Baada ya CCM kumpitisha Gwajima , nina uhakika Mdee atashinda uchaguzi katika Jimbo hilo tena kwa kura nyingi zaidi safari hii kuliko ilivyokuwa mwaka 2015 unless haki isitendeke.
Ukiacha watu kuichoka CCM, Gwajima bado ataponzwa na kauli zake zilizoko mitandaoni na uzuri hapa Dar wenye smartphone ni wengi, hivyo itakuwa rahisi watu ku-share clips zake.
Sababu nyingine itayochangia ashindwe ni kutokuwa chaguo la wana-CCM bali amekuwa chaguo la viongozi wa CCM kwani hakushinda katika kura za maoni, hivyo ni wazi wako baadhi ya wana-CCM ambao hawatampigia kura..
Kingine,waumini wa Gwajima ni sehemu ndogo sana ya wakazi na wapiga kura wa Jimbo la Kawe, hivyo advantage ya yeye kuwa kiongozi wa dini ni ndogo sana kumbeba bila kusahau ukweli kuwa watanzania hawana sana utamaduni wa kuchagua mtu kwasababu tu ni kiongozi wa kidini.
Kuanzia leo nakuendelee tutarajie kuona clip za Gwajima zikiibuka upya na kwa kasi mitandaoni.
Halima huko aliko bila shaka atakuwa anachekelea kupata mpinzani ambae teyari ameshajiharibia kwa kauli zake mwenyewe.
Muda utaongea.