Sasa nadhani umefika wakati muafaka kwa wananchi kuungana pamoja kuhakikisha kwamba Viongozi wetu na hasa hao wa CCM kuelewa kwamba wao ni waajiriwa!...
Kama kweli serikali ya CCM imefikia kukataa kwa kauli moja kuhusu KATIBA basi hakuna haja ya kuendelea na mijadala inayohusu mustakabali wa nchi yetu.
Vyama vya Upinzani kwa pomoja viungane na viandike barua nzito kwa vyombo vya kimataifa ambavyo mapema iwezekanavyo na watoe msimamao wao kuhusu Uchaguzi unaofuata. Bungeni kusiweko na amani tena bila serikali kubadilisha kauli hiyo na wala msidanganywe na uchache wenu bungeni ila mnaweza kukataa vikao vya Bunge kwa pamoja hadi kieleweke. Dunia nzima itawasikia hata kama mtakuwa watu wawili!...
Na wasikomee hapo ila waingie Mikoani hadi ktk vyuo vyetu vikuu kutoa hotuba zinazohusiana na mapungufu ya Katiba ya nchi. UMoja wao utasikilizwa na wananchi ambao wengi wao hawafahamu ni kitu gani hasa wapinzani wanakitaka. Wakumbuke tu kwamba kuhitaji katiba mpya hakueleweki kwa Watanzania walio wengi hasa wa vijijini ambao kwao maisha ni yao yanategemea rehma za Mungu.
Pasiwepo na lugha nyingine zaidi ya Katiba!..