Mpaka leo Watanzania hawajajua kosa la Nchimbi ni lipi?

Mpaka leo Watanzania hawajajua kosa la Nchimbi ni lipi?

Kama unajua tupeni maelezo
Kosa lisilo kosa ndiyo kosa lenyewe kwenye utawala huu uliojaa wanafiki na machawa watupu.

Kuwa na mawazo huru na kutoa maoni kama inavyosema Katiba kwa sasa ni jinai inayomtesa yeye na wengineo kina Lisu.

Usipoabudu na kuyasujudu mamlaka, utakwenda na maji bila kujali una cheo gani.

Ukiuliza kosa, hajafanya kosa lolote, angelifanya makosa angelifikishwa mahakamani.
 
Wananchi wanaomwona Nchimbi hana kosa wako sahihi kabisa.Kwa sababu maneno aliyowahi kutamka hayakuhusu Wana ccm pekee bali watanzania wote.Hakusrma Wana ccm pambanieni katiba mpya.Unless Kuna kosa tusilolijua.Habari ya kinyangnyiro Cha urais hayawahusu kwa sababu wananchi ndiyo wanaoamua yupi awe rais wao endapo tume na katiba vitabadilishwa
 
Kuungana na freemason tangu mwanzo wa safari! Walipofika mbele ya hiyo safari yao si akataka kumsaliti! Hili lilikuwa ni kosa kubwa sana. Ndugu wa freemason aliyetaka kumsaliti walianza kumuita Yuda! Baada ya kushindwa kumvumilia wakaamua kupita naye.
 
Kama unajua tupeni maelezo
Mkuu Kamu, Kamundu , hili ni swali very valid, hata mimi niliwahi kuuliza humu, Kuwa Mkweli Kunaponza!, Nilidhani Unawa Cost Malofa na Makapuku Tuu, Kumbe Hata Vigogo Wakubwa kama Huyu!. Kosa Lake Nini?, Au ni Kuwa Mkweli Sana?!

Hivyo inawezekana Nchimbi kafanya kosa kubwa sana!

Na kadri ziku zinavyokwenda bila Watanzania kuelezwa, kumuona, ndivyo kizazi cha kuhoji, kinavyozidi kuhoji!.
Sikumbuki kama Watanzania, tuliwahi kuelezwa sababu za kuuliwa kwa rais wa kwanza wa Zanzibar, Abedi Amani Karume, Sikumbuki kama Watanzania tuliwahi kuelezwa sababu za kujiuzulu kwa Aboud Jumbe Mwinyi, aliyekuwa rais wa pili wa Zanzibar baada ya kuuliwa Karume. Sikumbuki kama Watanzania, tumewahi kuelezwa, sababu za kujiuzulu uwaziri Mkuu wa JMT, Edward Lowassa, hivyo sijui kama tutakuja kuelezwa sababu.

Mzee. P
 
Kutounga mkono vitendo vya utekaji, ukandamizaji, mauaji, kubambikia kesi wapinzani, kudai katiba mpya
Kuna picha moja yupo Nchimbi, Lissu, Mnyika na Father Charles Kitima, sasa fanya tathmini kupata tafsiri ya kitu hapo kwanza kabisa Father Charles Kitima aliwahi kuvamiwa huko nyuma na kupigwa na kuumizwa vibaya sana sababu ya kumsemasema mtu yule ikawa hivyo, Lissu the same unajua kinachoendelea hadi hivi sasa sababu ya kumsemasema mtu yule, Mnyika yupo down ila yalimkuta mazonge hapo kati yakaishaisha hivyo sababu ndio vile sasa hivi hasikiki, Nchimbi the same na yeye kawekwa kwenye radar ikawa km ilivyokua akaanza kuongelea Katiba Mpya akawahamasisha watu wadai Katiba Mpya kitu ambacho mtu yule yeye alishasema ni "Kijitabu tu" kwa hio msinisumbue na hicho "Kijitabu", basi ndio hivyo wakamshushia rungu yakamkuta ya kumkuta sasa hivi hasikiki tena na haonekani tena, una swali lingine uliza ujibiwe
 
Maskin kijana wa watu hakuwa na kosa lolote !! Et kukemea mauaji, rushwa , kutaka utawala bora ,katiba mpya , kuzuia kutekana na kupenda demockasia ndiyo kumemponza .... ila kaondoka hana damu mikono yake iko salama mimi ninamuombea sana kijana huyu mzalendo wa kweli aliyeipenda nchi yake
 
Jana katika pitapita nilisoma mfano wa jamaa mmoja alieleza nitaeleza km alivyoeleza ila maana utajipatia mwenyewe alimaanisha nini

Alisema;

Kuna majambazi walijipanga kuvamia eneo fulani wakiwa na silaha za moto, katika makubariano ya hao majambazi jambazi mkuu na wale wasaidizi wake na vijakazi wakakubariana wanavamia hilo eneo ila sharti kuu hakuna kuua mtu na hakuna kumwaga damu hata iweje, basi wakakubariana sawa sawa.

Baada ya kufika eneo la tukio wameshavamia na kuweka watu chini ya ulinzi wale majambazi wakaanza kufanya tofauti na wakivyokubariana, wakaanza kubaka watu, kuwafira, kuwalawiti na kuwaua watu, wakamwaga damu za kutosha siku hio, kisha wakatokomea kusikojulikana na hawakufanikiwa kukamatwa wala kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria.

Baada ya kurudi kufanya tukio hilo la kihalifu, vyombo vya habari dunia nzima vikaanza kutangaza kuhusu uhalifu huo uliofanywa na hao majambazi, baadhi ya majambazi ambao hawakuafiki suala lile la kubaka, kufira, kulawiti na kuua wakaanza kua against na wale waliofanya lile tukio inamaana ugomvi baina ya majambazi ukaanzia hapo kwamba tulikubariana tukienda tunaenda kuwatuliza tu ila hakuna kubaka, hakuna kufira, hakuna kulawili wala hakuna kumwaga damu imekuaje nyinyi mmeenda kufanya unyama wote ule? Ugomvi ukaanzia hapo majambazi wakaanza kugombana wao kwa wao

Mwisho wa kunukuu
 
Nimekuelewa Mkuu
 
Back
Top Bottom