Movie ya EONII hakuna kitu

Movie ya EONII hakuna kitu

Watu tulisema hapa tukashambuliwa sana na Andrew Tate mpaka tukajiuliza tumemkosea nini huyu jamaa[emoji38][emoji38]
Mimi nilishaanza kuona ushuzi kwenye trailer,nilijua tu muvi itakuwa hovyo. Hizo milioni 473 wangeenda tu kusaidia masikini [emoji23][emoji23][emoji23]

Hapa ndio swali langu lipo, wamerudisha pesa yao au imekuwaje...nataka kujua ROI

Mauzo hayawekwi Public au? Kwa anaefahamu tafadhali?
 
JF kuna wajuaji kazi kukosoa tengenezeni yenu tuone mfano
Ukitengeneza kitu kibovu kwa ajili yetu, sisi tunakiruka. Hatuna muda wa kutengeneza vya kwetu ili muone mfano bali tunakimbilia vile vilivyotengenezwa vizuri. Sio kila mtu ni director wa filamu

Kama wataendelea kutoa movie za ovyo hivi basi hatutapoteza muda kuziangalia. Tutaendelea kufuatilia za USA, Korea na nchi nyingine zilizo serious
 
Huko unako tolea mfano walianza bila makosa? yaani movie ya kwanza tena kutoka Africa unataka ilingane na watu walio kwenye industry kwa miaka zaidi ya 100?
 
Huko unako tolea mfano walianza bila makosa? yaani movie ya kwanza tena kutoka Africa unataka ilingane na watu walio kwenye industry kwa miaka zaidi ya 100?
Kwani hao watu wa huko mbele walipofanya makosa hawakukosolewa?
Watengenezaji wa Bongo movie ni nani haswa mpaka kazi zao zisikosolewe?Kukosoa kitu kibovu leo hii imekuwa kosa?
Kwa hiyo unataka tusifie vitu vibovu? Eti kisa wameanza juzijuzi?
Aliyesema nataka walingane na hao waliopo kwenye industry miaka 100 ni nani?Mbona hata wao kazi zao nyingi tu zinakosolewa? Kwa nini za Bongo zisikosolewe?
Au kisa ni muvi ya nyumbani ndio tusiikosoe? Kisa wametumia hela nyingi kuliko Bongo movie nyingine basi ndio tukae kimya hata wakitoa kitu kibovu?
Kitu usipokipenda usiseme? Kukosoa muvi mbovu ndio mnaita roho mbaya? Sasa mtu akiona kitu cha hovyo mnataka akae kimya au? Mnataka asitoe mawazo yake?

Hapa tunaongelea movie, hata haihusiani na uzalendo wala roho mbaya, bali ni maoni ya watu juu ya movie hiyo. Kama wewe ni mpenzi wa movie basi kuna movie mbovu kibao utakuwa umeziona na kwenye thread ya movie kule muvi ikiwa mbovu inapondwa bila kujali ni ya nchi gani. Ila huku kuponda movie mbaya ya Kibongo ndio mnaita roho mbaya na kukosa uzalendo.

Kama mashabiki wa Bongo movie wenyewe wataendelea ku-judge movie kwa kuzingatia hisia kuliko uhalisia basi Bongo movie haitaendelea kamwe. Endeleeni kusifia ushuzi
 
Back
Top Bottom