Mpaka sasa CCM hawana Plan ya kueleweka kuendelea kushika Dola kwa ridhaa. Wana Missing systems za kutosha

Mpaka sasa CCM hawana Plan ya kueleweka kuendelea kushika Dola kwa ridhaa. Wana Missing systems za kutosha

Hamjambo wote!

1. Kwenye mambo ya Intelligence(ujasusi, ushushushu, unjangu) kuna kitu inaitwa Missing System/s.

2. Kitu hii ukikosa hata MTU binafsi mambo yako yanakuwa hatarini, usalama wako unakuwa mashakani.

3. Missing System ni uwepo wa ombwe la kimkakati, mfumo muhimu ambao unapaswa kuwepo ili kudhibiti, kutabiri, na kulinda nguvu za mamlaka, lakini mfumo huo haupo au haufanyi kazi.

4. Ni pale ambapo taasisi au chama kinaonekana kuwa na muundo kamili wa juu juu, lakini hakina mifumo ya ndani ya kusoma hatari, kupanga mustakabali, na kudhibiti mabadiliko ya mazingira ya kisiasa.

5. Kwa lugha ya kijasusi, Missing Systems ni akili ya mfumo iliyopotea, ndiyo maana nguvu huporomoka Siku hadi Siku.

6. Matumizi na utegemezi wa vyombo vya Dola katika siasa ni dalili nyingine inayoashiria kabisa kuwa kuna Ombwe la kimfumo, mkakati, mipango, mbinu ambalo CCM wanalo.

7. Ni kiashiria kwamba CCM imebakiwa na risasi ya mwisho.

8. Katika siasa za kidemokrasia, kulitegemea jeshi la polisi na vyombo vya Dola ni kuliingiza jeshi kwenye siasa. Ni kusema jeshi linafanya siasa.

9. Mtibeli najaribu kueleza kuwa, kisaikolojia, kitu unachokitegemea ndicho kinachokuongoza na kukutawala.

10. Kisiasa, Unapotegemea jeshi na vyombo vingine vya Dola, wewe inageuka kivuli tuu. Vyombo vya dola ndio vinakuwa vinatawala.

11. Kwamba CCM kama itategemea vyombo vya Dola tafsiri yake CCM sio chama tawala tena, isipokuwa Jeshi ndio linatawala.

12. Kwa sababu huwezi sema CCM inatawala wakati ikiletewa vyama vingine ili ipambane navyo inaanza kulialia na kupigia magoti jeshi ili lisapoti chama(CCM). Kwamba bila Jeshi CCM haiwezi kufutukuta. Na hapo ndipo Missing system katika chama inajitokeza waziwazi.

13. Jeshi sio chama cha siasa. Ukishaliingiza Jeshi au vyombo vya usalama lazima utaona viashiria vya kimabavu na uonevu kwa raia ukijitokeza. Na hapa nazungumzia raia waliopo kwenye vyama vya siasa vya upinzani, au hata waliopo CCM lakini wakaonekana mwiba ndani ya Chama.

14. Missing system iliyopo CCM iliyopelekea kulitegemea jeshi tija yake ni ipi? Je ni tija endelevu?

15. Iko hivi mahali popote unaposikia Uasi, mapinduzi, machafuko na taifa kugawanyika lazima uelewe kuna namna Jeshi liliingilia au kuingizwa kwenye Siasa.

16. Ukishaliingiza Jeshi kwenye siasa basi tegemea Uasi, mapinduzi, machafuko na mambo ya Aina hiyo.

17. Jeshi linafanya kazi kwa mujibu wa Sheria, na msingi wake Mkuu ni NIDHAMU. Lakini NIDHAMU inamipaka yake.

18. Jeshi litakuwa na nidhamu kama halitaingizwa katika mambo ya Siasa. Kutumika kama ngao ya chama Fulani.
Kutumika kama ngao ya chama Fulani hiyo haiwezi kuwa nidhamu tena. Itakuwa siasa, itakuwa ni maslahi.

19. Jeshi likiendeshwa kwa maslahi na sio nidhamu kazi inakuwa imekwisha. Hakuna jeshi hapo. Ule Wito WA kizalendo wa kutumikia taifa na wananchi utakuwa umekufa kifo cha asili.
Na hapo ndipo vurugu zinapoanzia.

