Mpaka sasa Bashe ndiyo kijana mzalendo wa ukweli atakayeleta mapinduzi ya kilimo na uchumi

Mpaka sasa Bashe ndiyo kijana mzalendo wa ukweli atakayeleta mapinduzi ya kilimo na uchumi

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
14,311
Reaction score
36,056
Wasalamu wana JF,

Wakati vijana wengine wako busy na ku-bet, Bashe ni kijana anayetaka kuleta mapinduzi ya kweli ya kilimo na uchumi

Kilimo ni biashara kama biashara nyingine, na kwa bahati nzuri sehemu kubwa ya raia wetu wanajishughulisha nayo.

Sasa basi, ukiongeza thamani ya mazao, yaani ukihakikisha mkulima anapata bei nzuri ya mazao yake inayotokana na ushindani wa soko, maana yake umenyanyua vipato vya wakulima ambao ni raia wengi sana.

Impact yake ni nini, vijana wengi wataingia kwenye kilimo kama ajira rasmi, uzalishaji utaongezeka na pia utanyunyua GDP na pato la wastani la wananchi wengi, mwisho wake ni kwamba unaongeza purchasing power ya watu wengi na kuboresha hali za maisha za watu wako.

Hatua anazochukua Bashe ni za kimapinduzi na za kizalendo.

Bashe alindwe na apewe ushirikiano.
 
Sisi tunaolima tunamuelewa sana, Mungu azidi kuwaongoza viongozi wetu waendeleee kuona kilimo ni biashara kama biashara zingine.

Hakika ni muda wetu wakulima. Kwa wale mnaotaka Michele uuzwe buku basi muda ndo huu twendeni mashambani mkaone ilivyo ngumu kufikia hatua ya kuvuna
 
Hakuna mzalendo hapo na hakuna mkulima anatefaidika na mazao kuuzwa nje ya nchi zaidi ya mafisadi

Yupo kwenye uwaziri kwasababu mzee yupo kwenye chama
Hakuna jitihada isiyo na changamoto, zitatatuliwa jinsi zinavyotokea, hii ndiyo njia pekee ya kuwainua wakulima na kuinua uchumi wa nchi yetu
 
Sisi tunaolima tunamuelewa sana,mungu azidi kuwaongoza viongozi wetu waendeleee kuona kilimo ni biashara kama biashara zingine.Hakika ni muda wetu wakulima. Kwa wale mnaotaka Michele uuzwe buku basi muda ndo huu twendeni mashambani mkaone ilivyo ngumu kufikia hatua ya kuvuna.
Hakika
 
Tuwatoe vijana kwenye kubet kama tumeshindwa kuwaajili Wacha wajiajili kupitia kilimo,kilimo ndio UTI wa mgongo Bashe na Serikali wapo sahihi kuwarahisishia njia na kuwawekea mazingira mzuri. Tena Mheshimiwa Waziri kasisitiza hakuna kilimo Cha Whatsapp Wala Instagram vijana waingie field nitajitahidi mwaka huu niingie shambani Mwenyezi Mungu akijaalia, Waziri Bashe na Rais Samia tuwaungwe mkono kwenye hili.
 
Hakika mkuu
 
Bashe ni msomali. Kachagua kujifungamanisha na kundi la wahuni. Nyie chawa wake anawapa tabu tu, tunamfahamu.
 
Bashe ni msomali. Kachagua kujifungamanisha na kundi la wahuni. Nyie chawa wake anawapa tabu tu, tunamfahamu.
Nchi hii ina watu wenye asili mbali mbali, wahindi, wasomali, wazungu na mashetani kama wewe. Tunachoangalia ni jambo gani jema huyo mtanzania analifanyia taifa lake. Wapo watu wazawa wanaibomoa hii nchi kwa kasi sana. Hivyo, asili ya mtu siyo kigezo.
 
Wasalamu wana JF,

Wakati vijana wengine wako busy na ku-bet, Bashe ni kijana anayetaka kuleta mapinduzi ya kweli ya kilimo na uchumi

Kilimo ni biashara kama biashara nyingine, na kwa bahati nzuri sehemu kubwa ya raia wetu wanajishughulisha nayo.

Sasa basi, ukiongeza thamani ya mazao, yaani ukihakikisha mkulima anapata bei nzuri ya mazao yake inayotokana na ushindani wa soko, maana yake umenyanyua vipato vya wakulima ambao ni raia wengi sana.

Impact yake ni nini, vijana wengi wataingia kwenye kilimo kama ajira rasmi, uzalishaji utaongezeka na pia utanyunyua GDP na pato la wastani la wananchi wengi, mwisho wake ni kwamba unaongeza purchasing power ya watu wengi na kuboresha hali za maisha za watu wako.

Hatua anazochukua Bashe ni za kimapinduzi na za kizalendo.

Bashe alindwe na apewe ushirikiano.
Tanzania tuna Wakulima wa Bustani,wewe unalima heka moja au tano unajiita Mkulima kweli!
Kama tunataka kuwekeza kwenye Kilimo ni mwendo wa kufungua plantations au Ranches au mnafikiri Mwalimu Nyerere alikuwa mjinga?
Mapinduzi ya Kilimo kwa bajeti ya Bilioni 900,kweli!
 
Nchi hii ina watu wenye asili mbali mbali, wahindi, wasomali, wazungu na mashetani kama wewe. Tunachoangalia ni jambo gani jema huyo mtanzania analifanyia taifa lake. Wapo watu wazawa wanaibomoa hii nchi kwa kasi sana. Hivyo, asili ya mtu siyo kigezo
Asili ya mtu sio kigezo? Nenda na wewe Somalia tuonea kama unaweza kuwa waziri kule.
 
Back
Top Bottom