Mpaka sasa bado sijaona makosa ya Hayati Magufuli labda kosa alilonalo ni kuipenda Tanzania kwa maisha yake na huo ndio upendo wa kweli.

Muhuni alikuwa yeye sio upinzani. Ndio maana kila siku alikiwa anahangaika na upinzani mpaka anaondoka.
Upinzani gani unaouzungumzia mzee au wapinzani ndio hawa wafanyabiashara wa siasa wanajitafutia kipato kwa njia isiyohalali kupitia siasa walilambishwa asali husiki kelele za kutetea maslahi ya wananchi
 
Utekaji,uuaji,kubambikia watu kesi,ukabila na ukanda,ubadhirifu na kubwa kuliko yote wizi wa kura. Haya ndiyo yamemfanya awe motoni sasa hivi.
 
Mwacheni mzee wa watu apumzike
 
Magufuli alikosea hapa:
1. Kutopandisha madaraja wafanyakazi ambalo ni takwa la kisheria.
2. Kutoajiri kama mzee Kikwete ambapo mpaka sasa wahitimu wamerundikana majumbani huku wakipigiwa mambio ya kujiajiri wakati elimu waliyopewa ni ya kuajiriwa.
3. Kuruhusu wasiojulikana wakaua watu wanaopaswa kuwalinda.
4. Kughairisha kupeleka SGR Kigoma na kupendelea njia ya kuelekea kwao usukumani.
5. Kukosa kabisa political tolerance.
6. Niongeze hujatosheka?...........
 
Umempa facts akikujibu nitag
 
K
Kila mtu ana maoni yake kuhusu Magufuli. Kwangu Mimi alikuwa worst president maana aliendekeza chuki za kisiasa hata Kama kuua angeua. Mimi yalinikuta kisa nipo Chadema.
Umber shida ni itikadi ya kisiasa aisee nilikuwa sijui hilo
 
Magufuli alikuwa mshenzi tu bana, mazuri gani alifanya? Mtu ambaye anasema nitawafanya matajiri waishi kama mashetani anaweza akawa na zuri?

Ningemuelewa kama angesema "Nitawafanya maskini waishi kama matajiri"

Hivi kweli inaingia akilini Magufuli anaiba mpaka uchaguzi wa Serikali za mitaa? Kweli hayo ndiyo mazuri? Acheni mzaha, yule ilikuwa lazima aage dunia tu kwa uovu wake
 
Inabidi uwe na akili ambazo zinafikiria principles, policies na sustainability!
Lakini ukiwa na akili za uchawa huwezi kuona makosa ya JPM. Marehemu alifanikiwa sana kuwarubuni kwa miradi ambayo hata wewe au mwingine angeweza kuifanya kumbe nyuma ya pazia alikuwa na madhaifu mengi sana!
Serikali lazima iajiri watu wake! Hakufanya!
Serikali lazima iangalie maslahi ya wafanyakazi wake! Hakufanya!
Serikali lazima iwe na sera za haki sawa Kwa kila raia... Alionesha wazi wazi kuwapenda kikosi kazi kuliko kawaida!
Alidhulumu na kuwaibia watu wazi wazi! Tena kwa dharau!
Kwangu... Ni aina ya watu waliofanikiwa kushika nafasi za juu kwa sababu nchi imepoteza dira na muelekeo!
Zaidi ya kuibua na kueneza chuki... Hakuna jipya alilotenda!
 
Ni mbiu za kihalifu zinazopigwa zisizo na vielelezo.
Hawezi na akikuwekea hivyo vielelezo na kujibu hayo maswali magumu kwa usahihi, naomba unitag.
 
Haiti kwenye viroba
 
Kosa lake kubwa ni kuwachukia mafisadi mpaka ndani ya Chama chake !!
 
Upinzani gani unaouzungumzia mzee au wapinzani ndio hawa wafanyabiashara wa siasa wanajitafutia kipato kwa njia isiyohalali kupitia siasa walilambishwa asali husiki kelele za kutetea maslahi ya wananchi
Wananchi wapi wa kuwatete Tanzania hii, hakuna kitu kigumu kama kuwatetea watu ambao wameridhika na hawajitambui, mara ngapi wapinzani wamwteswa, wamefungwa, wamwsingiziwa kesi, wapepigwa na polisi, wamewekwa ndani, na hata familia zao kupitia mateso kwa sababu ya kutetea wananchi, kuna mwanannchi hata mmoja aliwahi kunyanyuka kuungana na upinzani kutetea wanachosimamia? Sanasan tutapiga kelele kwenye keyboard, Watanzania tumeridhika hatuhitaji mtetezi waacheni walambe asali sasa maana mateso waliyopitia yametosha

Tubaki hivihivi mpaka siku akili zitarudi, tusiwatwishe mzigo wa kututetea watu wengine eti kisa mi wapinzani
 
Hivi wewe ni jini unaekunywa damu za watu waliopotezwa kuuliwa na kusokomezwa kusikojulikana hadi leo? wale waburundi waliokodiwa kushughulikia wanaoleta fyokoyoko kule Zanzibar siku za uchaguzi ulikunywa wewe damu zao? watu waliotekwa na wengine kupigwa risasi kupata ulemavu pia sio chochote, watu wenye maduka ya kubadilisha fedha za kigeni kunyanganywa hela zao kwa nguvu pia si chochote lakini haki za watu waliopiga kura na kuchagua watu wao badala yake uhuni ukafanyika wakaekwa aliotaka na kujisifu kwa wabunge mimi ndio nimekuleteni hapa bungeni na mengine mkuu, watu kuvunjiwa majumba yao na kunyanganywa mashamba yao ya miaka nenda miaka rudi bado si chochote si lolote, makesi watu kubambikiwa na kusekwa jela
 
Alale anapostahili na ahukumiwe kulingana na matendo yake, hakuna cha alale pma peponi, huo mi msemo tu, kila mtu huwa analala anapostahili
 
1. Hivi wewe, unajua zile 1.5T zilizotajwa na CAG, zilipo?

2. Wewe hivi unafahamu wale wakurugenzi wa NSSF waliotumbuliwa naye, na akawaweka wapya, hivi unafahamu kuna nafasi moja walikuwa wanalipwa watu wawili (mtumbuliwa na mteuliwa mpya) kwa mwaka mzima?

3. Unafahamu kituo cha mafuta cha TOTAL kilichopo mlimani city alikibomoa na jamaa wakalipwa fidia, na kituo kimejengwa tena pale pale?

4. Unafahamu kuwa kuna kituo cha mafuta kule Mwanza nacho alikibomoa na tukalipishwa?

5. Unajuwa hela za pre-bargai zilienda wapi?

ETC..

BTW,
Unadhani kwanini Rais Samia alisema kulikuwa na simba wa yuda?
Kwanini Kimei juzi tu hapa amesema watu walikuwa wanaziogopa benki?
ETC...

Ukifanya kama afanyavyo mbuni, kwamba alipokuona anajua haupo, basi anaamua aingize kichwa majanini, HUTAONA BWANA YULE ALICHEMKA WAPI, NA ITAKUWA UMEFANYA KWA MAKUSUDI TU..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…