Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

1. Wananchi Hawakushirikishwa na Uuundaji wa Katiba Ya sasa:-

Ukweli ni kwamba rasimu ya katiba sasa ilipendekezwa na kuasisiwa na kamati kuu au CC, ya CCM, na mchakato wote wa kupata katiba hii ulifanywa kwa muda wa mwezi mmoja tu! Hivyo hakukuwa na muda wa kukusanya maoni ya wananchi at large, na hasa sisi walalahoi, ndio maana katiba hii ya sasa ina uhalali tu wa kisheria, na kukubalika na nyinyi viongozi wetu wachache tu, lakini haikubaliki na sisi wananchi kwa ujumla.
 
hebu wanajambo kila mtu point out nini anataka katika katiba ambayo tunaitaka na iliyo ya wananchi sio CCM
 
hebu wanajambo kila mtu point out nini anataka katika katiba ambayo tunaitaka na iliyo ya wananchi sio CCM

Mie na tamani yafuatayo:
-PCCB 'iwe independent' isiwe chini ya raisi
-Tume huru ya uchaguzi
-Rais apunguziwe mamlaka ya kuteua watendaji wa serikali
-Mawaziri wasiwe wabuge
-Vyeo vya mkuu wa mkoa/ wilaya viunganishwe na visiwe na influence za kisiasa
-Sheria kandamizi kama vile za vyombo vya habari, kinga kwa raisi zirekebishwe
-Miiko ya uongozi iingizwe ndani ya katiba.
-Vision ya Taifa iwe wazi na isiyumbishwe na siasa na iwe ndo kipimo cha ufanisi wa serikali na siyo ilani za vyama!
-Maamuzi yote yanayo husu taifa yafanywe kitaalamu na si kisiasa(mfano upangaji wa mishahara, marupu rupu kwa viongozi, n.k)
-Idadi ya baraza la mawaziri iwe wazi kikatiba, siyo kila anaye kuja na lwake!

na mengineyo .....endeleza
 
..good point Rwabugili at least unaonekana you know what you want sio mpiga kelele tuu....wanajambo tunaendelea maana mafisadi najua wanasoma sana humu na wengine material yao wanapatia humuhumu.
 
2. Ndani ya katiba yetu iliyopo sasa, ibara ya 8 inatamka kuwa mamlaka ya umma yamo mikononi mwa wananchi, lakini ukweli imewekwa kama mapambo tu!:-

Mwananchi hawezi kwenda mahakamni kudai haki ake kama hiyo ibara invyosema. In fact leo sisi wananchi hatuwezi hata kumuondoa mbunge tuliyemchagua wenyewe anapokwenda kinyume na maadili ya uongozi huo kwetu sisi wananchi, lakini mbunge huyo huyo anaweza kufukuzwa na chama chake cha siasa pale tu anapokisaliti chama chake, hata kama ni cha upinzani, lakini sisi wananchi hatuwezi kamwe kumondoa unbunge, hayo ninayaon ani mapungufu makubwa sana kisiasa kwa wananchi walio huru kama sisi wa-Tanzania!
 
Kama straightforward issue kama ya richmond haikupatiwa muafaka sasa mnafikiri issue kubwa kama ya mabadiliko ya katiba ndio itafanyiwa kazi?
 
Kama straightforward issue kama ya richmond haikupatiwa muafaka sasa mnafikiri issue kubwa kama ya mabadiliko ya katiba ndio itafanyiwa kazi?

Wao wameshajiona ni watawala wa Tanzania milele, maamuzi yao siku zote yanaweka mbele maslahi yao na CCM badala ya Tanzania. Inatia moyo kuona kwamba Watanzania wameanza kuamka, na kama shinikizo wanalopata toka kwa baadhi ya viongozi wastaafu kama Warioba kuhusiana na katiba mpya na kelele toka kwa wananchi zitaendelea, basi muda si mrefu ujao watagundua kwamba wananchi wanataka mabadiliko ya kweli ndani ya Tanzania na hawana jinsi bali ni kukubali mabadiliko hayo. Sauti ya wanyonge ikivuma kwa umoja hakuna wa kuizuia.
 