20. Wanajeshi na Askari sio roboti au midoli ya AI(Artificial intelligence) kwamba wenyewe hawana akili za kufikiri. Nidhamu ni kwaajili ya taifa na nchi. Si kwaajili ya mambo ya kisiasa(maslahi) ya kikundi au chama Fulani.

21. CCM kama hawataziona gap na kuziziba. Wakiacha missing systems hizo ziendelee kuwepo. Sioni namna ya wao kuendelea kushika madaraka.

22. Kitu kimoja niweke wazi ambacho kitasaidia pande zote. Kadiri nguvu nyingi zinavyotumika ndivyo hata Yale mafanikio yaliyopo yanaharibiwa.

23. Unapomuona Gaddafi na watoto wake inaweza kuwa mfano mzuri katika kuyaendea mambo ya kisiasa na kushughulika na kuwaongoza watu.

24. Jeshi ni muhimu lakini watu ni muhimu zaidi. Kwa sababu jeshi hutoka kwa Watu.

25. Kwenye ujasusi kuna kitu kinaitwa Correction. Ambapo serikali au taasisi za kiusalama hutumia mbinu hiyo kufanya marekebisho na kufuta makosa unnotice na watu wa kawaida ili kurejesha Imani ya watu kwa serikali au chama Fulani.

26. Lengo la Correction ni kuondoa missing system, lakini pia kulinda maslahi ya taifa na future ya viongozi baada ya kustaafu.

27. CCM lazima iwe na mpango kabambe kwamba watawezaje kusimama bila kutegemea Vyombo vya Dola. Na sio kujivunia kwamba wao Wana dola. Hiyo ni dalili ya upungufu wa maarifa na kuhatarisha usalama wa chama na taifa kea ujumla.

28. Kitu kimoja cha uhakika. Huwezi tegemea jeshi Siku au miaka yote kama nyenzo ya kupata madaraka na kutawala.

29. Kiintelejensia kadiri unavyotegemea Jeshi ndivyo unavyokuwa hatarini, na unakuwa na mashaka zaidi.
Sababu kuu ni kuwa jeshi nidhamu yake hukoma pale linapoingiza maslahi mbele(siasa).

30. Na nidhamu ikikoma, basi mambo yanakuwa hayatabiriki, na kiusalama kutotabirika yafsiri yake hakuna usalama.

Mimi nimemaliza. Acha Nile makande.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Dola ndiyo inayotaka CCM kubaki madarakani
 
CCM wanategemea dola tangu 1995,na dola inataka CCM iendelee kutawala sababu hakuna chama chenye uwezo wa kuitawala Tanzania na nchi ikabaki kama ilivyo

Kwa bara tangu 95-2010 CCM haikuwa na sababu ya kutegemea Dola kubaki madarakani.

Wananchi wengi hasa wakawaida wanaiamini.

Lakini tangu 2015 mpaka sasa wanasababu ya kuwa na hofu
 
kazi kubwa ya vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi ni kuwahadaa vijana malofa wa kifikra na kuwafanya mamaluki na kisha kuwachochea wakaandamane kwasababu za kubuni zisizo na ukweli wowote, ambazo matokeo yake vijana hao malofa waliobebwa ufala wa kifikra wakajitokeza kuandamana, kupora mali za watu, kuharibu miundombinu ya umma na binafsi na hatimae wakapeleka zawadi za huzuni na majonzi kwenye familia zao, huku vibaraka wakifurahia hali hiyo yenye malipo manono kutoka kwa mabwana zao wanao watumia.

sasa mmeamua kuja na porojo, uongo na uzushi mwingine tena? dah :pedroP:

kwamba CCM hii ni ya kutishwa na uzushi na porojo kama hizo gentleman? acheni uongo wa kubuni bana

Dunia ya Leo watu hawana akili za namna hii Gentleman
 
Kwa bara tangu 95-2010 CCM haikuwa na sababu ya kutegemea Dola kubaki madarakani.

Wananchi wengi hasa wakawaida wanaiamini.

Lakini tangu 2015 mpaka sasa wanasababu ya kuwa na hofu
Kutegemea dola unamaanisha vyombo vya dola kupiga na kufunga wapinzani au hata vyombo vya dola kuhesabu kura?..kama ni kuhesabu kura pia basi idara imehesabu kura tangu 1995
 
Kama hakuna consequences, wala accountability kwa wauaji ni nini kinakupa uhakika wa kutojirudia ? Mpaka sasa tumeonyeshwa kuwa dola inamamlaka kamili ya kutumia nguvu "inayostahili" kubaki madarakani

Watafanya mabadiliko kidogo.

