Mpaka sasa CCM hawana Plan ya kueleweka kuendelea kushika Dola kwa ridhaa. Wana Missing systems za kutosha

Dola ndiyo inayotaka CCM kubaki madarakani
 
CCM wanategemea dola tangu 1995,na dola inataka CCM iendelee kutawala sababu hakuna chama chenye uwezo wa kuitawala Tanzania na nchi ikabaki kama ilivyo

Kwa bara tangu 95-2010 CCM haikuwa na sababu ya kutegemea Dola kubaki madarakani.

Wananchi wengi hasa wakawaida wanaiamini.

Lakini tangu 2015 mpaka sasa wanasababu ya kuwa na hofu
 

Dunia ya Leo watu hawana akili za namna hii Gentleman
 
Kwa bara tangu 95-2010 CCM haikuwa na sababu ya kutegemea Dola kubaki madarakani.

Wananchi wengi hasa wakawaida wanaiamini.

Lakini tangu 2015 mpaka sasa wanasababu ya kuwa na hofu
Kutegemea dola unamaanisha vyombo vya dola kupiga na kufunga wapinzani au hata vyombo vya dola kuhesabu kura?..kama ni kuhesabu kura pia basi idara imehesabu kura tangu 1995
 
Kama hakuna consequences, wala accountability kwa wauaji ni nini kinakupa uhakika wa kutojirudia ? Mpaka sasa tumeonyeshwa kuwa dola inamamlaka kamili ya kutumia nguvu "inayostahili" kubaki madarakani

Watafanya mabadiliko kidogo.

Unamuda gani hujasikia mtu katekwa au kapotezwa Kwa sababu za kisiasa?
 
Watafanya mabadiliko kidogo.

Unamuda gani hujasikia mtu katekwa au kapotezwa Kwa sababu za kisiasa?
Wametekwa watu wengi na kupotea bila kuwa na mahusiano ya kisiasa,ila wanaharakati wanatembelea humohumo,watu wanatekana kwa mambo yao,wengi tu
 
Mimi huwa nawalaumu CCM sababu ni wao tu ndio wana nguvu ya kuung'oa huu mzizi, ila hawataki kufanya hivyo sababu wana uchu na tamaa ya madaraka,

Hii nchi ni CCM tu ndio anaweza kuibadili kwa amani bila kumwaga damu, na tena kwa mizizi yao laiti wangefanya hivyo basi wangetawala bila force daima.
 
Wanaoamua nani awe rais kupitia CCM siyo NEC wala kikao chochote cha chama bali deep state, yaani vigogo wa vyombo vya ulinzi na usalama na vigogo wastaafu,CCM ni rubber stamp tu
 
Hata hili andiko ni tishio kwao ,Kila kitu wanaweweseka
 
Wabadili mpango.

Alafu huwezi kuamini hata wakiweka haki na usawa bado Wana asilimia kubwa ya kushinda
Na hapo ndipo huwa nawashangaa. Huwa najiuliza shida ya CCM ni nini? Mbona bado uwezekano wa kushinda general election binafsi naona huwa bado wanao mwingi sana pamoja na upinzani mkali wanaokutana nao.
 
Huwa najiuliza INGE tokea NCHI Ina MAJI ya uhakika miundombinu ya uhakika, UMEME WA uhakika, teknolojia ya uhakika, NCHI isiyo na ufisadi nani aende kuandamana? China WANA chama kimoja TU na raia wanarizika MANA MAISHA wanayaona mr
 
Wanaoamua nani awe rais kupitia CCM siyo NEC wala kikao chochote cha chama bali deep state, yaani vigogo wa vyombo vya ulinzi na usalama na vigogo wastaafu,CCM ni rubber stamp tu
Sawa hao deep state unawatenganisha vipi na CCM, hap vigogo wa vyombo vya ulinzi na usalama ni CCM, vigogo wastaafu ni CCM pure.. kilichopo hao ni huwa wanapambana kuweka watu wao toka ndani ya CCM, rejea ishu ya mkapa 1995, jinsi kikwete alivyoenguliwa, rejea 2010 ishu ya lowasa huku magufuli, rejea 2025 kwa samia suluhu.

CCM ndio DEEP STATE yenyewe na kibaya zaidi woote hao hakuna anaejali masalahi ya taifa, hakuna anaeifikiria tanzania ya kesho wala mtanzania, wao ni wao na vizazi vyao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…