Mpaka Mwalimu Nyerere anaondoka madarakani, uchumi wa Tanzania ulikuwa ni mkubwa kuliko wa Kenya. Marais waliomfuatia walikwama wapi?

Unaweza kuleta na takwimu za GNP ? Halafu ndio tuongee vizuri
 
Inaelekea mmesahau au hamjui hali ilivyokuwa ngumu kuanzia 1980 hadi 1985, ukisikia kufunga mkanda unajua maana yake nini?

Wakati Nyerere anaondoka madarakani watu wanavaa midabwada, magunia, bidhaa adimu, Deni la kutisha la Taifa, Uchumi ulikuwa unakua kwa negative growth, halafu unazungumzia habari za GDP?
Labda wewe hukuwepo mwaka 1985 nchi ilivyokuwa choka mbaya
 
Ethiopia tatizo ni less resourceful ukilinganisha na nchi zingine ndio maana kwa sasa investment yao kubwa ni kwenye service industry ambayo ni muhimu pia...

Kenya itaendelea mbele zaidi sababu ya human resource na wanazidi kuinvest humo maana ndo point yao kubwa of Economic supremacy, Tanzania tukiweka nguvu hapa hatutoshikika
Hatuna dalili ya kuandaa vyema human capital, tazama products za vyuo vyetu Nadhani CCM inachangia kwa kiasi kikubwa vijana wengi waroho na waongo, usitegemee kutangeneza nchi kwa vijana wa silka hiyo. Huenda tukibadili uongozi tunaweza kuona matokeo, jpm alijaribu kwenye vyeti feki akakwama
 
Acha uongo, kipindi cha nyerere kulikuwa na shida kubwa sana ukilinganisha na kipindi cha Mwinyi, mkapa, na Kikwete.

Hao wanaoleta historia za uchumi wa Nyerere kuwa mzuri mwaka 1985, hawajui wanazungumza nini!

Underperformance ya Kenya mwaka 1985 haimfanyi Nyerere kuwa alifanya uchumi wetu uwe mzuri.

Mleta mada ananikumbusha stori za mtu anayefurahia baada ya kufeli mtihani kwa sababu kichwa wa darasa naye kafeli. Akipiga difference ya marks baina yao anaona ni ndogo then anaona yes iko poa.

bora angefurahia kufaulu licha ya kwamba kichwa wa darasa kampiga gepu kubwa kwenye ufaulu!

Huo ndo mfano wa Uchumi wa Kenya na Tanzania tangu enzi za Nyerere hadi leo
 
Hatuna dalili ya kuandaa vyema human capital, tazama products za vyuo vyetu Nadhani CCM inachangia kwa kiasi kikubwa vijana wengi waroho na waongo, usitegemee kutangeneza nchi kwa vijana wa silka hiyo. Huenda tukibadili uongozi tunaweza kuona matokeo, jpm alijaribu kwenye vyeti feki akakwama

ukiniuliza mimi Elimu bure bado ilikuwa sio solution ama kwa jina jingine "BAD MOVE" japo inaungwa kwa nguvu zote na watu wanaotumia zaidi emotions

tatizo la hii elimu lipo kwenye miundombinu na content yake. Bado ipo kwenye kutoa information kuhusu mambo mbali mbali lakini sio transformational, walimu wenyewe wamechoka na cream yetu ya taifa haitaki kujiingiza huko.maana ni kama ajira ya watu wa chini

na hata kwa time hii ambapo hizo cream zipo mtaani kwa kukosa ajira bado selection inafanywa kijima. in reality hatupo serious kwenye kutengeneza watu mwisho wa siku tutangeneza vitu vitakavyoendeshwa na foreigners. Sad !!!
 
Azimio la Arusha ndilo lilisababisha wazungu na wahindi kibao walifunga virago Wakati Kenya wwaliwabakiza

Unachongea uongo uchumi uliharibika NYERERE AKIWA madaraka usisukumie maraisi wengine

Vita ya kagera pia ilichangia uchumi kufa

Nchi ilikuwa tupu Haina hata pesa za kigeni.Mwinyi alipokea uongozi kwa Nyerere nchi ikiwa hoi bin taabani kiuchumi

Mleta mada Kawadanganyeni wajnga wenzio

Azimio la Arusha lengo lake halikuwa la muda mfupi. Ndio maana wengi leo tunaweza kumiliki ardhi. Kaoneni owners wa Ardhi Kenya ni kina nani.
Tunaweza kubeza Azimio la Arusha sababu ya kuamua kutoona mbali. Ila malengo yake mpaka kesho na hata kesho kutwa yatabeba Haja za kizazi cha Tanzania. Ipo siku tena sio mbali, Kenya tutawaacha huko
 
Acha uongo, kipindi cha nyerere kulikuwa na shida kubwa sana ukilinganisha na kipindi cha Mwinyi, mkapa, na Kikwete.

