Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 5,203
- 3,913
Yote uliyoandika hapo juu ni mipango ya muumba na hakuna anayeijua hata dakika moja mbele iwapo atakuwa hai au moyo utakuwa umesimama.Soma mauaji mengine ya Magufuli hapa chini.
UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA BIHARAMULO
👉Mnamo Mwaka 1985 Mwalimu wa Kemia shule ya sekondari Sengerema John Pombe Magufuli aligombea ubunge wa jimbo la Biharamulo akichuana na Mkulima Phares Kabuye. Kabuye alishinda na kutangazwa Mbunge, na Mwalimu Magufuli akarudi Sengerema kufundisha.
👉Mwaka 1990 Mwalimu Magufuli alichuana tena na Mkulima Kabuye kwa mara ya pili. Kabuye alimshinda tena Magufuli na kutetea kiti chake.
👉Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, jimbo la Biharamulo liligawanywa na kupatikana majimbo mawili (Biharamulo Magharibi na Mashariki). Kabuye aligombea Magharibi akashinda. Magufuli nae akagombea Mashariki na kushinda kwa mara ya kwanza baada ya mpinzani wake wa muda mrefu kwenda magharibi.
Baadae jimbo la Biharamulo Mashariki lilibadilishwa na kuitwa Chato..
Miaka kadhaa baadaye Phares Kabuye alifariki kwa ajali Morogoro.
RIP Phares kabuye
"Bila kuigawa Biharamulo mara mbili nazani sasa hivi John pombe magufuli angekuwa mwalimu mstaafu"
Anayemtetea Magufuli ni mshenzi tu.
Ni historia ya maisha binafsi na siku zote zinakuwa na milima na mabonde, huyo JPM hayupo tena juu ya uso wa ardhi kwa miaka minne, bado mpaka leo anaongelewa kwa chuki nzito namna hii?.
Alikuwa ni shujaa mwenye maamuzi magumu na ameondoka kafanya mengi yenye kuonekana na yataendelea kumtetea kwa miaka na miaka ijayo.