Unamuda gani hujasikia mtu katekwa au kapotezwa Kwa sababu za kisiasa?
 
Watafanya mabadiliko kidogo.

Unamuda gani hujasikia mtu katekwa au kapotezwa Kwa sababu za kisiasa?
Wametekwa watu wengi na kupotea bila kuwa na mahusiano ya kisiasa,ila wanaharakati wanatembelea humohumo,watu wanatekana kwa mambo yao,wengi tu
 
Uko sahihi.

Tatizo la nchi yetu halipo CCM tuu. Bali lina mizizi ya kiutamaduni, desturi na falsafa zetu.

CCM wao kinachowasumbua ni hofu na kujiwekea uhakika wanaouona Kwa kinguvu. Hawataki kubet na kum- under estimate mpinzani wao. Ni nzuri hiyo kama haitatumika nguvu iliyopitiliza na kudhuru kabisa.
Lakini ni mbaya kama nguvu ikizidi Akili
Mimi huwa nawalaumu CCM sababu ni wao tu ndio wana nguvu ya kuung'oa huu mzizi, ila hawataki kufanya hivyo sababu wana uchu na tamaa ya madaraka,

Hii nchi ni CCM tu ndio anaweza kuibadili kwa amani bila kumwaga damu, na tena kwa mizizi yao laiti wangefanya hivyo basi wangetawala bila force daima.
 
Mimi huwa nawalaumu CCM sababu ni wao tu ndio wana nguvu ya kuung'oa huu mzizi, ila hawataki kufanya hivyo sababu wana uchu na tamaa ya madaraka,

Hii nchi ni CCM tu ndio anaweza kuibadili kwa amani bila kumwaga damu, na tena kwa mizizi yao laiti wangefanya hivyo basi wangetawala bila force daima.
Wanaoamua nani awe rais kupitia CCM siyo NEC wala kikao chochote cha chama bali deep state, yaani vigogo wa vyombo vya ulinzi na usalama na vigogo wastaafu,CCM ni rubber stamp tu
 
Wabadili mpango.

Alafu huwezi kuamini hata wakiweka haki na usawa bado Wana asilimia kubwa ya kushinda
Na hapo ndipo huwa nawashangaa. Huwa najiuliza shida ya CCM ni nini? Mbona bado uwezekano wa kushinda general election binafsi naona huwa bado wanao mwingi sana pamoja na upinzani mkali wanaokutana nao.
 
Mimi huwa nawalaumu CCM sababu ni wao tu ndio wana nguvu ya kuung'oa huu mzizi, ila hawataki kufanya hivyo sababu wana uchu na tamaa ya madaraka,

Hii nchi ni CCM tu ndio anaweza kuibadili kwa amani bila kumwaga damu, na tena kwa mizizi yao laiti wangefanya hivyo basi wangetawala bila force daima.
Huwa najiuliza INGE tokea NCHI Ina MAJI ya uhakika miundombinu ya uhakika, UMEME WA uhakika, teknolojia ya uhakika, NCHI isiyo na ufisadi nani aende kuandamana? China WANA chama kimoja TU na raia wanarizika MANA MAISHA wanayaona mr
 
Wanaoamua nani awe rais kupitia CCM siyo NEC wala kikao chochote cha chama bali deep state, yaani vigogo wa vyombo vya ulinzi na usalama na vigogo wastaafu,CCM ni rubber stamp tu
Sawa hao deep state unawatenganisha vipi na CCM, hap vigogo wa vyombo vya ulinzi na usalama ni CCM, vigogo wastaafu ni CCM pure.. kilichopo hao ni huwa wanapambana kuweka watu wao toka ndani ya CCM, rejea ishu ya mkapa 1995, jinsi kikwete alivyoenguliwa, rejea 2010 ishu ya lowasa huku magufuli, rejea 2025 kwa samia suluhu.

CCM ndio DEEP STATE yenyewe na kibaya zaidi woote hao hakuna anaejali masalahi ya taifa, hakuna anaeifikiria tanzania ya kesho wala mtanzania, wao ni wao na vizazi vyao.
 
Back
Top Bottom