Unajua mataifa yote makubwa yalitaka kuona Nyerere anashindwa na anatolewa madarakani na vibaraka wao. Kiuchumi walihakikisha anashindwa. Strategy za kuiinua Kenya hazikuwa kwa bahati mbaya
 
Uongo!

Tanzania haijawahi kuwa na Uchumi mkubwa klk Kenya, simple logic tu mpaka Nyerere anaondoka TZ yetu ilikuwa planned socialist economy wakati Kenya ni capiatalistic from day one, kwanza Uchumi wa Kenya ulikuwa mkubwa mara 2 ya Tanzania, bidhaa karibia zote zilikuwa made in Kenya, hivyo sasa hivi ndiyo pengo limepungua lkn si TZ wala Uganda zilizowahi kuwa na Uchumi mkubwa klk Kenya, ...

In 70s Tanzania ilikuwa mbali kuliko Kenya
 
Kuna shida mahali.

Pamoja na watu kumnanga (very incorrectly and unfairly) Mwalimu Nyerere (RIP mzee wetu) kuhusu sera zake za uchumi, inaonekana dhahiri kuwa alikuwa akifanya vizuri zaidi kiuchumi kwa kuchukulia nchi ya Kenya kama benchmark. Nimeichukulia Kenya kama benchmark kwa vile ndiye mshindani wetu mkubwa kiuchumi kwenye EAC na mara zote Tanzania tumekuwa tukifanya kila jitihada kutaka kuwa juu yake.

Mnyonge mnyongeni lakini...

Sasa ukiangalia graphic trend kwenye video clip hii hapa chini utagundua kuwa wakati mwalimu alipokuwa anaondoka madarakani, Tanzania ilikuwa always juu ya Kenya kiuchumi (GDP) miaka ya 80s hadi anaondoka ofisini 1985. I mean pamoja na changamoto nyingi sana zilizopelekea mdororo wa kiuchumi kwenye late 70s (kuvunjika kwa EAC, vita vya Kagera, nk), bado Tanzania ilibaki kuwa ni "economy giant" kwenye EAC.

Sasa embu angalia performance ya marais waliofuata (ukimuondoa mzee Ruksa) vs Kenya kuanzia 1996:

Mkapa:
1996 aliingia na kukuta Kenya wametuzidi GDP kwa $6B
2005 alitoka na kuacha Kenya wametuzidi GDP kwa $2B
Alijitahidi kupunguza GDP gap, so tunaweza kumpongeza kwa hilo lakini alishindwa kufanya alichokifanya Mwalimu (yaani kuifanya TZ iwe economically superior to KE)!

JK:
2006 aiingia na kukuta Kenya wametuzidi GDP kwa $8B
2015 alitoka na kuacha Kenya wametuzidi GDP kwa $17B
JK aliruhusu gap lipanuke zaidi, pamoja na kwamba alijitahidi ku boost per capita kwa kiwango kikubwa kuliko Mkapa ($480B vs Mkapa's $330B).

JPM:
by 2016 Kenya walikuwa wametuzidi GDP kwa $20B
by 2020 Kenya tayari wameshatuzidi GDP kwa $44B
JPM is the worst performer vs Kenya. Sijui itakuwaje tukimpa tena nchi October - tunaweza kujikuta Kenya wametuzidi kwa $100B!

Kazi kwenu Watanzania. October hiyo yaja!

