Mpaka sasa CCM hawana Plan ya kueleweka kuendelea kushika Dola kwa ridhaa. Wana Missing systems za kutosha

Huwa najiuliza INGE tokea NCHI Ina MAJI ya uhakika miundombinu ya uhakika, UMEME WA uhakika, teknolojia ya uhakika, NCHI isiyo na ufisadi nani aende kuandamana? China WANA chama kimoja TU na raia wanarizika MANA MAISHA wanayaona mr
Shida ipo kwenye viongozi wetu ni washamba wa madaraka, ni walafi mnoo, hawajui kula na vipofu.
 
Piga makande shushia na bia mbili kwa bili ya ngu nduguu Taikoon
 
Polepole alisema ccm inahitaji kumwaga oil, watu wakaona ni bora gari itembee hivyo hivyo bila kumwaga oil.

Matokeo yake injini imeanza kugonga ila safari bado inaendelea.
 
Hiyo deep state inaitumia tu CCM, yaani siku pakiwa na chama kama CCM,haohao deep state wataipiga chini CCM na kukiingiza hicho chama madarakani Ili kituliza hali ya hewa na wataendelea kukidhibiti
 
Na hapo ndipo huwa nawashangaa. Huwa najiuliza shida ya CCM ni nini? Mbona bado uwezekano wa kushinda general election binafsi naona huwa bado wanao mwingi sana pamoja na upinzani mkali wanaokutana nao.
Si kweli. Sio kwa kizazi hiki cha Wasomi jobless!. Unadhani wanavyobaka uchaguzi wanajipendea?. Wanakuwa na taarifa kamili za uhakika kwamba HAWATOBOI
 
Hiyo deep state inaitumia tu CCM, yaani siku pakiwa na chama kama CCM,haohao deep state wataipiga chini CCM na kukiingiza hicho chama madarakani Ili kituliza hali ya hewa na wataendelea kukidhibiti
Mpaka sasa hakuna, na deep state ndio CCM wenyewe, hao hao deep state ni wazee wa maslahi yao kwanza, hakuna Kiongozi wa CCM kwa kizazi hiki ninaemuonq atakuja kwa ajili ya taifa, ni wizi tu na ubadhirifu ili yao yawaendee
 
Tatizo la nchi hii limekuwa kukubali habari za uchochezi na uzushi kutawala vichwa vya wasomi na wenye elimu zao.

CCM ukisoma humu mitandaoni unaweza kuamini kwamba haipo tena, lakini ukitazama kinachofanyika unaelewa uwepo wake bado haukwepeki.

Jamii inayoishi kwa kutegemea uchochezi, ulaghai na uzushi ina matatizo makubwa.

Ule uasi wa tarehe 29 October usiwadanganye mkaamini kwamba chama hakipo imara, mlitengeneza vurugu zikiwa sehemu ya uchochezi wenyewe lakini haijawasaidia chochote.

Nguvu ya upotoshaji hata siku moja haiwezi kushindana na namna kinachofanyika kinavyoyagusa maisha ya mtu mmoja mmoja na jamii nzima.

Mmetengeneza chuki na fitina nyingi za hatari lakini ukubwa wa kinachofanyika utaendelea kuizidi roho ya uchochezi.

Vijana waliingia mtaani tarehe 29 October baada ya hapo walioitishia maandamano wamejikuta wakiweka video za matukio ya zamani ili kuamsha hasira, mbinu ambayo imeangukia pua.
 
Mpaka sasa hakuna, na deep state ndio CCM wenyewe, hao hao deep state ni wazee wa maslahi yao kwanza, hakuna Kiongozi wa CCM kwa kizazi hiki ninaemuonq atakuja kwa ajili ya taifa, ni wizi tu na ubadhirifu ili yao yawaendee
Nyerere na mwinyi tu ndiyo sioni Nia ya maslahi toka kwao,waliobaki hasa walioshika nafasi kuu hawakosi udokozi wa hapa na pale
Hayo ma-deep state muda ukifika yataunda chama na mtakifuata na kitaingia ikulu,yaani mtauziwa gongo ileile kwenye chupa nyingine
 
Wabadili mpango.

Alafu huwezi kuamini hata wakiweka haki na usawa bado Wana asilimia kubwa ya kushinda
Hawana uwezo wa kupata 2/3 bungeni ya kuwaruhusu kuamua watakacho bungeni. Na wakikubali haki chaguzi mbili tu hawapo. Waliona ukweli huo chaguzi za 2010 na 2015. Hawako tayari tena kwa haki, machafuko pekee ndio yatawatoa kwani kwa sasa vyombo vya dola ndio nguvu yao pekee.
 
Viongozi wetu hawana UDOKOZI ni MAJAMBAZI.. iwe france, usa πŸ‡ΊπŸ‡Έ, πŸ‡¨πŸ‡³ Japan, πŸ‡°πŸ‡· πŸ‡¬πŸ‡§ πŸ‡©πŸ‡ͺ πŸ‡·πŸ‡Ί huko kote udokozi upo, ika kwanini wenzetu wameendelea sana, sio MAJAMBAZI kama haya ya kwetu.. kwenye 100 wanakula 2, sisi huku kwenye 100 wanakula 85, yaani kifupi wetu ni MAJAMBAZI A+
wenzetu huko wanakula na vipofu lakini pia wanajenga kwa taifa lao la kesho.. trump akija kusaka dili hapa ni litamnufaisha mmarekani na yeye mwenyewe kiasi.. sisi huku viongozi dili ni kuiba tu
 
Marais wa marekani hawaibi hazina bali hutumia nchi kupiga dili zao, trump na Venezuela, DRC, Bush na acacia, Obama na symbion, wanakuja hapa wanakaa siku tatu kuweka issue zao sawa
 
Marais wa marekani hawaibi hazina bali hutumia nchi kupiga dili zao, trump na Venezuela, DRC, Bush na acacia, Obama na symbion, wanakuja hapa wanakaa siku tatu kuweka issue zao sawa
Wanakuja wanapiga dili zenye manufaa kwao na taifa lao, ila sisi huku viongozi wetu ni dili kwa manufaa yao
 
Dili zao mkuu,not necessarily zinufaishe taifa lao
Mara nyingi taifa lao huwa halikosi kitu.. kuanzia makampuni yatakayofanya hiyo tenda na kila kitu lazima, taifa lifaidike, hivi unadhani mchina akija hapa, akaingia dili la gesi kampuni ya kichina ndio ichimbe hiyo gesi, unadhani china kama taifa haifaidiki?
Venezuela kule marekani kaona maslahi yake yameguswa binafsi na taifa kiujumla kaleta ubabeloni
 
Baada ya mauaji yale ya 29 Oct, ni ngumu CCM kujirekebisha na kujakukubalika, maana hawawezi kuaminika tena….inshort miaka ijayo upinzani mkali hautakuwa ni CCM na vyama vya upinzani bali ni CCM na Wananchi kama uchaguzi feki uliopita.
 

Inaweza kuwa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…