Mowzey Radio tunamlilia, lakini je tunayafahamu haya?

Mowzey Radio tunamlilia, lakini je tunayafahamu haya?

Hizi sifa za marehemu[emoji23] , kabla ya kifo chake sijawahi ona thread inayomuhusu hata1 hapa JF
Kwa hiyo unataka kusemaje ? Mimi im big of the radio , kama unabisha tafuta kazi zake , ww unafikiri watu kama museveni au wizkid wakiandika msg za nzito za maombolezo ni wajinga ? Masupa star wakali wengi tu humu hawana nyuzi , bonjov, scorpion, hakeem olajuwan , stephen nzonzi , chris euban, sade, lennox lewis , chicago, dick & chicks, inni kanuze, vanilla ice, lady namu mariam etc
 
Hata mimi nilijua tu yalikua makosa ya marehemu.

Kuna watu wakishakua maarufu basi hudhani kila mtu anaweza kunyenyekea umaarufu wao na kufanya fujo zisizo na msingi.

Umwamba mwingine hua ni upumbavu. Ukipenda fujo ujue ipo siku mambo yatakuendea vibaya.

Sasa bouncer akampiga chini kama vile mtu anaangusha kiroba cha simenti, tena kwa ile style ya kina Taker na Kane, Rest In Peace.(upside down).

Fujo siku zote hazijawahi kua na faida.
Alipigwa msumari km afanyavyo undertaker kule wwe?
 
Babu yangu(RIP) aliwahi kuniambia kuwa hakuna marehemu mbaya. Yaani mtu akishafariki ni ngumu na ni mara chache mno kuzungumziwa mabaya yake. Kinachotawala huwa ni mema ya marehemu tu!

Mowzey Radio jina halisi ni Moses Ssekibogo kaicha dunia akiwa bado kijana kabisa miaka 33. Alikuwa na kipaji cha sanaa na kupendwa pia. Inawezekana kabisa kama ni mashindano ya kupendwa Kampala angeweza kuchukua number moja. Alipendwa sana yeye na nyimbo zake pia kupendwa huku hasa na mabinti na wanawake ilimpelekea kuwachakaza hasa.

Alikuwa anaelekea kwenye kilele cha mafanikio kupendwa, utajiri na umaarufu kifo kilipomkuta kwenye ugomvi uliotokea kilabuni kwa kupokea kipondo kilichosababisha alazwe hospital siku kadhaa.

Mowzey Radio msanii huyu maarufu akifanya kazi zake na Weasel licha ya kipaji mafanikio na kupendwa kwake alikuwa ni kijana mkorofi sana na mwenye jazba sana. Hali hii ilimpelekea kugombana na kuwa na mitafaruku ya mara kwa mara na watu wake wa karibu, wasanii wenzake na wana jamii.

Magomvi yake ni mengi lakini kwa uchache yanayokumbukwa zaidi ni kati yake na
1. Khalifa Aganaga. Huyu waliwahi kufanya kazi pamoja Goodlyf

2. Bebe cool msanii mwenzake

3. Jeff Kiwa manager

4. Traffic police. Huyu mama akitaka kumkamata kwa makosa ya kuendesha gari kwa fujo na ulevi

5. Huu wa mwisho ulioondoka na roho yake inasemekana alimuita bouncer wa bar husika BOOZER ambayo maana yake kwa kiswahili ni mlevi mbwa.

Mowzey alikuwa anapenda kujiona star na kutaka kupewa VIP treatment kila alipokuwa hali iliyomfanya agombane na watu kila mara. Kwenye msiba wa Ivan alichukua laptop ya DJ na kuitumbukiza kwenye maji kwa kisa kidogo tu.

Waganda wanamlilia sana. Museveni Kaguta alichangia dola 8300 kwenye Matibabu yake lakini hakuweza Kupona. Kaondoka ni msiba mkubwa kwenye tasnia ya usanii Afrika mashariki lakini huo ndio ulikuwa upande wake wa pili.

RIP Mowzey Radio

Na hivi ndivyo maisha yake yalivyokatika...kikatili sana.
 

Attachments

  • VID-20180203-WA0033.mp4
    VID-20180203-WA0033.mp4
    2.6 MB · Views: 36
  • IMG-20180203-WA0027.jpg
    IMG-20180203-WA0027.jpg
    62.8 KB · Views: 50
Masupa staaa wetu wapenda mkono akina Ze Dudu, TID, Chid, Nyoso nk nk jifunzen kitu hapo.
 
Masupa staaa wetu wapenda mkono akina Ze Dudu, TID, Chid, Nyoso nk nk jifunzen kitu hapo.
 
Masupa staaa wetu wapenda mkono akina Ze Dudu, TID, Chid, Nyoso nk nk jifunzen kitu hapo.
 
Masupa staaa wetu wapenda mkono akina Ze Dudu, TID, Chid, Nyoso nk nk jifunzen kitu hapo.
 
Style ya maisha yako ndo style ya kifo chako .R.I.P Mozey Radio,kila mtu ana mapungufu yake hapa duniani
 
Back
Top Bottom