2. Ndani ya katiba yetu iliyopo sasa, ibara ya 8 inatamka kuwa mamlaka ya umma yamo mikononi mwa wananchi, lakini ukweli imewekwa kama mapambo tu!:-

Mwananchi hawezi kwenda mahakamni kudai haki ake kama hiyo ibara invyosema. In fact leo sisi wananchi hatuwezi hata kumuondoa mbunge tuliyemchagua wenyewe anapokwenda kinyume na maadili ya uongozi huo kwetu sisi wananchi, lakini mbunge huyo huyo anaweza kufukuzwa na chama chake cha siasa pale tu anapokisaliti chama chake, hata kama ni cha upinzani, lakini sisi wananchi hatuwezi kamwe kumondoa unbunge, hayo ninayaon ani mapungufu makubwa sana kisiasa kwa wananchi walio huru kama sisi wa-Tanzania!

...power to the people,ndio maana napenda States maana ukileta upuuzi kuna hii kitu inaitwa petition ni nightmare kwa viongozi wa kuchaguliwa...muulizeni Gov.Gray davis(California) yaliyomkuta na kweli huo ni upungufu mkubwa sana katika katiba yetu na ndio maana hawafanyi kazi,inabidi tuwe na uwezo wa kusurubu hawa watu ndio watafanya kile tunachowatuma bungeni
 
Field Marshal Es,
Nitashukuru sana kama kuna mtu ataweza kumpelekea salamu hizi JK popote alipo.
Akitaka ushindi mkubwa ktk awamu yake basi swala la Katiba litampa kura asilimia 90 badala ya 80 alizozipata mwaka 2005.
Bila mabadiliko ya katiba nadhani JK yupo ktk wakati mgumu sana kuweza kuepuka kimbunga kinachomjia....
kwani matatizo yote yanayo zungumziwa na wananchi wengi yanatokana na MAPUNGUFU ktk katiba yetu.
Rwabugiri,
Mie na tamani yafuatayo:
-PCCB 'iwe independent' isiwe chini ya raisi
-Tume huru ya uchaguzi
-Rais apunguziwe mamlaka ya kuteua watendaji wa serikali
-Mawaziri wasiwe wabuge
-Vyeo vya mkuu wa mkoa/ wilaya viunganishwe na visiwe na influence za kisiasa
-Sheria kandamizi kama vile za vyombo vya habari, kinga kwa raisi zirekebishwe
-Miiko ya uongozi iingizwe ndani ya katiba.
-Vision ya Taifa iwe wazi na isiyumbishwe na siasa na iwe ndo kipimo cha ufanisi wa serikali na siyo ilani za vyama!
-Maamuzi yote yanayo husu taifa yafanywe kitaalamu na si kisiasa(mfano upangaji wa mishahara, marupu rupu kwa viongozi, n.k)
-Idadi ya baraza la mawaziri iwe wazi kikatiba, siyo kila anaye kuja na lwake!
Shukrani kubwa kwa kuweza kuiweka kumbukumbu ya madai ya JF toka tuanze kulizungumzia swala hili la katiba. Haya machache uloyaweka ni mwanzo mzuri sana na ndio pekee unaweza kuipa sifa serikali iliyopo madarakani.
 
hivi huyo JK anaona ugumu kukubali katiba mpya ili atuachie nchi safi na yenye haki zaidi maana ataondoka soon na kwenda kijijini kwake na nchi itaendelea kuwepo kwa wajukuu zake,yaani sijui anafikiria nini?
 
na hili la mgawanyo wa mapato yatokanayo na kodi lingeingizwa kwenye katiba kama Marekani,sio kodi inakusanywa nzega then yote inapelekwa Dar wenyewe wakibaki watupu kusubiri Jk afurahi ili awalipe mishahara,mikoa/wilaya na serikali kuu wagawane ili wananchi wawe na uchungu wa kujiletea maendeleo yao
 