Mimi ningependa kusema hivi, jmbo la kwanza ni mimi ni mkenya na mara nyingi huwa nashindwa kueleza tofauti hii yaletwa na nini haswa, samehea kiswahili changu.
Anyway kuna mambo kadhaa ambayo nilifanya uchunguzi wangu na kuona ndio yaweza kuwa shida halisi. Awali nilijiuliza mbona iwe hivi wakati TZ lina idadi kubwa zaidi ya watu ,TZ ina eneo kubwa la ardhi tena lenye rotuba na madini kibao? and so I came up with the following issues which if you tanzanians mkiyatilia maanani basi mnaweza kutu pita tena kwa mbali;

1. UVIVU
Kuna muda fulani nilikuwa tanzania kwa muda wa mwezi mmoja hivi na nilizuru sehemu za arusha, manyara, ngorongoro na serengeti. Jambo nlilojionea pale lilinishangaza, watu wengi hawana msukumo wa kufanya kazi, jambo hili lina wadhuru sana kiuchumi. inastahili muwe mnaamka saa kumi asubuhi na kuchapa kazi ya aina yoyote kwa udi na uvumba. kenya twa fanya hivyo,,, twaamka mapema na twa fanya kazi kweli.

2. HASIRA ZA KIPUZI KUFWATIWA MAAMUZI YASIYO FAA
Kuna kipindi kenya ilizozana na uganda kuhusu migingo, tz wakashika ngombe za kenya na kuzipiga mnada halafu pia tz waka choma vifaranga zetu. tz ikaikataza kenya airways kupaa katika anga ya tz among others.
Chunguzeni kwa makini vile kenya huwa ina handle such issues. WE SIMPLY DONT FIGHT BACK, actually what we do ni kutafuta mazungumzo ya ki diplomasia ili kile kidogo tunapata kutoka tz au ug kiuchumi na tuendelee kukipata. Mna stahili kufata mfano huo kwa sababu TZ mnapenda sana kulipza kisasi mkiddani ndio njia bora.

3.KUTOPENDA WAGENI

Leo hii ukija kenya utakuta wa chaga kibao, utakuta wasomali kibao, utakuta wahindi kibao, utakuta wa sudanese kibao... hawa wote tunaishi nao kwa upendo hutojua hata kama si wakenya. kipindi kile nilikuwa TZ nilijionea ubaguzi openly na sio wakufichwa ...niliambiwa kabisa peupe. ilifika wakati hadi nikaletewa askari . ilhali wakati huo mimi nilikuwa tz kihalali kabisaa.
Cha ukweli hapa hampendi wageni, kuna vile wageni wanawakera kimpango sijawahi elewa ni kwa nini na jambo hili pia lina wagharimu kiuchumi.
Acheni wageni waje hata na waishi huko , wafanye biashara na hii kwa njia moja au nyingine itawainulia uchumi.

USHINDANI MBAYA

Mashindano ya aina yoyote ilre ni mazuri lakini do not put hard feelings ndani yake, shida nyingine hii hapa, mna machungu sana na kenya kwa kuwa ipo juu. machungu haya huwa yanafanya kubaki nyuma maana mtu hujisahau na kuanza kufikiria ya mwenzake sana. although hili sikulipa uzito sana.

ni kitambo niandike kiswahili kinachokaa sanifu hivi... I have really tried.
 
Mimi ningependa kusema hivi, jmbo la kwanza ni mimi ni mkenya na mara nyingi huwa nashindwa kueleza tofauti hii yaletwa na nini haswa, samehea kiswahili changu.
Anyway kuna mambo kadhaa ambayo nilifanya uchunguzi wangu na kuona ndio yaweza kuwa shida halisi. Awali nilijiuliza mbona iwe hivi wakati TZ lina idadi kubwa zaidi ya watu ,TZ ina eneo kubwa la ardhi tena lenye rotuba na madini kibao? and so I came up with the following issues which if you tanzanians mkiyatilia maanani basi mnaweza kutu pita tena kwa mbali;

1. UVIVU
Kuna muda fulani nilikuwa tanzania kwa muda wa mwezi mmoja hivi na nilizuru sehemu za arusha, manyara, ngorongoro na serengeti. Jambo nlilojionea pale lilinishangaza, watu wengi hawana msukumo wa kufanya kazi, jambo hili lina wadhuru sana kiuchumi. inastahili muwe mnaamka saa kumi asubuhi na kuchapa kazi ya aina yoyote kwa udi na uvumba. kenya twa fanya hivyo,,, twaamka mapema na twa fanya kazi kweli.

2. HASIRA ZA KIPUZI KUFWATIWA MAAMUZI YASIYO FAA
Kuna kipindi kenya ilizozana na uganda kuhusu migingo, tz wakashika ngombe za kenya na kuzipiga mnada halafu pia tz waka choma vifaranga zetu. tz ikaikataza kenya airways kupaa katika anga ya tz among others.
Chunguzeni kwa makini vile kenya huwa ina handle such issues. WE SIMPLY DONT FIGHT BACK, actually what we do ni kutafuta mazungumzo ya ki diplomasia ili kile kidogo tunapata kutoka tz au ug kiuchumi na tuendelee kukipata. Mna stahili kufata mfano huo kwa sababu TZ mnapenda sana kulipza kisasi mkiddani ndio njia bora.

