Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

Hawa wabunge wanachekesha kweli

Wenzangu bado imani na bunge letu ipo???.

Hivi kuna kitu wanchi twaweza kufanya kulionyesha bunge kuwa hatulidhiki nalo na wabunge au Spika akatuskia?
 
duh! mbona wamechelewa kuamka? au ndio safari hii ng'ombe kaliwa wao wamepewa sungura tu kama wengine?? kazi kweli kweeeli
 
Mikataba yagonganisha vichwa serikali, Bunge
  • Wabunge kutaka kuijadili kabla ya kusainiwa
  • Mwanasheria Mkuu asema hajapata maombi
  • Spika asema serikali ipeleke muswada bungeni

Ramadhan Semtawa na Tausi Mbowe

KILIO cha wabunge kutaka kushirikishwa katika kuijadili bungeni mikataba yote kabla ya kusainiwa, kinaonekana kugonga ukuta kutokana na Bunge na serikali kutegeana.

Uwezekano wa mikataba hiyo kuonwa na kujadiliwa na wabunge kuiona na kuijadili kabla ya kutiwa saini na serikali unapaswa kuwapo baada ya kuwasilishwa muswada wa hoja hiyo bungeni na kutipishwa, kisha kutiwa saini Rais ili iwe sheria.

Wakati utaratibu ukiwa wazi kwa pande zote mbili, ombi hilo la wabunge kutaka kushirikishwa katika kuona na kuijadili mikataba, Spika wa Bunge Samuel Sitta, amesema serikali ndiyo yenye jukumu la kupeleka muswada huo bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na wabunge.

Akizungumza na waandishi wa gazeti hili mwishoni wiki iliyopita, Sita alisema kazi yakupeleka muswada ni ya serikali kupitia mawaziri wake na kwamba wao ni watekelezaji kwa kujadili baada ya kufikishwa bungeni.

"Hatuwezi kufanya kazi zote sisi, wabunge wanatakiwa kujadili kwa kuukosa, kutoa marekebisho na kuupitisha mswaada huo mpaka unapofikia hatua ya kuwa sheria, hivyo si kazi yetu kuandaa muswada huo na sisi wenyewe kuupitisha, kwani huwezi kuwa mgonjwa na kujitibu mwenyewe, " alisema Sitta.

Hata hivyo, Sitta alisema suala la wabunge kujadili mikataba ya nchi kabla haijatiwa saini ni jambo zuri na endapo litatekelezwa ni wazi kuwa wananchi wataweza kujua kilichopo katika mikataba hiyo badala ya hivi sasa ambapo ni siri.

Alitoa mfano wa nchi ya Thailand ambayo wabunge wake wana uwezo wa kujadili mikataba hiyo na kusema kuwa hali hiyo inaonyesha uwazi na uwajibikaji zaidi katika utawala.

Sitta alisema kuwashirikisha wabunge inaonyesha jinsi serikali inawashirikisha wananchi wake katika maamuzi yao wenyewe kwa kuwa wabunge hao wapo kwa niaba ya wananchi wao.

"Hii inajenga umoja, Bunge ni chombo chetu cha Kitaifa kinasimama badala ya wananchi, kuwashirikisha ni sawa na kushirikisha mwananchi mmoja mmoja katika maamuzi, "alisistiza Sitta.

Kwa mujibu wa Katiba ya nchi (Ibara ya 63 (d), Bunge ndilo lenye jukumu la kutunga sheria, chini ya utaratibu maalumu wa kanuni za chombo hicho (sehemu ya tisa).

Taratibu hizo zinahusu muswada wa sheria katika hatua mbalimbali, kabla ya haujafikishwa bungeni, namna utakavyowasilishwa na kujadiliwa (pamoja na kamati zake), na hatimaye kupitiwa kuwa sheria.

Muswada wa sheria waweza kuwa wa serikali, ambao huwasilishwa na Mwanasheria Mkuu, Waziri au wa Mbunge ambaye si waziri, mwanasheria wa serikali na pia unaweza kuwa wa kamati ambao utawasilishwa na mwenyekiti au mjumbe.

Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Johnson Mwanyika alisema wiki iliyopita alisema kwamba suala hilo halijafika kwao kama ombi.

