Mpaka sasa bado sijaona makosa ya Hayati Magufuli labda kosa alilonalo ni kuipenda Tanzania kwa maisha yake na huo ndio upendo wa kweli.

Mkuu, ungetukumbusha pia kuwa weww ni NANI labda.

Kwani umeshapewa hiyo nafasi ya kuipenda nchi?

Unayo ushahidi wa kila uliloliongea?

Kariakoo wamegoma kule!
Mimi ni raia mwema mweny mapenzi na nchi, kuzaliwa Tanzania pekee ni nafasi ya kuipenda nchi ambayo sio ya kupigiwa kura wala ya kuteuliwa
 
Mimi ni raia mwema mweny mapenzi na nchi, kuzaliwa Tanzania pekee ni nafasi ya kuipenda nchi ambayo sio ya kupigiwa kura wala ya kuteuliwa
Mkuu, mamlaka ni kwa mujibu wa taratibu, na nadhani kwa mujibu wa vitabu vya imani, vinaamuru KUTII MAMLAKA.

Hayo mapenzi kwa nchi ni yapi kama unamtuhumu aliyekuwa KIONGOZI mkuu wa nchi bila ushahidi wowote?

Huo sio UHAINI?

Hakuna kesi moja kwenye hizi mahakama zetu, sio kumshitaki marehemu, angalau tu kudai haki walionyimwa hao walalamikaji!

Kinyume chake, serikali ya sasa, mara iwarudishe vyeti feki, mara iwalipe sijui nini! Ukiangalia facts zao, ni ku-gain popularity tu
 
Basi tuendele kutii mamlaka mkuu, hata ikirudisha vyeyi feki, ikituuza kwa mikopo ya masharti haramu bado tuendelee kutii mamlaka tusifanye uhaini

Penye makosa lazima tuseme ili Taifa likae kwenye msitari, viongozi sio malaika kwamba hawakosei, na kumbuka maamuzi ya viongozi yanaweza kuangamiza au kuliponya taifa
 
Penye makosa lazima tuseme ili Taifa likae kwenye msitari, viongozi sio malaika kwamba hawakosei, na kumbuka maamuzi ya viongozi yanaweza kuangamiza au kuliponya taifa
👍
 
Kwa vile hakuua aliye wako!
 
Hizo 1.5b aliingiza kwenye account yake binafsi au "alitohoa" matumizi?

Tofautisha ufisadi unaopigiwa kelele sasa na kubadilisha "mfumo" wa manunuzi ama matumizi lakini fedha zikawa zimefanya kazi zile zile za umma kwa mtindo mwingine.

Mimi niseme tu kwamba haitakuja kunitokea hata siku moja kum'rank' Magufuli tofauti, kwa maelezo yoyote mabaya anayozuliwa kwayo hivi sasa baada ya kifo chake.

Ujue, sababu kubwa hasa inayofanya watu kuanza kulalamika na kukufuru baada ya kifo chake ni zile tabia za kuleana zilizomo kwenye damu, wizi na janja janja walizozoea waTz.

Uhalifu ulishakuwa ni utamaduni wa jamii, ndiyo maana hata ufisadi unaofanywa sasa, hakuna anayeshangaa wala kujali.

Alivyofukuza watumishi wa umma wenye vyeti ghushi, viongozi wasiowajibika nk nk, tunajua hakuna ulimi wala vinywa vyao ama vya wahalifu wengine vinavyoweza kumsema vyema pamwe kutambua mchango wake mkubwa alioutoa kwa Taifa hili na kuacha alama za kudumu kwa kipindi chake kifupi.

Mwenyezi Mungu amuweke mahali pema peponi, amina.
 
Ukiulizwa maswali huwezi jibu!

Mfano mdogo, unasema aliiba 1.5t, utuambie alizipeleka wapi na kwenye makusanyo gani ambapo unasema alipika data za TRA na wakati huo huo akifanya ujenzi wa miradi mikubwa mikubwa Karibu nchi nzima?

Kwa sasa serikali inakopa sana na inasema inakusanya kuliko kipindi cha mpika data, utuambie, kwa nini serikali ya sasa inayokusanya kodi kwa wingi zaidi na ambapo miaka yote miwili haijajenga barabara mpya hata moja tu, pesa wanapeleka wapi?

Ukisema inapeleka kwenye miradi, miradi ipi iliyoongezwa tofauti na iliyoikuta?

embu thibitisha wizi wa Magufuli tuuone mkuu
 
Swala la wabunge pekee wa ccm,lilitokana na upinzani kutosimamia ajenda maalum.

Kila kitu wanakataa,kila kitu wanakubali.

Akaona hawa ni wahuni tu.
Muhuni alikuwa yeye sio upinzani. Ndio maana kila siku alikiwa anahangaika na upinzani mpaka anaondoka.
 
Alikosea alipofukuza vyeti feki halafu akamteua Makonda kuwa mkuu wa mkoa.
 
Bora hata angeiba Trilioni 700 haisumbui kama kumpoteza Ben Saa8 na Azory Gwanda kutaka kwa uchache.
 
Au we kwa vile hukutekwa? Waulize waliotekwa, kuiba pesa kwenye account zao, kufukuza watu bila ushahidi eti vyeti feki wakati ki ukweli siyo kweli ndo mana wamerudishwa, kuua au kumpoteza kila anayempinga, lisu kushambuliwa kwa risasi kama ng'ombe nk
 
Swala la wabunge pekee wa ccm,lilitokana na upinzani kutosimamia ajenda maalum.

Kila kitu wanakataa,kila kitu wanakubali.

Akaona hawa ni wahuni tu.
Yeye ndio anaamua ipi iwe ajenda kwa wananchi? Wananchi wanachagua wamtakaye, sio anayetakiwa au kuwa mtiifu kwa rais.
 
Yeye ndio anaamua ipi iwe ajenda kwa wananchi? Wananchi wanachagua wamtakaye, sio anayetakiwa au kuwa mtiifu kwa rais.

Nani alikwambia nchi hii wananchi wanaamua wanayemtaka??
 
Ukichunguza kwa jicho la tatu wanamchukia Magufuli ni wale walamba asali, majizi, wauza madawa ya kulevya, wafanyabiashara wa siasa wanajitafutia kipato kwa njia isiyohalali, vyeti feki, wakwepa kodi, wadhulumaji wapigaji huku wakijificha kwenye kichaka cha democrasia na haki za binadamu mfano kusema watu wanatekwa, wanauawa wameokotwa kwenye mifuko lakini hawa watu wanajimwambafai ni watetezi wa haki za binadamu ukuwaulizi mbona dk ulimboka alitekwa na kung'olewa meno,dk Mvungi aliuawa, David Mwangosi aliuawa,na kibiti,ikwiriri police waliuawa na viongozi wa CCM waliuawa mbona hatukuona malalamiko na utetezi wenu kumbe ndio hao hao mafisadi na vyeti feki ambao mirija yao ilifungwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…