3.KUTOPENDA WAGENI

Leo hii ukija kenya utakuta wa chaga kibao, utakuta wasomali kibao, utakuta wahindi kibao, utakuta wa sudanese kibao... hawa wote tunaishi nao kwa upendo hutojua hata kama si wakenya. kipindi kile nilikuwa TZ nilijionea ubaguzi openly na sio wakufichwa ...niliambiwa kabisa peupe. ilifika wakati hadi nikaletewa askari wakati nilikuwa humo tz kihalali kabisaa.
Cha ukweli hapa hampendi wageni, kuna vile wageni wanawakera kimpango sijawahi elewa ni kwa nini na jambo hili pia lina wagharimu kiuchumi.
Acheni wageni waje hata na waishi huko , wafanye biashara na hii kwa njia moja au nyingine itawainulia uchumi.

USHINDANI MBAYA

Mashindano ya aina yoyote ilre ni mazuri lakini do not put hard feelings ndani yake, shida nyingine hii hapa, mna machungu sana na kenya kwa kuwa ipo juu. machungu haya huwa yanafanya kubaki nyuma maana mtu hujisahau na kuanza kufikiria ya mwenzake sana. although hili sikulipa uzito sana.

ni kitambo niandike kiswahili kinachokaa sanifu hivi... I have really tried.
wacha matusi nyang'au wewe 😅😅😅...!! una maana Watz bado ni wavivu hata sasa chini ya #hapakazitu??!!
 
kwa ile akili ya Mwinyi unatarajia nini zaidi ya huu utopolo.
CCM toka iwepo ni mdororo wa uchumi toka mwanzo wake hata sasa haijalishi nani aliyeingia au kutoka!!
Wanajitahidi lakini ndio la kuvunda...
Hii nchi watu walishawahi kuishi kama nyau... hii nchi kuvaa ilionekana ni anasa... nchi hiihii sukari na sigara ziliwahi kuwa bidhaa adimu!!! Ni nchi hiihii Siha na gloria ilikuwa mikate bora huku watu wakigombea kuvaa cha cha cha na safa
 
Hivi purchasing power na uhakika wa kupata basic needs ukoje kati ya nchi hizi mi mgeni kidogo, naomba mnisaidie sijui vizuri kwa kuwa naamini kama watu wanaweza kumudu inaweza kuleta tija zaidi. japo kwangu naona kama kwa nchi yetu kuna mabadiliko makubwa toka miaka ya 2000 hasa kwa vijijini japo wamekuwa na changamoto za maji na huduma za jamii kama shule,maji na hospitali japo tukirasmisha na waganga wa kienyeji gap la afya linapungua (natania tu kwa kuwa kuna wilaya fulani kusini mtu akiumwa lazima aende kwa mganga na mganda ndo anaweza kumshauri hiki sio kirogo nenda hospitali achilia mbali kule vijijini kwa kibajaji watu wanakunywa maji ya kuchemsha kipindi cha dawa za daktari zikiisha na maagizo ya kuchemsha maji yanaishia hapo).
 
Unajua mataifa yote makubwa yalitaka kuona Nyerere anashindwa na anatolewa madarakani na vibaraka wao. Kiuchumi walihakikisha anashindwa. Strategy za kuiinua Kenya hazikuwa kwa bahati mbaya
Hizi porojo kweli Tanga wezi wengi, nyerere aliyekuwa kibaraka wa wazungu unajaribu kumsafisha kwa jiki, kadanganye watoto wenzio huko madrasa
 
In 70s Tanzania ilikuwa mbali kuliko Kenya

Siyo kweli, haijawahi kutokea, mpaka Mwalimu Nyerere anaondoka madarakani Tanzania yetu ilikuwa nchi ya 3 kwa umaskini Duniani baada ya Baglandeshi na Msumbiji, Kenya haijawahi kuwa nchini hivyo kwa maana ni capitalistic economy tangia ukoloni, miaka ya 70 Tanzania ilikuwa inategema misaada ktk nje kwa > 85%, Kenya haijawahi kutegemea misaada kwa kiwango hicho, siku zote imekuwa ikifadhili bajeti zake kwa kodi kama tufanyavyo sisi leo hii.