"Umesikia wapi hilo, sisi hatujalisikia kaulize oOisi ya Bunge wao watakuwa wanajua vizuri zaidi," alisema Mwanyika kwa kifupi.

Hivi karibuni kumueibuka mjadala ambapo wabunge wanasema kuna haja ya kuiona mikataba na kuijadili bungeni kabla serikali haijatia saini.

Miongoni mwa mikataba mibovu ya hivi karibuni ambayo imeibua mjadala ni pamoja wa Kampuni ya kufua kuzalisha umeme ya Richmond Development Corporation (RDC) na mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.

Source: Mwananchi
 
Speaker anasema bunge la Tanzania lina kazi nyingi sana, what kind of non sense? Serikali kaye ni kuandaa na kusign mikataba hii mobovu, then speaker anasema kazi yao wao ni kukosoa, sasa nani kamwambia kwamba mkataba ukishasign na ukiwa ni mbovu hata wao wakikosoa inasaidia nini?

Bunge lina wawakilishi wa wanchi kutoka kila kona, ni haki ya wawikilishi hao wa wananchi kujadili mambo yote yatakayo wapa nguvu waanchi. Time imefika serikali ya Tanzania kurudisha nguvu kwa wananchi kwa kutumia bunge lao tukufu. Serikali inapokuwa na system ambayo haina check and balance ni upuuzi, sababu ndio matokeo yake waziri anafanya upuuzi wa kusign mikataba ya kijinga kisha hakuna wa kumuhoji.

Bunge lina kazi nyingi za kujadili pesa za Taifa stars au? Maana huu ni upuuzi wa hali ya juu.
 
Posted Date::12/17/2007
Mikataba yagonganisha vichwa serikali, Bunge

* Wabunge kutaka kuijadili kabla ya kusainiwa

* Mwanasheria Mkuu asema hajapata maombi

* Spika asema serikali ipeleke muswada bungeni

Ramadhan Semtawa na Tausi Mbowe
Mwananchi

KILIO cha wabunge kutaka kushirikishwa katika kuijadili bungeni mikataba yote kabla ya kusainiwa, kinaonekana kugonga ukuta kutokana na Bunge na serikali kutegeana.

Uwezekano wa mikataba hiyo kuonwa na kujadiliwa na wabunge kuiona na kuijadili kabla ya kutiwa saini na serikali unapaswa kuwapo baada ya kuwasilishwa muswada wa hoja hiyo bungeni na kutipishwa, kisha kutiwa saini Rais ili iwe sheria.

Wakati utaratibu ukiwa wazi kwa pande zote mbili, ombi hilo la wabunge kutaka kushirikishwa katika kuona na kuijadili mikataba, Spika wa Bunge Samuel Sitta, amesema serikali ndiyo yenye jukumu la kupeleka muswada huo bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na wabunge.

Akizungumza na waandishi wa gazeti hili mwishoni wiki iliyopita, Sita alisema kazi yakupeleka muswada ni ya serikali kupitia mawaziri wake na kwamba wao ni watekelezaji kwa kujadili baada ya kufikishwa bungeni.

"Hatuwezi kufanya kazi zote sisi, wabunge wanatakiwa kujadili kwa kuukosa, kutoa marekebisho na kuupitisha mswaada huo mpaka unapofikia hatua ya kuwa sheria, hivyo si kazi yetu kuandaa muswada huo na sisi wenyewe kuupitisha, kwani huwezi kuwa mgonjwa na kujitibu mwenyewe, " alisema Sitta.

Hata hivyo, Sitta alisema suala la wabunge kujadili mikataba ya nchi kabla haijatiwa saini ni jambo zuri na endapo litatekelezwa ni wazi kuwa wananchi wataweza kujua kilichopo katika mikataba hiyo badala ya hivi sasa ambapo ni siri.

Alitoa mfano wa nchi ya Thailand ambayo wabunge wake wana uwezo wa kujadili mikataba hiyo na kusema kuwa hali hiyo inaonyesha uwazi na uwajibikaji zaidi katika utawala.

Sitta alisema kuwashirikisha wabunge inaonyesha jinsi serikali inawashirikisha wananchi wake katika maamuzi yao wenyewe kwa kuwa wabunge hao wapo kwa niaba ya wananchi wao.

