William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
hebu wanajambo kila mtu point out nini anataka katika katiba ambayo tunaitaka na iliyo ya wananchi sio CCM
Kama straightforward issue kama ya richmond haikupatiwa muafaka sasa mnafikiri issue kubwa kama ya mabadiliko ya katiba ndio itafanyiwa kazi?
2. Ndani ya katiba yetu iliyopo sasa, ibara ya 8 inatamka kuwa mamlaka ya umma yamo mikononi mwa wananchi, lakini ukweli imewekwa kama mapambo tu!:-
Mwananchi hawezi kwenda mahakamni kudai haki ake kama hiyo ibara invyosema. In fact leo sisi wananchi hatuwezi hata kumuondoa mbunge tuliyemchagua wenyewe anapokwenda kinyume na maadili ya uongozi huo kwetu sisi wananchi, lakini mbunge huyo huyo anaweza kufukuzwa na chama chake cha siasa pale tu anapokisaliti chama chake, hata kama ni cha upinzani, lakini sisi wananchi hatuwezi kamwe kumondoa unbunge, hayo ninayaon ani mapungufu makubwa sana kisiasa kwa wananchi walio huru kama sisi wa-Tanzania!
Shukrani kubwa kwa kuweza kuiweka kumbukumbu ya madai ya JF toka tuanze kulizungumzia swala hili la katiba. Haya machache uloyaweka ni mwanzo mzuri sana na ndio pekee unaweza kuipa sifa serikali iliyopo madarakani.Mie na tamani yafuatayo:
-PCCB 'iwe independent' isiwe chini ya raisi
-Tume huru ya uchaguzi
-Rais apunguziwe mamlaka ya kuteua watendaji wa serikali
-Mawaziri wasiwe wabuge
-Vyeo vya mkuu wa mkoa/ wilaya viunganishwe na visiwe na influence za kisiasa
-Sheria kandamizi kama vile za vyombo vya habari, kinga kwa raisi zirekebishwe
-Miiko ya uongozi iingizwe ndani ya katiba.
-Vision ya Taifa iwe wazi na isiyumbishwe na siasa na iwe ndo kipimo cha ufanisi wa serikali na siyo ilani za vyama!
-Maamuzi yote yanayo husu taifa yafanywe kitaalamu na si kisiasa(mfano upangaji wa mishahara, marupu rupu kwa viongozi, n.k)
-Idadi ya baraza la mawaziri iwe wazi kikatiba, siyo kila anaye kuja na lwake!
4. Katiba yetu haina kabisa suala la umiliki wa ardhi:-
Ingawa ardhi ndiyo msingi wa maisha na uti wa mgongo wa uchumi wetu, dosari hiii imekuwa chanzo cha wananchi kunayng'anywa ardhi zao bila huruma au kusikilizwa na authorities. Kwa mfano wananchi kufukuzwa kwenye maeneo yao bila maelezo ya kutosha na serikali, mashamba yao wapewe wawekezaji wa kuchimba migodi, kupitisha bara bara, au shughuli zingine za serikali ambazo sio profitable kwa society at large!
5. Katiba yetu ya sasa haina kabisa suala la uraia.
Wananchi wote tumekuwa kama wakimbizi ndani ya nchi yetu. Hata suala la uzalendo wa dhati linaelekea kufa au kufifia, miongoni mwa wa-Tanzania, ndio maana tumekuwa tukikimbilia nchi za nje na hasa ulaya, kwenda kuishi moja kwa moja maana uzalendo wetu hauwezi kuletwa kwa kuitumia timu yetu ya mpira wa miguu ya taifa, bali kwa katiba kuwa serious na firm kwenye utaifa na wasiokuwa kutoka taifa hili. Passport zetu zimekuwa kama karatasi tu maana kila mtu anaweza kuwa nayo, hata wageni!
6. Haki ya kupiga kura iwe ni msingi wa mamlaka ya umma katika kutoa uongozi kisheria na sio haki ya kibinadamu tu!.
Kupiga kura inatakiwa kuwa ni haki ya kimsingi kisheria na kilelezo cha mamlaka ya umma katika uongozi wa nchi, siyo sehemu ya haki za msingi za binadamu tu, kwa hiyo ni makosa kwa kifungu hiki katika katiba yetu kuwekwa kwenye ibara ya 5, kwenye haki za binadamu kama ilivyo sasa hivi. Maaana hata mwananchi akinyimwa kupiga kura hawezi kwenda mahakamni kudai haki yake kibinadamau badala ya haki yake kisheria, kwa mfano, kuna wakati wa uchaguzi wananchi wamekuwa waikjipanga mistari na baadaye kuambiwa makaratasi yameisha kwa hiyo wanaishia kutopiga kura, (ambazo huwa ni njama za wanaosimamia uchaguzi kumpitisha wanayemtaka), lakini hawawezi kwenda kushitaki mahakamni na kudai haki yao tu ya kibinadamu kupiga kura, wanatakiwa waende mahakamni kudai haki yao kisheria ya kupiga kura.