Tanzania yetu haijawahi kuipita Kenya Kiuchumi tangia kuchukuliwa na Mkoloni Muingereza labda wakati wa Mjerumani hapo sijui hali ilikuwaje, ...
 
takwimu hazidanganyi ndugu!
 
takwimu hazidanganyi ndugu!

Weka hapa hizo takwimu, hata logic ya kawaida tu inakwambia, labda nikuulize kwa nini Jumuiya ya AM ilivunjika kama ni kweli Tanzania ilikuwa ni tajiri zaidi ya Kenya? Unaijua sababu hasa?
 
Source/chanzo cha habari hii?
Kuna shida mahali.

Pamoja na watu kumnanga (very incorrectly and unfairly) Mwalimu Nyerere (RIP mzee wetu) kuhusu sera zake za uchumi, inaonekana dhahiri kuwa alikuwa akifanya vizuri zaidi kiuchumi kwa kuchukulia nchi ya Kenya kama benchmark. Nimeichukulia Kenya kama benchmark kwa vile ndiye mshindani wetu mkubwa kiuchumi kwenye EAC na mara zote Tanzania tumekuwa tukifanya kila jitihada kutaka kuwa juu yake.

Mnyonge mnyongeni lakini...

Sasa ukiangalia graphic trend kwenye video clip hii hapa chini utagundua kuwa wakati mwalimu alipokuwa anaondoka madarakani, Tanzania ilikuwa always juu ya Kenya kiuchumi (GDP) miaka ya 80s hadi anaondoka ofisini 1985. I mean pamoja na changamoto nyingi sana zilizopelekea mdororo wa kiuchumi kwenye late 70s (kuvunjika kwa EAC, vita vya Kagera, nk), bado Tanzania ilibaki kuwa ni "economy giant" kwenye EAC.

Sasa embu angalia performance ya marais waliofuata (ukimuondoa mzee Ruksa) vs Kenya kuanzia 1996:

Mkapa:
1996 aliingia na kukuta Kenya wametuzidi GDP kwa $6B
2005 alitoka na kuacha Kenya wametuzidi GDP kwa $2B
Alijitahidi kupunguza GDP gap, so tunaweza kumpongeza kwa hilo lakini alishindwa kufanya alichokifanya Mwalimu (yaani kuifanya TZ iwe economically superior to KE)!

JK:
2006 aiingia na kukuta Kenya wametuzidi GDP kwa $8B
2015 alitoka na kuacha Kenya wametuzidi GDP kwa $17B
JK aliruhusu gap lipanuke zaidi, pamoja na kwamba alijitahidi ku boost per capita kwa kiwango kikubwa kuliko Mkapa ($480B vs Mkapa's $330B).

JPM:
by 2016 Kenya walikuwa wametuzidi GDP kwa $20B
by 2020 Kenya tayari wameshatuzidi GDP kwa $44B
JPM is the worst performer vs Kenya. Sijui itakuwaje tukimpa tena nchi October - tunaweza kujikuta Kenya wametuzidi kwa $100B!

Kazi kwenu Watanzania. October hiyo yaja!

Kwa Tanzania uchumi wetu ulikuwa more stable kwenye Era ya Mkapa wakati Kenya bado ilikuwa kwa Moi ambaye nae hakuwa mzuri

Kikwete kaingia lakini hakuwa mzuri kwenye uchumi ukilinganisha na mkapa, kigezo kizuri tu ni control ya mfumuko wa bei na thamani ya shillingi dhidi ya dollar. Ukirudi kwa Kenya time hiyo ndio aliingia Kibaki nayo ikawa golden Era kwa Kenya

Kibaki kaacha msingi imara haswa kwenye miundombinu na demokrasia, fikiria tu mfumo wa kenya kwa sasa ambao serikali kuu imeachia uhusu serikali za chini kama mikoa kujiamulia baadhi ya mambo yake kama budget. Hiyo imechochea zaidi ukuaji wa Kenya

Sitegemei Uchumi ukue in figures kwenye Kipindi cha magufuli maana Sera zake za uchumi ni kama anarekebisha na si kuukuza na mbaya zaidi Private sector inapumulia mashine tu. So, Kenya kwa speed yao wapo vizuri though sisi bado tuna potential kubwa ya kukua kuliko wao
Mwai kibaki was Best president Ever
 
Back
Top Bottom