"Hii inajenga umoja, Bunge ni chombo chetu cha Kitaifa kinasimama badala ya wananchi, kuwashirikisha ni sawa na kushirikisha mwananchi mmoja mmoja katika maamuzi, "alisistiza Sitta.

Kwa mujibu wa Katiba ya nchi (Ibara ya 63 (d), Bunge ndilo lenye jukumu la kutunga sheria, chini ya utaratibu maalumu wa kanuni za chombo hicho (sehemu ya tisa).

Taratibu hizo zinahusu muswada wa sheria katika hatua mbalimbali, kabla ya haujafikishwa bungeni, namna utakavyowasilishwa na kujadiliwa (pamoja na kamati zake), na hatimaye kupitiwa kuwa sheria.

Muswada wa sheria waweza kuwa wa serikali, ambao huwasilishwa na Mwanasheria Mkuu, Waziri au wa Mbunge ambaye si waziri, mwanasheria wa serikali na pia unaweza kuwa wa kamati ambao utawasilishwa na mwenyekiti au mjumbe.

Hata hivyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Johnson Mwanyika alisema wiki iliyopita alisema kwamba suala hilo halijafika kwao kama ombi.

"Umesikia wapi hilo, sisi hatujalisikia kaulize oOisi ya Bunge wao watakuwa wanajua vizuri zaidi," alisema Mwanyika kwa kifupi.

Hivi karibuni kumueibuka mjadala ambapo wabunge wanasema kuna haja ya kuiona mikataba na kuijadili bungeni kabla serikali haijatia saini.

Miongoni mwa mikataba mibovu ya hivi karibuni ambayo imeibua mjadala ni pamoja wa Kampuni ya kufua kuzalisha umeme ya Richmond Development Corporation (RDC) na mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.
 
Bunge halihitaji KUIOMBA serikali ifanye kitu. Kama sehemu kubwa ya wabunge inataka serikali isisaini mikataba mikubwa ambayo haijajadiliwa, basi atoke mbunge mmoja awasilishe mswada binafsi utakaolazimisha utekelezaji wa hilo.

Kuna wakati nadhani wabunge wetu wanasahau nguvu waliyonayo. Tumeshajadili hapa, siku za nyuma, na kuona kwamba katiba ya nchi yetu inasema waziwazi kwamba Bunge litasimamia shughuli za serikali. Tuliweka hapa JF dondoo za vipengele husika.

Kama hata Sitta anataka miswada mikubwa ya kiuchumi ijadiliwe na Bunge kabla ya kusainiwa na serikali, hao walarushwa wanaotaka kusaini kwa siri mahotelini (in between drinks) wataweza kumzuia?
 
Moshi,

Tatizo wabunge makini wanaoelewa structural checks and balances ni wachache.Na hao makini wengi wao wanakuwa politically biased.Serikali,Bunge na Mahakama hakuna anayempita mwenzake.

Wabunge "wasitake" au "wasiombe", wapitishe miswada bungeni na kuifanya kuwa sheria kama kweli wana nia.Otherwise itakuwa sawa na mchezo wa kutaka kuonekana umetoa shilingi ili jimboni kwako wakusikie halafu ukikaripiwa na waziri unarudisha.
 
yote hiyo ya kuwa na wabunge vilaza wasiojua kitu ni rushwa na unazi wakati wa uchaguzi,naaamini bila kuiangusha CCM TZ itabaki maskini milele,hawa watu vitu wanavyofanya utafikiri ile nchi ni mali yao na wao ni masultani wateule
 
naendelea kusisitiza huyu Sitta ni Kilaza..................labda kama waandishi wamem-quote vibaya.....eti kazi ya wabunge ni kukosa tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!..................hivi lile naneo kutunga sheria liliondoka ktk vocabulary ya Sitta!!!!!!!!!.........................hawa ndio viongozi ninawaita sio serious......bado wanatuona wananchi kuwa hatujui wanalosema.

Inabidi kuwapa semina hawa wabunge ya kuwaeleza nini majukumu yao......inaelekea wengi wao Sitaa akishasema kitu wao ni Yes Sir................shame on you wabunge wote.

