usafi wa kila aina na hata basic 1st Aid (Sayansi Kimu)...
Tukiongea kwamba tumesikia wakipasuwa mno vyuoni au huko nje waendapo baadaye hakuna! Ndipo tunaposhangaa, kumbe king'eng'e peke yake siyo sababu ya mtoto kupasuwa darasani!
Shule ziko overated, bei overpriced na Target yake haifiki hata asilimia 1 ya watoto TZ...
Tusubiri tuone kama bado wanapata wateja hasa wakibongo na vyuma hivi vilivyokaza..
Expatriates na wafanyakazi wa kigeni ndipo wanapoppeleka watoto wao, itakuwa vyema iwe kwa mishahara wanayolipwa na UN au makampuni ambayo hayakwapuwi hela hapa...
kweli kabisa hivi SEPETU, PFUNKY,KALI ONGALA, TID.LEMUTUZ wamesoma shule gani na fananisha na MILARD AYO, MNYIKA, SHIGONGO nk
 
Ila hzo shule watoto wake wanaosoma wanakuaga ma genius,..achana na u genius wa kukariri huu wa saint kayumba,..hawa madogo mfano wa hyo IST,..wanakuaga wanajua mambo meng sana,hata umchukue mtoto wa primary ukae uongee nae maswala yenye mantik,atakustaajabisha,so ukute sasa ana akili za kuzaliwa ndo utakubal..

mkuu unajua kweli maana ya mtu genius?. Kati ya mtoto anayesoma FEZA mfano na anayesoma Mirare secondary school shule ya kata yenye waalimu 5 bila maabara wote wakipata dv one NECTA. Wa FEZA akiwa na 1.7 halafu wa mirare akawa na 1.9 hapo nani ni genius?. assume no leakage of examination
 
hiyo fees ni gharama ya spaghetti, swimming pool,sausage na wengi wanajifunzia kulamba unga huko,Anamaliza shule hata kufua nguo hajui na ukipata bahati mbaya ukao aliyepitia huko watoto watakuwa wanakula chips kila siku tena za kununua magengeni.kupika na kufua sifuri ila English poa
Mkuu, mtoto aliyesoma IST unataka afikirie kufua?,sijui kupika?.Hayo ni mawazo ya uku uswahilini.
 
hata siku nikiwa na hela kama za baresa bado mtoto wangu atasoma shule za serikali kuanzia darasa la 1 hadi chuo
 
Kina mo dewji na kina manj ndo wamesoma hyo IST,...sasa angalia vichwa vyao,..hiv ushawai msikia dewj au manji wakiongea kuhusu ulimwengu wa biashara,ndo utajua hawa jamaa ni ma genius hata kama walirith mali,ku run bi empires kama zile inabid uwe genius asee,hawa jamaa wanaongeaga point had unajiuliza,hawa jamaa hii elim wametoa wap
ah wapi wana u genius gani vichwa maji tu! ku manage mali za urithiu vizuri sio lazima uwe genius
 
Kwangu seminary za kikatoliki ndo naona shule bora kielimu hata kimaisha kuliko shule hizo za maela MTU aliyetoka seminary ndo naona unakuwa ameiva hasa mfano angalia viongozi wazuri na watu wenye mafanikio nchini kimaisha wengi ni waseminary
 
Back
Top Bottom