Moto warudi tena Soko Kuu la Kariakoo

Moto warudi tena Soko Kuu la Kariakoo

Nilibahatika kupita hayo maeneo Leo asubuhi palikua Pana Moshi na harufu Kali mno.

Madhara yalikua makubwa.
 
Hapo ndio huwa wahenga wananichanganya Sana methali zao
Kuna tofauti kati ya sumu na dawa. Dawa hufanya kitu husika kirudi kwenye uimara ama ubora zaidi ya pale. Sumu hufanya kitu kife kipotee ama kipunguze ubora wa mwanzo. Moto unaofifia unatakiwa uuletee dawa ambayo nayo nimoto. Ila moto uliozidi unatakiwa uuletee sumu ambayo ni maji

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Siyo huduma za moto peke yake ni kila kitu. Imagine mtu ndiyo umepata heart attack au stroke. Ambulance mpaka ikakufikie ni kazi. Na ikifika si ajabu ikawa mbovu au ikaishiwa mafuta njiani. Na paramedics waliomo humo wanaweza wasije na kifaa hata kimoja. Kwa hizi huduma aisee wenzetu huko duniani wametuzidi sana. Moto kama huo dakika 5 tu wameshafika na mamitambo ya kila aina. Hata huwa sielewi tatizo letu ni nini yaani.
Andengenye alisaini dili bora kabisa kupata ufadhili wa vifaa vya kisasa na mafunzo, akapigwa chini
 
Hapa kuna namna na kuna ushirikina unafanyika sio bure watafutwe wazee Mara moja
Ushirikina upo kila sehem lakini sio sababu ya kuushikilia bango. Hapa kuna namna inayoleta shida...lazima tutafute sababu ya tatiz holo
 
Hapa kuna namna na kuna ushirikina unafanyika sio bure watafutwe wazee Mara moja
Hapana mzee mle ndani hasa juu kule kuna nafaka, sasa kama unayajua marando yale wanayokaangia chips Yakiwaka moto utazima kwa maji juu ila chini moto unaendelea kuwepo ndo same na hiyo.

Magunia ya nafaka ndiyo yanasababisha hiyo hali wala sio hchawi.
 
Hapo timu moja lazima ihamie mkoani.....
Au wazee wa Dabi dabi wanasemaje?
 
Hivi Ina ruhisiwa kuwa na kampuni binafsi ya uzimaji Moto na uokoaji? Wajuzi tafadhali mnijuze.
 
Hiyo lazima maana kuna bidhaa unakuta hazikufikiwa na moto awali ila jivu halikupata maji ya kulizima hivyo linaunda moto taratibu hadi ulivyokolea tena
 
Mbona hiyo timu ipo, Soma Sheria ya wakala wa usimamizi wa maafa, 2014

7.-(1) Kutakuwa na Baraza la Usimamizi wa Maafa Tanzania.
(2) Baraza litaundwa na wajumbe wafuatao-
(a) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana ya
Usimamizi wa maafa ambaye atakuwa
Mwenyekiti;
(b) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye atakuwa Makamu wa Mwenyekiti;
(c) Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
(d) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana ya mamlaka na tawala za mikoa na serikali za mitaa;
(e) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na fedha;
(f) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na afya na ustawi wa jamii;
(g) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na
mawasiliano;
(h) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na
mazingira;
(i) Katibu Mkuu Wizara yenye dhamana na
Kilimo; na
(j) Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Hali ya
Hewa Tanzania.
Kwenye makaratasi kila kitu kipo🤣
Jamaa wanakula tu posho ila magari hayana maji mpaka wayafate Airport
 
Siyo huduma za moto peke yake ni kila kitu. Imagine mtu ndiyo umepata heart attack au stroke. Ambulance mpaka ikakufikie ni kazi. Na ikifika si ajabu ikawa mbovu au ikaishiwa mafuta njiani.

Na paramedics waliomo humo wanaweza wasije na kifaa hata kimoja. Kwa hizi huduma aisee wenzetu huko duniani wametuzidi sana. Moto kama huo dakika 5 tu wameshafika na mamitambo ya kila aina. Hata huwa sielewi tatizo letu ni nini yaani.
Na sio kwamba kibunda hatuna chakununua iyo nitambo ila ni uzembe wa serikali yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom