Mpaka sasa mitandao ya kijamii imekusaidiaje katika harakati za kupambana na umasikini?

Mpaka sasa mitandao ya kijamii imekusaidiaje katika harakati za kupambana na umasikini?

Mr. Purpose

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2016
Posts
1,468
Reaction score
2,767
Mkuu kwema? Pole na uchovu wa safari ya kuperuzi JF.

Matumizi ya mitandao ya kijamii Tanzania.png

Boss, ebu tuongee kidogo kuhusu hii mitandao ya kijamii mpaka leo imekusaidia chochote ?

Au unaonaga mauzauza tu 😅?

Graduate uliyehitimu chuo na hauna Ajira, vipi hii mitandao ya kijamii unaichukuliaje?

Ni sehemu ya kupotezea muda na mawazo baada ya kutemmbea sana kusambaza CV?

Mwanachuo ambaye bado upo hapo chuoni unasoma, hii mitandao ya kijamii kwako unaionaje? Je unaiona kama huyo graduate hapo juu anavyoiona au unalo jicho la tofauti?

Mfanya Biashara vipi kuhusu wewe mtazamo wako kuhusu mitandao ya kijamii ukoje?

Ni baadhi ya maswali tu ambayo yanaweza saidia katika kufanya tathmini fupi juu ya mtazamo wako kuhusu mitandao ya kijamii.

Sasa naomba nikupe siri hii wewe mkuu unayesoma hii post,

Mitandao ya kijamii ni Dili ambalo Ukiweza kufahamu njia sahihi ya kuitumia unaweza hifadhi vyeti vyako kwenye makabati na badala ya wewe kutafuta kazi, waajiri watakutafuta wewe wakupe kazi.

Soma kwa kutafakari na ruhusu akili yako kuelewa hayo maneno hapo juu.

Kabla ya kuingia mtandaoni jiulize nini utaenda kufanya mtandaoni.

Ebu Fikiria, unaweka bando lako, unafungua Facebook, Instagram au Jamii Forum halafu unaingia kutazama tu vitu mpaka bando linakata.

Halafu unatafuta tena pesa unaweka bando lingine kurudi kufanya vilevile ulivyo fanya mwanzo.

Na katika harakati zako zote hizo kukimbia kimbia Instagram mara Facebook, hujakaa Sawa upo Twitter na kabla ya kutulia unakumbuka nyuzi za MMU unarudi Jf.

Hakuna hata Mia unaingiza, na hakuna mtu yoyote unaye gusa maisha yake huko mtandaoni.

Kiufupi unaishi ndani ya MATRIX (Gereza huru) pasipo kujua.

Ebu jaribu kutafakari muenendo wako mtandaoni halafu kaa ujiulize naweza kufanya nini na bando langu na kufikia malengo yangu katika maisha kwa kutumia mtandao.

Unataka connection? Kujenga ujuzi? Kujenga biashara yako kuwafikia watu wengi? Kuongeza maarifa yako?

Aisee hii mitandao ya kijamii imejaa majibu yote hayo.

Amka, halafu Usione uvivu kutafuta watu wanaoweza kukusaidia kufikia hayo malengo yako mtandaoni.

Ni hayo tu mkuu.

Imeandaliwa na Mr. Purpose 0752026992.

Tuambie namna gani mitandao ya kijamii imekunufaisha au kukupotezea muda. Andika tujifunze zaidi.
 
Mitandao ya kijamii ujue kwanza umelenga nini.
Mimi niliamua kulenga wafanyabiashara wa kati. Nikaamua kukomaa na instagram username @kelvinkibenje huko nikajitifautisha badala ya kuweka motivation kama watu wengi wanavyofanya mimi nikawa naweka mafundisho ya biashara hasa mbinu za kuongeza mauzo na mbinu za masoko.

Baadae nikaanza kufundisha watu kuagiza bidhaa nje ya nchi kama vile China, Uturuki na Dubai. Nikaanza kuona baadhi ya watu hawamufu kuagiza wenyewe, nikaanza kuwa inaelekeza watu machimbo ya bidhaa Kariakoo bei nafuu/jumla.

Hapa sasa hivi account ina zaidi ya followers 90K ambao wote ni wafanyabiashara. Nauza course na vitabu E book za biashara. Kifupi nimesaidia wengi maana watu wengi wanakosa taarifa sahihi hivyo nawapa taarifa sahihi. Napiga pesa sana lakini zinatoka kwenye kusaidia watu.

Mtandaoni ujue nini unataka, tatizo vijana wengi wanakomaa na udaku na kucheza muziki huko ili kuvuta followers kumbe wanaatract followers with low purchasing power MWISHO wanaishia Kupata pesa elfu kumi kumi za matangazo.

Kiufupi mtandaoni kuna pesa, ujue nini unataka, jionyeshe wewe ni mtaalam, tatu tatizo fulani, tangulia kusaidia watu, kuwa mbuni na fanya kwa muendelezo.

Pitia page yangu huko kwa jina la @kelvinkibenje uibe tips
 
Mitandao ya kijamii ujue kwanza umelenga nini.
Mimi niliamua kulenga wafanyabiashara wa kati. Nikaamua kukomaa na instagram username @kelvinkibenje huko nikajitifautisha badala ya kuweka motivation kama watu....
Huwa nakufuatilia sana mkuu kuanzia LinkedIn hadi Instagram.

Unafanya kazi kubwa sana na ni mfano mzuri wa kuigwa.

Ukiwa na malengo thabiti na nia ya kweli hakuna kitu utashindwa kukipata mtandao.

Muhimu tu uelewa kwanini unafanya.

Be blessed brother Kelvin.
 
Instagram ni muhimu sana kwangu

My business highly depends on clients from Instagram

Kwa products zangu Nikilipia tangazo moja tu simu zinaita,dm kama zote Chap tu Nakua out of stock
 
Instagram ni muhimu sana kwangu

My business highly depends on clients from Instagram

Kwa products zangu Nikilipia tangazo moja tu simu zinaita,dm kama zote Chap tu Nakua out of stock
Hii ni moja ya ushuhuda mzuri sana mkuu.

Bila shaka wengine watajifunza kitu.

Ushauri: kama unafanya biashara ambayo unategemea kuifanya maisha yako yote, Epuka kutegemea platform moja tu.

Ongeza platform zingine mbili au tatu kisha, endelea kukomaa na hii moja ambayo inalipa wakati huo hizi zingine pia zinakua taratibu.
 
Point yako ni ya msingi mkuu

Ila Kwangu mimi Instagram ndo inanipa instant results lakini pia natumia platform nyingine,kama nyingi tu hata hapa jamiiforum napatumia pia mkuu
 
Point yako ni ya msingi mkuu

Ila Kwangu mimi Instagram ndo inanipa instant results lakini pia natumia platform nyingine,kama nyingi tu hata hapa jamiiforum napatumia pia mkuu
Kwa hali hiyo basi upo katika nafasi nzuri. Tuendelee kupambana mkuu.
 
Baada ya Mungu ni Google.
Google ndie Mwalimu Tosha uhitaji kupoteza mda darasani unakaririshwa.
Maarifa yote, shule zote zipo google
Nakubaliana na wewe mkuu.

Unaweza kuwa mtu hatari sana kama Ukiweza kutumia Google kujifunza vitu na kufanya kwa vitendo mpaka kupata matokeo.

Ulimwengu wa sasa Shule zetu hizi za kawaida zinaenda kupoteza thamani.

Ulimwengu unahitaji wajuzi.
 
Mimi mashine zote nikihitaji naingia youtube tu napata michoro na vipimo vyote.
Kitu cha kukaa darasani miaka youtube ni bando lako tu mb zikiisha tu na ushaelimika.
Thus wenzetu wameshatoka mfumo wa kupimwa kwa vyeti.
We ni mtaalamu " kamata chombo hicho" Test ya vitendo
 
Pia mitandao ya kijamii imenisaidia kupata siri nyingi Sana za Dunia na vilivyomo ikiwemo mbinu na maarifa ya kuzishinda nguvu za giza, hazinisumbui
 
Na hii ndiyo njia nzuri ya kupima uwezo wa mtu.

Siyo vyeti, ila mpe kazi afanye alete matokeo.
 
Pia mitandao ya kijamii imenisaidia kupata siri nyingi Sana za Dunia na vilivyomo ikiwemo mbinu na maarifa ya kuzishinda nguvu za giza, hazinisumbui
Ulimwengu wa sasa kila kitu kimewekwa wazi.

Yaani hakuna kitu kitakuwa siri milele, kuna muda kitajulikana tu.
 
LinkedIn ndo mpango mzima nimefahamu mambo mengi husasani katika career pia kule fursa zipo kimataifa yaani ukiwa labda ni mtu poa unashare mambo ya maana unashangaa unapendwa automatically na kupata fursa .. weirdly ule mtandao bongo hauna watu wengi
 
Upo sahihi mkuu.

Kibongo bongo LinkedIn inaogopwa sana sijui tatizo ni lugha au aina ya watu waliopo.

Ila ukijitoa akili ukazama mzima mzima na kuanza kushare na watu vitu vya maana, ni kweli unapata connections za maana sana.
 
Back
Top Bottom