Pia tutajenga Taifa la Kidemokrasia kama tutaingiza haya yafuatayo katika katiba mpya:
-Baraza huru la vijana
-katiba iruhusu kutungwa kwa sheria ya kulinda minority bungeni
-Mabalozi wa nyumba kumi wachaguliwe kidemokrasia na si lazima wawe CCM
-suala Rais kumteua jaji mkuu liangaliwe upya
 
3. Katiba ya sasa ina utata sana kuhusu muungano!

Kwa vile katiba yetu ni ya muuungano ifafanuliwe zaidi na kwa uwazi mambo yanayohusu muungano wetu wa nchi mbili. Sioni sababu ya kuwa na katiba ya Zanzibar ndani ya katiba yetu ya jamhuri wa muungano, kwa mfano katika katiba yetu ya muungano hakuna hoja ya msingi ya tulichoungania au tunachoungania? Ingawa ibara ya kwanza inatamka kuwa Jamhuri ya Muungano ni nchi moja, lakini ukiangalia orodha ya mambo muhimu ya muungano huu ardhi siyo suala la muungano, sasa tunakuwaje na chi moja ya muuungano yenye ardhi mbili tofauti?
 
4. Katiba yetu haina kabisa suala la umiliki wa ardhi:-

Ingawa ardhi ndiyo msingi wa maisha na uti wa mgongo wa uchumi wetu, dosari hiii imekuwa chanzo cha wananchi kunayng'anywa ardhi zao bila huruma au kusikilizwa na authorities. Kwa mfano wananchi kufukuzwa kwenye maeneo yao bila maelezo ya kutosha na serikali, mashamba yao wapewe wawekezaji wa kuchimba migodi, kupitisha bara bara, au shughuli zingine za serikali ambazo sio profitable kwa society at large!

5. Katiba yetu ya sasa haina kabisa suala la uraia.

Wananchi wote tumekuwa kama wakimbizi ndani ya nchi yetu. Hata suala la uzalendo wa dhati linaelekea kufa au kufifia, miongoni mwa wa-Tanzania, ndio maana tumekuwa tukikimbilia nchi za nje na hasa ulaya, kwenda kuishi moja kwa moja maana uzalendo wetu hauwezi kuletwa kwa kuitumia timu yetu ya mpira wa miguu ya taifa, bali kwa katiba kuwa serious na firm kwenye utaifa na wasiokuwa kutoka taifa hili. Passport zetu zimekuwa kama karatasi tu maana kila mtu anaweza kuwa nayo, hata wageni!
 
JK hawezi kukubali kwani kufanya hivyo maana yake ni kuwa ifikapo ukomo wake wa kutawala hapo 2010 ,na mauzauza aliyofanya kwenye kipindi chake basi wananchi wataweza kumchukulia hatua za kisheria na hata kumweka kizuizini kama Charles Taylor wa liberia na wengine wengi tuu.

Naunga mkono hoja ya katiba mpya kwa nguvu zangu zote kwani hiki ndicho kikwazo kikubwa kwenye kulifikia taifa lenye heshima na lisilo na umasikini wakati lina rasilimali za kutosha,.
 
6. Haki ya kupiga kura iwe ni msingi wa mamlaka ya umma katika kutoa uongozi kisheria na sio haki ya kibinadamu tu!.

Kupiga kura inatakiwa kuwa ni haki ya kimsingi kisheria na kilelezo cha mamlaka ya umma katika uongozi wa nchi, siyo sehemu ya haki za msingi za binadamu tu, kwa hiyo ni makosa kwa kifungu hiki katika katiba yetu kuwekwa kwenye ibara ya 5, kwenye haki za binadamu kama ilivyo sasa hivi. Maaana hata mwananchi akinyimwa kupiga kura hawezi kwenda mahakamni kudai haki yake kibinadamau badala ya haki yake kisheria, kwa mfano, kuna wakati wa uchaguzi wananchi wamekuwa waikjipanga mistari na baadaye kuambiwa makaratasi yameisha kwa hiyo wanaishia kutopiga kura, (ambazo huwa ni njama za wanaosimamia uchaguzi kumpitisha wanayemtaka), lakini hawawezi kwenda kushitaki mahakamni na kudai haki yao tu ya kibinadamu kupiga kura, wanatakiwa waende mahakamni kudai haki yao kisheria ya kupiga kura.
 