Hii statement ya Sitta inabidi ipingwe vikali........
 
Serikali yadai katiba ya Tanzania haina kasoro
Na James Magai

WAKATI Muungano wa vyama vya upinzani nchini umetangaza kuwa mwaka 2008 ni wa mapambano ya kukamilisha agenda yao ya kudai Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, serikali imesisitiza kuwa katiba ya sasa haina kasoro na kwamba inakidhi mahitaji yote ya msingi.

Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Mary Nagu alimweleza mwandishi wa gazeti hili kuwa Katiba ya sasa ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliotungwa mwaka 1977, bado inakidhi mahitaji kwa kuwa ilitungwa kwa umakini mkubwa kwa kuwashirikisha watanzania wengi

"Katiba hii bado inakidhi mahitaji na inahimili mabadiliko yote ya kijamii yanayotokea nchini kwa kuwa ina mambo yote yanayotakiwa kuwemo katika katiba ya kidemokrasia," alisema Dk Nagu.

Akizungumzia hoja ya wapinzani kuhusu kutungwa kwa katiba mpya, Dk Nagu alisema huu sio wakati wake wala kwa sasa hakuna sababu za kutunga katiba mpya kwa sababu iliyopo inakwenda na wakati.

Alieleza sababu za kutungwa kwa katiba mpya kuwa ni kutokana na matukio makubwa ikiwamo kubadilisha mamlaka ya dola.

"Kwa mfano tulipotoka serikali ya kikoloni na kwenda serikali ya uhuru tulitunga katiba mpya. Pia tulipoachana na Malkia wa Uingereza tulitunga katiba mpya na baada ya kuwa na Muungano tukawa na katiba mpya tuliyonayo sasa," alibainisha Dk Nagu.

Hata hivyo alisema serikali haijui hoja ya msingi katika madai ya wapinzani kuhusu katiba, kwamba wanataka itungwe katiba mpya au iliyopo ifanyiwe marekebisho.

Alisema wapinzania hawajawahi wasilisha mapendekezo yao serikalini kuhusiana na madai yao zaidi ya kusikia madai hayo kupitia vyombo vya habari.

"Suala la kutunga katiba mpya wakati huu hatuna na sio agenda yetu. Agenda yetu kuu na iliyoko kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ni kuondoa umaskini na kuleta maendeleo kwa wananchi, kujenga shule, zahanati na vituo vingi vya afya na kuleta mabadiliko ya kilimo ili kuboresha maisha ya Watanzania," alisema Dk Nagu.

Alisema kama hoja ya wapinzani ni kutunga katiba mpya kwa maana ya kuifuta katiba yote inayotumika sasa, hiyo ni vigumu kwa sasa kwa sababu, licha ya kutokuwa agenda ya serikali pia sio wakati muafaka.

Dk Nagu alisema kama hoja ya wapinzani ni kufanya mabadiliko katika baadhi ya mambo ambayo wanadhani yanahitaji mabadiliko ndani ya katiba basi wanapaswa kuyawasilisha serikali kwa utaratibu ulioainishwa na katiba.

Alisema katiba si Msahafu wala si Biblia bali ni waraka hai unaoruhusu mabadiliko, lakini akaonya kuwa ni sheria kuu ambayo ikitikiswatikiswa inaweza kusababisha nchi kuondokana na amani ambayo alisema yeye anaamini imedumishwa na katiba ya sasa.

Akizungumzia utaratibu wa kufanya mabadiliko katika katiba alisema ni lazima kwanza kukusanya maoni kutoka kwa wananchi, kuona kama wanakubaliana na jambo husika na kisha kupeleka muswada bungeni, ambalo litaipitisha kwa niaba ya wananchi.

Alisema hadi sasa katiba imekwishafanyiwa mabadiliko mbalimbali na kwa nyakati tofauti tofauti, ikiwa ni pamoja na kuweka misingi ya haki za binadamu mwaka 1984 na wakati wa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

"Sasa kama kuna mengine, tufuate utaraibu tulioufuata wakati ule ambao uko katika katiba, kwa sababu katiba sheria mama ambayo inaruhusu mabadiliko kwa mambo yale yanayohitaji mabadiliko kulingana na muda wenyewe," alisema na kuongeza:

"Lakini katiba itabakia ile ya mwaka 1977 hivyo tutenganishe kati ya kutunga katiba upya na kufanya mabadiliko ndani ya katiba iliyopo sasa hivi. Kwa ujumla wapinzani haieleweki kama wanataka katiba mpya au wanataka mabadiliko".

