MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 305
- 728
Baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 uongozi wa Chadema ulitangaza kususia kupokea ruzuku kutoka Serikalini ikiwemo ruzuku ambayo walistahili kupata kupitia Wabunge 19 wa viti maalum wa chama hicho kwa madai kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki pamoja na kudai kuwa mchakato wa upatikanaji wa wabunge hao wa viti maalum ulikuwa batili.
Cha kushangaza ni kwamba, kupitia taarifa za ndani ya Chadema zinaeleza kuwa katika kikao cha Kamati kuu cha chama hicho kilichoanza kufanyika jana (17/09/2022) ambacho mpaka sasa kinaendelea. Freeman Mbowe na John Mnyika walitoa azimio la kutaka kuanza kudai ruzuku kwa serikali ambayo awali waliisusia, jambo ambalo baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo hawajakubaliana nalo kwa kuwa wanaona kufanya hivyo ni kwenda kinyume na msimamo wa chama hicho kuhusu uchuguzi mkuu wa 2020 pamoja Wabunge 19 wa viti maalum wa chama hicho.
Kinachoendelea kupitia suala hilo ni tamaa ya Freeman Mbowe na John Mnyika juu fedha za ruzuku, jambo ambalo linaleta maswali mengi kwa wajumbe wengine wa kamati hiyo, kuwa fedha hizo zikianza kupokelewa zitatumika kwa ajili ya maendeleo ya chama hicho au zitatumika kwa maslahi binafsi ya viongozi hao? , Je kupitia suala hilo Chadema inakwenda kuwatambua rasmi akina Halima Mdee na wenzake kama wabunge wake halali?
Endapo Chadema itakuja na azimio la kudai ruzuku baada ya kikao hicho itakuwa ni jambo la kushangaza sana kwa sababu hapo awali Freeman Mbowe alitamba kuwa chama hicho kitaweza kujiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka Serikalini. Nukuu: "Tulivyoacha kupokea ruzuku walidhani tusingeweza kujiendesha hata kwa mwezi mmoja, walidhani kwamba Chadema inajiendesha kwa ruzuku pekee ya serikali bila kusahau Chadema inaendeshwa kwa akili, maarifa na upendo"-Freeman Mbowe.
Chadema haiaminiki.