4. Katiba yetu haina kabisa suala la umiliki wa ardhi:-

Ingawa ardhi ndiyo msingi wa maisha na uti wa mgongo wa uchumi wetu, dosari hiii imekuwa chanzo cha wananchi kunayng'anywa ardhi zao bila huruma au kusikilizwa na authorities. Kwa mfano wananchi kufukuzwa kwenye maeneo yao bila maelezo ya kutosha na serikali, mashamba yao wapewe wawekezaji wa kuchimba migodi, kupitisha bara bara, au shughuli zingine za serikali ambazo sio profitable kwa society at large!

5. Katiba yetu ya sasa haina kabisa suala la uraia.

Wananchi wote tumekuwa kama wakimbizi ndani ya nchi yetu. Hata suala la uzalendo wa dhati linaelekea kufa au kufifia, miongoni mwa wa-Tanzania, ndio maana tumekuwa tukikimbilia nchi za nje na hasa ulaya, kwenda kuishi moja kwa moja maana uzalendo wetu hauwezi kuletwa kwa kuitumia timu yetu ya mpira wa miguu ya taifa, bali kwa katiba kuwa serious na firm kwenye utaifa na wasiokuwa kutoka taifa hili. Passport zetu zimekuwa kama karatasi tu maana kila mtu anaweza kuwa nayo, hata wageni!

Wageni ndio wamekuwa wamiliki na sisi ndio manamba. Tena wanatesa sana na kutucheka, Hivi ni nani ambaye angependelea kuishi ugenini kwa muda wote huu kama mambo yangekuwa mazuri pale bongo? Tena wanatufanyia dhihaka hadi kubadilisha mfumo wa malipo na kuwa wa dollars na hakuna wa kuwauliza. KATIBA NI LAZIMA ISAHIHISHWE TENA IWE PRIORITY.
 
6. Haki ya kupiga kura iwe ni msingi wa mamlaka ya umma katika kutoa uongozi kisheria na sio haki ya kibinadamu tu!.

Kupiga kura inatakiwa kuwa ni haki ya kimsingi kisheria na kilelezo cha mamlaka ya umma katika uongozi wa nchi, siyo sehemu ya haki za msingi za binadamu tu, kwa hiyo ni makosa kwa kifungu hiki katika katiba yetu kuwekwa kwenye ibara ya 5, kwenye haki za binadamu kama ilivyo sasa hivi. Maaana hata mwananchi akinyimwa kupiga kura hawezi kwenda mahakamni kudai haki yake kibinadamau badala ya haki yake kisheria, kwa mfano, kuna wakati wa uchaguzi wananchi wamekuwa waikjipanga mistari na baadaye kuambiwa makaratasi yameisha kwa hiyo wanaishia kutopiga kura, (ambazo huwa ni njama za wanaosimamia uchaguzi kumpitisha wanayemtaka), lakini hawawezi kwenda kushitaki mahakamni na kudai haki yao tu ya kibinadamu kupiga kura, wanatakiwa waende mahakamni kudai haki yao kisheria ya kupiga kura.

Vipengele vyote hivi anavyorusha FMES si kwamba ni vyake bali ni madai ya Umoja wa Vyama vya Siasa vya Upinzani. Madai haya yapo katika barua aliyopelekewa Rais Kikwete na pia yametolewa kwa vyombo vya habari kama matangazo.

ES sijui anatupasha habari au huko mbele atakebehi, kwa kweli natazama tu nione. Maana mpaka sasa anapost kama yake vile... hebu tuone mwisho wake
 
Back
Top Bottom