Alifafanua pia kuwa sio kila mabadiliko yanayotokea duniani na nchini ni lazima kufanya mabadiliko katika katiba bali mengine huweza kufanywa kupitia katika sheria mbalimbali ambazo pia zinatungwa kwa kuangalia katiba.

Alitoa mfano wa mabadiliko yaliyowahi kufanyika katika sheria kuwa ni pamoja na kuundwa kwa mamlaka na vyombo mbalimbali vya udhibiti ikiwamo Ewura na Sumatra.

"Kwa hivyo kama nilivyokwisha kusema wao walete tu mapendekezo yao na sisi tutayaangalia, jambo ambalo linahitaji mabadiliko tutawaeleza utaratibu na namna ya kufanya kuleta mabadiliko hayo kama hayako kwenye katiba na kama hayawezi kufanyika kupitia katika sheria," alisisitiza Dk.Nagu.

Hivi karibuni vyama vya upinzani nchini vilifanya mkutano na vyombo vya habari na kutoa tamko kuwa mwaka 2008 ni mwaka wa mapambano ya kukamilisha agenda ya kutungwa kwa katiba mpya na kwamba tayari wamekwisha kamilisha rasimu ya katiba mpya ambayo wataanza kuipeleka kwa wananchi ili kupata maoni kabla ya kluishinikiza serikali kuipitisha.

Kwa muda mrefu wapinzani wamekuwa wakidai kuwa katiba ya Tanzania ina mapungufu hivyo inatakiwa kuandikwa upya lakini serikali imkuwa kikipinga hadi bungeni.

Hata hivyo, kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, wapinzani walishindwa kujenga hoja ya pamoja juu ya madai yao hayo kutokana na kutokuwa na umoja, kufautia umoja waliouunda kuvunjika wakati wanaelekea kwenye mchakato wa uchaguzi huo.

Safari hii vyama hivyo vimeunda umoja ambao pia baadhi ya vyama vimejitoa na kuunda wa kwao hivyo kuifanya kambi hiyo kuwa na makundi mawili.
 
Kazi ipo hapo,ila inabidi tuu maana katiba ya sasa ni kichekesho na bado inasimamia chama tawala na kuilinda serikali iliyomo madarakani badala ya kulinda haki za kila mtanzania na utawala bora/demokrasi...hawa CCM wamejisahau sana au inawezekana hawana idea na wanachoongea ila moto wao wataupata siku wakishindwa uchaguzi na kuwa upande mwingine,na kibaya zaidi wakianza kupigwa ndani kwa amri za wakubwa bila mashtaka kwa jina la usalama wa taifa ndio watajua
 
Mwishowe yatatukuta ya Kenya. Mungu apitishie mbali balaa hilo.

Kwa nini serikali isikubali kuangalia vipengele vinavyodaiwa na upinzani halafu wavijadili na kuvipatia ufumbuzi?
 
..hawa CCM wamejisahau sana au inawezekana hawana idea na wanachoongea ila moto wao wataupata siku wakishindwa uchaguzi na kuwa upande mwingine,na kibaya zaidi wakianza kupigwa ndani kwa amri za wakubwa bila mashtaka kwa jina la usalama wa taifa ndio watajua

Ngugu yangu Koba, umenikuna haswaa kwa vile ukweli do huo hapo ulivyousema!

Namwomba Mungu aniweke hai niione siku hiyo kwa macho yangu mwenyewe, niwaangalie machoni na kuwauliza .. Ndugu zangu vipi tena, kulikoni?? Hayawi hayawi sasa imekuwaje???
 
