Tunahitaji katiba mpya haraka sana ili Taifa hili la Tanzania liweze kuendelea, katiba hiyo mpya inahitaji kuwa na yafuatayo
1.tunahitaji katiba ambayo itazipatia Bunge, Mahakama na tume ya uchaguzi nguvu zaidi ili vyombo hivi vifanye kazi bila woga
2. watu watakao kuwa kwenye vyombo hivi watachaguliwa na wananchi kama wachaguliwavyo wabunge na maraisi
3. kurudisha madaraka ya mwisho kabisa kwa wananchi na katiba itaje ni wakati gani wananchi wanatakiwa kuulizwa
4. wananchi wawe na uwezo wa kumfukuza kazi mbunge, judge au raisi wakiona hafanyi kazi yake sawa sawa kwa kukasanya idadi fulani ya sahihi
5. sheria kumlinda mtu yeyote anayetofautiana na mbunge, raisi, judge au hata kamanda wa polisi na aweze kukampeni kama anataka kufanya hivyo ili akusanye sahihi za kutosha kumfukuza kazi kiongozi yeyote wa kuchaguliwa
najua kuna mawazo mawazo mazuri zaidi kutoka kwenu, naomba niwakilishe hoja yangu ili muendelee kuichangia
ahsanteni sana