Kazi ipo hapo,ila inabidi tuu maana katiba ya sasa ni kichekesho na bado inasimamia chama tawala na kuilinda serikali iliyomo madarakani badala ya kulinda haki za kila mtanzania na utawala bora/demokrasi...hawa CCM wamejisahau sana au inawezekana hawana idea na wanachoongea ila moto wao wataupata siku wakishindwa uchaguzi na kuwa upande mwingine,na kibaya zaidi wakianza kupigwa ndani kwa amri za wakubwa bila mashtaka kwa jina la usalama wa taifa ndio watajua

KOBA unachosema ni kweli kabisa. Kwanza ukiangalia utaona katiba yetu ni ileile ya mkoloni. Kule Lancaster walichofanya ni kuondoa neno gavana na kuweka waziri mkuu na baadaye wakaendelea kubadilisha vipengele vidogo vidogo ili viendane na matakwa ya Nyerere, Msekwa na CCM.

Lakini blunder iliyopo ni kuwa wanasiasa wa bongo ndio wanapower ya kushughulika na ubadilisha wa katiba, na wako free nayo sana. Hata watu wa upinzani usiwaamini hata kidogo. Sasa hivi ikitokea by chance upinzani wakaingia madarakani, wanaweza kuitumia katiba hiyo hiyo kuidhibiti CCM mpaka ikapotea.

Unaweza kuona Kibaki alipokuwa opposition aliunga mkono mabadiliko ya katiba, na kubadilisha tume ya uchaguzi, lakini alipoingia madarakani akaona kufanya hivyo ni kama suicide. Hali ya Kenya inaweza kufika Tanzania. Lakini sio leo, hapa nyumbani watu bado wamelala sana!!
 
Ukimwuliza Dr Nagu kuhusu Ukweli kwamba Phd yake ni Fake atakwambaia haoni ubatili wowote wa PhD yake kwa sababu hata rais anamtambua kwamba yeyey ni DR.

Katiba haiwezi kubadirishwa kirahisi itabadirishwa kwa mbinde, mageuzi yote duniani yanaletwa kwa harambee ya nguvu iliyo kinyume cha walioko madarakani.

Mtu abishaye hili asubiri kitakachotokea Kenya ndani ya miaka 2 tu.

Nagu kashika mpini anadhani kisu chote ni mpini ndo maana haoni makali ya kisu tulalamikayo yako wapi?

Hatusubiri mpini umponyoke tutaunyakua kinyume na matarajio yake hapo ndo utamsikia akitoa mayowe ya kikwao.

Katiba yetu ina vifungu vingi vya kulinda Ufisadi na Mafisadi wenyewe ni lazima ibadirishwe tu.
 
Of course, katiba haina kasoro...inaruhusu ulaji, uozo, ufisadi wa CCM uendelee kwa faida ya viongozi wachache wa CCM. Sasa kwa nini tuibadilishe?
 
Viongozi wetu bado wanaishi miaka ile ya sitini ambapo Julius na other viongozi walikuwa wanajua madaktari wote nchini, mainjinia, wanasheria na watu wenye Phd's. Na hiyo ilitosha kuwafanya waamini kwamba ni wao tu wenye akili na hao wanaowajua.

Sasa hili la katiba huyu mama anasema kwamba haoni kwamba ni ishu simply kwa sababu halijatoka kwa watu ambao anaamini they are brave! Huyu anaweza kuwa anaamini kwamba katiba ni mali ya viongozi wa serikali, na ni hao tu inayoweza kuamua kuifanyia mabadiliko!
 
Mheshimiwa ana haki ya kusema aliyoyasema maana ndio msimamo wa serikali yake. Kama alivyoshauri, wale wanaoona katiba ina matatizo waainishe hayo matatizo. Basi tufanye alivyotushauri. Mwenye hiyo katiba aitundike hapa halafu ijadiliwe kifungu kwa kifungu. Vyama vya upinzani wanachoweza kufanya ni kufungua mjadala kwa wananchi kama walivyofanya ishu ya madini.

Wachukue katiba hadharani na waueleze umma matatizo yake waonavyo wao yako wapi. Hapo mjadala wa haki na uwazi utaanza maana chama tawala na watu wengine ambao wanaona hakuna matatizo itabidi wajibu hizo hoja. Naamini kuwa wananchi (wakiwemo wana JF) ndiyo watakaoamua kama kweli kuna haja ya kuwa na katiba mpya au tuendelee kuifanyia marekebisho. Tuwape nafasi ya kutafakari hili suala muhimu.
 
Back
Top Bottom